Mtu mmoja alitaka watu wajue kwamba alikuwa na shukrani kwa ukarimu wa Rais wa Togo Faure Gnassingbé. Wiki hii, bango kubwa liliwekwa jijini Lomé, Togo kusifia kitendo cha Rais kutoa chakula cha mchana kwa watoto. Bango hili linaloonekana hapa chini lina maneno haya kwa lugha ya Kifaransa:” Asante sana Baba Faure kwa chakula cha mchana kwa wanafunzi/a>”. Raia wa Togo waliguswa na kuvutiwa na ujumbe huo. Waliingia kwenye mtandao wa Twita kuchekeshana kuhusiana na bango hilo na kutengeneza alama habari #merciPapaFaure (Asante sana Baba Faure).
Bon, et si on lançait le hashtag #MerciPapaFaure pour rire un peu? #gnadoe @Nounfoh @AphtalC @teteenyon @liebeBAT pic.twitter.com/gjq030YkRw
— Kelly Adediha (@KellyGeek) September 11, 2014
Sawa, vipi cheka kidogo na alama habari #mercipapaFaure ?
Picha hiyo juu imesambaa mno kwenye mtandao wa Twita. Adzima anatoa maelezo kidogo kuhusu hali ya mambo ilivyo kwa watoto wa Togoshuleni.