Wakimbizi Nchini Marekani Wadumisha Tamaduni za Kimuziki kwa Nyimbo za Watoto

Marta Sam sings with a classroom of four-year-olds. Credit: Erika Beras

Marta Sam akiimba kwenye darasa lenye watoto wenye umri wa miaka minne. PICHA: Erika Beras

Simulizi hili lililosimuliwa na Erika Beras awali lilionekana kwenye mtandao wa PRI.org mwezi Mei, 2016. Limechapwa hapa kama sehemu ya ushirikiano baina ya PRI na Global Voices.

Marta Sam amezungukwa na watoto wachangamfu wenye umri wa miaka minne. Anafanya kazi kwenye kituo cha kulea watoto kinachojulikana kama St. Martin kilicho kwenye mji wa Erie, Pennsylvania, anawasaidia watoto namna ya kuimba na kucheza.

Sam anaweza kuimba kwa Kiarabu, na Kiingereza. Akiwaelekeza watoto kuimba wimbo wa Kikongo, kisha anawaongoza kuimba wimbo wa “Five Little Monkey Jumping on The Bed”  [Nyani Watano Wadogo Wakiruka Kitandani]. Watoto huiga anayoyafanya huku wakicheza na kutaja majina ya baadhi ya nyimbo wazozipendelea. Ni hali ambayo Sam ameizoea .

“Wanaponiona darasani huwa wanasema, ‘Dada Marta Je, tunaweza kufanya hivi? Dada Marta Je,tunaweza kuimba wimbo huu? Dada MartaJe,tunaweza kuruka?'” na huwa nawajibu. “Ndiyo, Halafu nitaruka pamoja nao na kuwa kama mtoto mwenzao — ukifanya kazi na watoto huna budi kujishusha na kuwa kama wao  … fanya nao fujo.”

Sam,mwenye miaka 59, ni muelimishaji anayezungukia kituo hichi maarufu cha kulelea watoto cha St. Martin. Hupitia chumba kimoja baada ya kingine akiimba nyimbo tulivu za sansuri kuwafanya watoto walale. Asili yake ni Sudani ya Kusini, alikuja mjini Erie miaka 13 iliyopita ikiwa ni kundi la kwanza la wakimbizi  waliopewa ardhi katika mji huu mdogo uitwao Rust Belt .

Alifanya kazi katika kiwanda cha plastiki na akaanza kujifunza lugha ya kiingereza. Ndipo aliposikia nafasi ya kazi katika kituo cha kulea watoto. Kwa upande mwingine angeweza kushiriki  nao nyimbo za asili alizowahi kuwaimbia watoto wake wakati wakiwa bado wadogo.

Hilo ndilo lilikuwa tamanio lake.

“Oh, kwa kweli ilibadilisha maisha yangu sana. … na mimi sasa najisikia kuwa mtu,” anasema.

Sam anafanya kazi katika kituo hiki cha St. Martin kwenye kipindi kiitwacho  Old Songs, New Opportunities [Nyimbo za Zamani, Fursa Mpya] programu  iliyokuwa ni ndoto ya Kelly Armor, msimuliaji na  muelimishaji katika sehemu ya makumbusho ya sanaa ya Erie. Armor amtokea mjini Erie, lakini muda mwingi  kwenye miaka ya 1980 alisomea nyimbo za asili nchini Kenya na Tanzania. Alipotambua uwepo wa wakimbizi katika sehemu hii ya Erie miaka ya karibuni, akapata wazo.

“Ya kwamba inawezekana … wanawake hawa wakimbizi wangependa kufanya kazi na watoto wadogo? Na hivi Je, kuna uwezekano wanawake hawa wakawa wanajua nyimbo nyingi za asili na  pia namna ya kuzitumia nyimbo hizo hasa wakiwa na watoto?” akafikiri.

Ikatokea kweli wakafanya hivyo na katika mazingira fulani nyimbo zilikuwa ni kitu pekee walichoweza kuizawadia Marekani. Hiyo ilitokea kwa Victoria Angelo, ambaye pia asili yake ni Sudani ya Kusini.

“Sikuwa na uwezo wa kuleta chochote. Sio sahani, hakuna kitu, wala [nguo],” anasema. “Kitu pekee nilichowaletea ni nyimbo.”

Lakini pia kwa upande wa pili nyimbo ziliwakilisha kila kitu ambacho hatukuleta.

“Ni katika hali ya kuonyesha hisia zetu, furaha yetu, huzuni yetu, vita inayoendelea huko tulikokimbia, kuelezea misimu, wakati wa mvua za masika , wakati wa kiangazi,” anasema.

Victoria Angelo and some of the toddlers she works with. Credit: Erika Beras

Victoria Angelo akiwa na baadhi ya watoto wanaojifunza kutembea katika sehemu yake ya kazi. Picha: Erika Beras

Muelimishaji kupitia simulizi za mdomo, Armor, aliwekeza kuwapa ujuzi wanawake kama  Angelo na Sam ili waweze kuajiriwa katika kituo hichi cha kulea watoto. Kisha, kama alivyofanya huko Afrika, akazikusanya nyimbo zao na kuzitafsiri.

Kuunganisha ujuzi wa kikazi na  and tamaduni za kimuziki imekuwa kazi yenye mafanikio kwa kiwango kikubwa, kakika sehemu ya makumbusho walitoa CD. Angelo akiimba baadhi ya nyimbo, moja ya nyimbo hizo ni kama ule waaacholi wanaouimbaga watto wanapofikia umri wa kujifunza kutembea.

“Ni njia ya kumuita mtoto atembee kukufuata mahali na pia unamwimbia mtoto ageuke upande wa mtu mwingine ambaye nae atamwimbia amfate,” Armor akilezea.

Nchini Marekani, baadhi ya nyimbo nyingi maarufu za watoto asili ya ni nchi za nje — fikiria  “Daraja la London likivunjika ” au “Ring Around The Rosie.” Lakini kila nchi na utamaduni zina nyimbo za aina hii, na uhamiaji wa watu pamoja na mazoea, ni baadhi ya vitu ambavyo tunaweza kuvipoteza — au kuvipata.

Armor amefanikiwa kupata takribani nyimbo mia moja kutoka nchi nyingi na tamaduni mbalimbali. Zinagusa  vitu vyote — wanyama, hisia, uzoefu.

Wimbo mmoja wakinepali maudhui yake ni kupanda wakati wa mapumziko kutungua embe liliyoiva.

“Lakini mwisho wa wimbo huu kengele inagongwa bila kufanikiw kupata embe,” she anasema”Naifikiria hali hiyo kama ya, pale unapokwenda kuna ukweli wenyewe. Mapumziko hayawezi kuwa kipindi kirefu cha  kutosha. Na wakati mwingine unaweza hata usipate muda wa kilila embe hilo.”

Hii hapa ni orodha ya nyimbo kwenye CD iitwayo “Simba La La: World Music for Children,” jina la CD hiyo kwa hisani ya Makumbusho ya Sanaa ya Erie.

Wimbo huu unakihusu kiumbe kiitwacho kipepeo wa kijani, kinachopatikana Asia ya Kusini. Kwa upendo unaelezea namna kipepeo kikiruka baadae kutangaza kwamba kuruka huwa bora zaidi pale kinapokuwa nje:

 

Watoto wa Kongo wanapoimba wimbo huu, huwa wanapiga makofi upande mmoja wa kichwa:

Wimbo huu unafanana na wimbo maarufu wa zamani uliopenda na watoto uitwao “I’m A Little Teapot” [Mimi ni birika dogo la chai]:

Tafrsiri ya wimbo huu imewekwa na watu wa kituo cha kulea watoto cha Erie kumwezesha mtoto kuelewa:

 

 

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.