Mradi Mkubwa wa Reli Kati ya Mji wa Niamey na Cotonou Kuanza

Mradi wa reli wa urefu wa kilometa 1,500 kati ya Niamey, mji mkuu wa Niger na Cotonou, mji mkuu wa Benin umepitishwa na mamlaka ya nchi hizo mbili na ujenzi utaanza Machi 2014 [fr].  Francois Ndiaye katika Niamey anaelezea kuhusu makubaliano ya fedha [fr] inayojumuisha wadau mbalimbali na itasimamiwa na kundi la uwekezaji la Bolloré [fr]. Benoît ILLASSA mjini Cotonou anashangaa kwa nini vikundi binafsi vya kuwekeza kutoka aidha Niger au Cotonou havikuchaguliwa kuelekeza miradi hiyo.Bajeti ya makadirio imewekewa kati ya mabilioni 100 za CFA (takribani dola bilioni 2). Reli lazima iendelezwe siku zijazo kwa miji mitatu mingine mikuu ya mkoa Afrika Magharibi: Abidjan, Ouagadougou na Lomé.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.