Togo Yafuta Adhabu ya Kifo

Bunge la Taifa la Togo limepiga kura ya kukomesha adhabu ya kifo na kuifanya nchi hiyo kuwa mwanachama wa 15 wa Umoja wa Nchi za Afrika kuipiga marufuku adhabu hiyo.

Japokuwa adhabu ya kifo imekuwa ikitolewa kwa ajili ya makosa hadi kufikia mwaka 2003, Togo haijawahi kuitekeleza adhabu hiyo tangu mwaka 1978.

Ephrem L anaandika katika tovuti ya togosite.com:

Le Togo vient d'inscrire son nom dans le livre d'or des pays ayant aboli “la peine de mort” dans leur législation pénale. La solennité, l'enthousiasme et l'unanimité qui a entouré ce vote nous fait penser que les togolais peuvent ensemble faire de grandes choses pourvu que la volonté y est. Ce fut une victoire collective hier au parlement.

Togo imeandika jina lake katika kitabu cha dhahabu kwa kuifuta adhabu ya kifo katika kitabuchake cha sheria za adhabu. Taadhima, shauku na uamuzi usiopingika vilivyomabatana na kura hii vinatufanya tufikiri kuwa watu wa Togo wanaweza kufanya mambo mengi makubwa kwa pamoja, kama wakiwa na nia. Kilichotokea jana bungeni kilikuwa ni ushindi wa pamoja.

Une question non moins importante aussi et qui est celle de l'IMPUNITE doit également faire l'objet d'une attention particulière. Elle doit être combattue sans concession pour le triomphe des droits de l'homme et des libertés individuelles et collectives. C'est à ce prix que la réconciliation sera possible.

Suala jingine la muhimu ni lile la KUTOKUFUATA SHERIA, ambalo linahitaji kuangaliwa kwa makini zaidi. Linatakiwa kupiganiwa ili kufanikisha ushindi wa haki za binaadamu na uhuru binafsi kadhalika uhuru kwa wote. Suluhisho linawezekana tu kwa gharama hii.

Msomaji katika tovuti ya LePost.fr anaandika:

Merci Animariio….Le TOGO…bravo…………………..bon et bien Monsieur OBAMA,
à vous !!!!

Ahsante Animariio… TOGO… Hongera…………. Na sasa Bw. Obama, zamu yako imefika!!!!

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.