Habari kuhusu Togo
Mtazamo wa Tamasha la Kwanza la WanaBlogu na Vilogu wa Barani Afrika Lililofanyika Huko Dakar, Senegal
Kwa siku mbili, wanablogu na wanavilogu maarufu barani Afrika, wakiambatana na wadau kadhaa wa teknolojia barani Afrika walikuwa na majadiliano ya namna ya kuboresha kazi zao
Baada ya Maandamano Burkina Faso na Burundi, Naija na Togo Zinafuata?
Wanaija 20,000 wameingia mitaani mjini Niamey, Naija mnamo Juni, 6. Kuna ababu nyingi za maandamano hayo: umaskini uliokithiri, utawala mbovu na kubanwa kwa uhuru wa kujieleza yakiwa ni moja wapo ya malalamiko ya asasi za kiraia nchini humo. Maandamano kama haya yalitokea katika nchi za Burkina Faso, Burundi na Togo....
2015 Mwaka wa Kufanyika Chaguzi Huru na Haki Barani Afrika
Wekesa Sylvanus anataraji kwamba 2015 utakuwa mwaka wa chaguzi huru na haki barani Afrika: https://wekesasylvanus.wordpress.com/2015/02/18/will-2015-be-a-year-of-free-and-fair-elections-in-africa/ Tangu kurejeshwa kwa mfumo wa demokrasia ya vyama vingi barani Afrika, ushindani nyakati za uchaguzi umekuwa suala la kufa na kupona kwenye nchi nyingi za ki-Afrika. Chaguzi barani Afrika ni suala lenye hatari zake na...
Wanabogu wa Togo Wamtania Rais Kufuatia Ujumbe wa Bango Barabarani
Mtu mmoja alitaka watu wajue kwamba alikuwa na shukrani kwa ukarimu wa Rais wa Togo Faure Gnassingbé. Wiki hii, bango kubwa liliwekwa jijini Lomé, Togo kusifia kitendo cha Rais kutoa chakula cha mchana kwa watoto. Bango hili linaloonekana hapa chini lina maneno haya kwa lugha ya Kifaransa:” Asante sana Baba Faure...
Mradi Mkubwa wa Reli Kati ya Mji wa Niamey na Cotonou Kuanza
Mradi wa reli wa urefu wa kilometa 1,500 kati ya Niamey, mji mkuu wa Niger na Cotonou, mji mkuu wa Benin umepitishwa na mamlaka ya nchi hizo mbili na ujenzi utaanza Machi 2014 [fr]. Francois Ndiaye katika Niamey anaelezea kuhusu makubaliano ya fedha [fr] inayojumuisha wadau mbalimbali na itasimamiwa na kundi la uwekezaji...
Togo: Muhubiri Asafirisha Kilo 4.2 za Madawa ya Kulevya Yaliyofichwa kwenye Pipi ‘k Build Church
Muhubiri wa Injili raia wa Togo, Woegna Yao Koufoualesse alikamatwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Accra akiwa na kiasi cha kilo 4.2 za madawa ya kulevya aina ya Cocaine akiwa kwenye safarini kutokea Sao Paulo, chapisho la Afrique Infos linaripoti [fr]. Madawa hayo yalikuwa yamefichwa ndani ya peremende za...
Togo Yaondolewa Kwenye Mashindano ya Kombe la Afrika baada ya Shambulizi Baya
Timu ya Taifa ya Togo sasa imeondolewa rasmi kutoka kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kufuatia shambulizi lililoelekezwa kwa msafara wa timu hiyo Ijumaa iliyopita katika eneo la Kabinda lililo nchini Angola na ambalo liko kwenye ukanda wa mapigano baina ya vikosi vya serikali na vile vya waasi wanaotaka kujitenga. Huku kukiwa na shutuma nyingi kutoka kwenye serikali ya Angola na maafisa wanaosimamia soka barani Afrika, wanablogu wa Ki-Togo wanauliza maswali magumu kuhusu msiba huo.
Togo Yafuta Adhabu ya Kifo
Bunge la Taifa la Togo limepiga kura ya kukomesha adhabu ya kifo na kuifanya nchi hiyo kuwa mwanachama wa 15 wa Umoja wa Nchi za Afrika kuipiga marufuku adhabu hiyo.