Wanaija 20,000 wameingia mitaani mjini Niamey, Naija mnamo Juni, 6. Kuna ababu nyingi za maandamano hayo: umaskini uliokithiri, utawala mbovu na kubanwa kwa uhuru wa kujieleza yakiwa ni moja wapo ya malalamiko ya asasi za kiraia nchini humo. Maandamano kama haya yalitokea katika nchi za Burkina Faso, Burundi na Togo. Serikali iliachia ngazi nchini Burkina Faso wakati uchaguzi ukiahirishwa nchini Burundi. Mwezi Mei, wananchi wa Lome waliandamana kupinga matokeo ya urais yaliyompa ushindi rais Faure Gnassingbe aliyeshinda kwa muhula wa tatu.