Togo Yaondolewa Kwenye Mashindano ya Kombe la Afrika baada ya Shambulizi Baya

Timu ya Taifa ya Togo sasa imeondolewa rasmi kutoka kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kufuatia shambulizi lililoelekezwa kwa msafara wa timu hiyo Ijumaa iliyopita katika eneo la Kabinda lililo nchini Angola na ambalo liko kwenye ukanda wa mapigano baina ya vikosi vya serikali na vile vya waasi wanaotaka kujitenga.

Wachezaji wa timu ya Taifa ya Togo kabla ya mashindano ya utangulizi huku Biberach/Riss siku chache kabla ya Mashindano ya Kombe la Dunia (Chanzo: Wikipedia)

Wachezaji wa timu ya Taifa ya Togo kabla ya mashindano ya utangulizi huku Biberach/Riss siku chache kabla ya Mashindano ya Kombe la Dunia (Chanzo: Wikipedia)


Kocha msaidizi na ofisa wa habari wa timu waliuwawa na mlinda mlango, Kodjovi “Dodji” Obilale, alijeruhiwa vibaya sana. Hata hivyo, imeripotiwa kwamba hali ya Obilale sasa imetengemaa baada ya kufanyiwa upasuaji nchini Afrika ya Kusini, ingawa bado anaendelea kupumua kwa kutumia mashine maalumu ya kusaidia upumuaji.

Kundi la waasi linalojulikana kwa jina la FLEC na ambalo limedai kuhusika na shambulizi hilo lilieleza kwenye taarifa yake kwamba wao walikuwa wamelenga kushambulia msafara wa polisi na si timu ya wachezaji ya Togo. Kwa upande wake, serikali ya Angola, imeelezea kwamba shambulizi hilo limetokea “kwa bahati mbaya” na kwamba inazihakikishia timu nyingine usalama. Hivi sasa mechi zinaendelea kama zilivyopangwa huko kwenye jimbo la Kabinda.

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, wachezaji walionyesha nia ya kutaka kuendelea na mashindano, lakini serikali ya Togo iliamua kuirudisha nyumbani timu hiyo siku ya Jumamosi. Togo ambayo ilikuwa icheze dhidi ya Ghana mapema leo, imeondolewa rasmi kwenye mashindano baada ya kushindwa kutokea uwanjani.

Tangu kutokea kwa shambulizi hilo, wananchi wengi wa Togo wamekuwa wakiuliza maswali magumu kuhusu msiba huo ambao pengine ungeweza kuepukika: Kwa nini timu hiyo ilisafiri kwa basi na si kwa ndege? Je, nini hasa ilikuwa nia ya serikali ya Angola kuchagua kuendesha mashindano hayo katika jimbo la Kabinda, je, ilikuwa kwa nia ya kuonyesha kwamba imewashinda waasi? Je, hivi, mchezo wa soka una manufaa makubwa ya kusababisha mtu ujiweke kwenye hatari ya msiba kama huo? Je, mashindano hayo yafutiliwe mbali?

Je, mashindano yaendelee?

Mara baada ya shambulizi hilo, kulizuka mjadala mkubwa wa mtandaoni kuhusu kama timu ya Togo ijitoe au la. Rêve d'Afrique, ambayo ni blogu ya raia wa Togo na mwandishi Gerry Taama alijenga hoja zake kwamba mchezo uendelee:

A la seule condition que la CAN soit annulée (les autres équipes décidant de boycotter l’évènement), nous devons jouer ce match…Nous devons être à cette CAN, pour occuper notre place, pour honorer nos morts, leur dire combien nous les aimons, et combien nous leur montrons que refusons que leur mort soit vaine. Jouer pour ne pas laisser les terroristes nous vaincre, pour ne pas laisser la barbarie l’emporter sur le droit et nos valeurs. Refuser de jouer, c’est capituler…

Labda kama Kombe la Mataifa ya Afrika litafutiliwa mbali (timu nyingine ziamue kususia mashindano hayo), vinginevyo sisi tushiriki kwenye mchezo huu…Hatuna budi kushiriki katika mashindano haya, kuingia kiwanjani ili kuwakumbuka waliokufa, kuelezea upendo wetu kwao, na tuonyeshe kwamba vifo vyao havikuwa bure. Tushiriki ili kuwaonyesha magaidi kwamba hawakushinda, tusiruhusu ushenzi kushinda sheria au yale tunayoyapa thamani. Kama tukikataa kushiriki basi tutakuwa tumekubali kushindwa…

Yipka-Au Village yeye hakubaliani:

Comment est-ce qu’ont espere qu’ils jouent au foot apres avoir echappe belle a la mort en essayant d’aller jouer au foot, et aussi avec deux joueurs et des entraineurs et medecins gravement blesses??

Je, tunawezaje kutumaini kwamba watacheza mara tu baada ya kuwa wamenusurika na kifo, tena huku wachezaji wawili, makocha na madaktari wakiwa wamejeruhiwa vibaya??

Kwa upande wake, Kangi Alem, anakubali na anaongeza kusema kwamba Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ya mwaka 2010 yafutwe:

La CAF porte une responsabilité dans le fait d’avoir fait passer les joueurs togolais dans une enclave réputée dangereuse, elle doit maintenant prendre ses responsabilités en annulant la CAN 2010! C’est mon sentiment, antisportif peut-être, mais c’est mon sentiment.

Shirikisho la Soka Barani Afrika, CAF, linawajibika. Liliruhusu wachezaji kupita katika eneo linalofahamika kwamba ni la hatari, kwa hiyo ni haki kabisa kuwajibika kwa kuyafuta mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afika ya mwaka 2010! Hayo ni maoni yangu, labda kidogo yako kinyume na uanamichezo, lakini hayo ndiyo maoni yangu.

CAF limedai kwamba halikuwa na taarifa na mpango wa safari wa timu hiyo na kwamba daima limekuwa likizishauri timu kusafiri kwa ndege. Alem anaona kuwa hiki ni kama “jambo la ajabu” maana timu hiyo ilisindikizwa na kikosi cha askari waliobeba silaha, yote kwa hisani ya serikali ya Angola.

Kwa nini mashindano yaendeshwe katika jimbo la Kabinda?

Bila shaka hili ni swali kubwa kwamba hivi kwa nini mashindano yafanyike katika jimbo la Kabinda awali ya yote. Yikpa anaandika:

Je pense que c’etait une decision politique de l’Etat Angolais cautionne par la CAF d’organiser des matchs dans cette region de la Cabinda pour prouver qu’il y a securite dans cette region riche en petrole afin d’attirer les investisseurs etrangers dans cette region. Alors cette attaque viens de prouver le contraire.

Nafikiri huo ulikuwa ni uamuzi wa kisiasa kwa upande wa serikali ya Angola huku CAF wakiunga mkono kwamba mashindano yafanyike katika jimbo la Kabinda ili kuudhihirishia ulimwengu kwamba eneo hilo, ambalo lina utajiri mkubwa wa mafuta, lilikuwa salama kiasi cha kutosha kuvutia wawekezaji kwenda huko. Shambulizi hili limethibitisha vinginevyo.

Paul Archer, akiandika maoni yake kwenye makala ya Alem, anasema:

Il faut jouer, c’est la vie! les rebelles sont chez eux,je ne les approuve pas mais un terrain de guerre est un terrain de guerre.

Walikuwa kwenye eneo lililo chini ya waasi. Sikubaliani na jambo hilo, maana uwanja wa vita ni uwanja wa vita.

Michezo & Msiba

David Kpelly, aliyeandika kwenye blogu ya Alem, alikumbusha kwamba tukio hilo halikuwa la kwanza katika michezo kuhusishwa na vitendo vya utumiaji nguvu au mashambulizi, hasa katika mchezo wa soka. Mnamo mwaka 2007. Jumla ya viongozi wa michezo na washabiki 13, akiwemo Waziri wa michezo, waliuwawa nchini Sierra Leone, katika ajali ya helikopta. Pia anakumbusha kwamba baada ya mechi ya kufuzu kati ya Togo na Mali kwa ajili ya Kombe la Afrika la mwaka 2006, raia kadhaa wa Togo waliuwawa jijini Bamako. Vilevile anakumbushia juu ya tukio lililotokea katika uwanja wa Kegue jijini Lome ambapo washabiki kadhaa wa soka walikufa, yote hiyo ni ukiachia mbali tukio la hivi karibuni zaidi lililotokea nchini Ivory Coast ambapo watazamaji 19 walikufa kutokana na kukanyagana. Anahitimisha:

Sur le plan africain, le foot, toujours lui, ne fait pas moins de victimes…Bon Dieu! le foot fait trop de victimes!

Barani Afrika, soka, ndiyo soka, … Mungu wangu! Mchezo wa Soka husababisha wahanga wengi mno!

Katika maoni yanayotaka kufanana na hayo, msomaji mwingine, Sami, anajiuliza kama endapo vurugu ambazo mara nyingine huambatana na michezo, “Michezo maarufu ambayo huchochea hisia za utaifa ambazo bado ni za kijima kabisa, je, hizi si viwanja vya vita vilivyojificha”.

Mchezo unaendelea

Felix Makayaba, ambaye alitoa maoni yake katika Reve d'Afrique, anaomboleza hisia kwamba wakati Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika yakiendelea, ulimwengu, na hata watazamaji kule Togo, tayari wamekwishasahau msiba huo:

En effet, tant que la CAN continue, il y'aura une ambiance festive partout au Togo. Et ala douleur de la mort des nôtres rique d'être occulté pour laisser la place au football. J'ai pour preuve les cris qde joie qui fusent de tout de Lomé du seul fait de l'égalisation des 4 buts par l'équipe du Mali. Déjà les Loméens se mettent dans la peau de leurs frères Maliens…Déjà nos morts d'Angola, sans avoir encore été inhumés nous occupent de plus en plus moins.

Wakati Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika yakisonga mbele, kutakuwa na shamrashamra za mashangilio kila mahali nchini Togo. Na yale maumivu ya vifo vya baadhi yetu yakiwa katika hatari ya kufunikwa na soka. Nina ushahidi, kelele za furaha zilizorindima huko Lome mara tu baada ya magoli 4 yaliyoletwa na timu ya Mali. Tayari wakazi wa Lome wameanza kujiweka katika nafasi ya ndugu zao wa-Mali… Tayari tumeanza kutojihangaisha na wenzetu waliofia kule Angola, yaani hata kabla hawajazikwa.

Pengine ni kutokana na asili ya binadamu kwamba licha ya kupata hasara kubwa, maisha bado huendelea. Fasokan anaelezea hisia za shamrashamra zilizotawala jiji la Bamako hivi karibuni kabla ya mechi kati ya Mali na Angola (ambayo ilimalizika kwa suluhu ya 4-4).

Ce soir, le Mali joue contre l’Angola, C’est un grand évènement aujourd’hui au Mali et on le sent partout à travers le drapeau malien accroché aux motos, aux vélos, aux voitures, sur les hangars et les toits par les supporteurs. C’est le seul grand sujet à la Une partout à Bamako.

On voit des hommes habillés en vert, jaune, rouge et certaines femmes attacher le drapeau malien autour de la tête comme foulards pour dire aux Aigles du Mali que tout le monde est derrière eux.

Leo usiku, nchini Mali, tunashindana na Angola. Ni tukio kubwa hapa Mali na unaweza kulihisi kila mahali hasa kwa kushuhudia bendera ya Mali ikipepea kwenye pikipiki, baiskeli, magari na katika paa za vibanda na nyumba za watu wanaotushabikia.

Unaweza kuwaona watu waliovalia kijani, njano na nyekundu, huku baadhi ya wanawake wakiwa wamejifunga bendera ya Mali vichwani mwao kama vilemba, na yote hii ni kuipelekea ujumbe timu ya Taifa ya Mali ya Eagles kwamba wana uungaji mkono mkubwa nyuma yao.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.