Mtazamo wa Tamasha la Kwanza la WanaBlogu na Vilogu wa Barani Afrika Lililofanyika Huko Dakar, Senegal

oster du Festival Africain des Blogueurs et Youtubeurs FABY via Armelle avec permission

Bango la Tamasha la WanaBlogu na WanaVilogu kutoka kwa Armelle. Imetumiwa kwa ruhusa yake

Armelle Nina Sitchoma aliripoti  katika tamasha la kwanza la Waafrika wanao miliki Blogu na Vilogu lililofanyika tarehe 3-5 Juni 2016 (FABY, ikiwa ni kifupisho chake katika lugha ya Kifaransa), lililofanyika huko Place du Souvenir mjini Dakar, Senegal.

Mwanablogu kutoka Douala, Cameroon, aliandika katika tovuti yake kuwa tamasha hilo la siku mbili lilivutia wanablogu na vilogu wa viwango vya juu kabisa wapatao 36 na wadau wengine wa masuala ya mitandao kutoka pande zote za Afrika. Wataalam hawa wa masuala ya mitandao walitoa mada mbalimbali zinazohusu  masuala ya mtandao barani Afrika na fursa za kiuchumi zinazopatikana katika mitandao hiyo ya Afrika.

Aliendelea kueleza kuwa:

Deux panels avec comme axe le « Big Data : Quelle place pour les contenus africains ? » modéré par Aboubacar Sadikh Ndiaye, Consultant web 2.0 et « La vidéo en Afrique : Quel avenir ? » modéré par Mountaga Cissé du Sénégal meubleront les deux jours d’échanges.

Les panels seront animés par des blogueurs et des youtubeurs de renom tels Edith Brou de la Côte d’Ivoire, Yassine Massouath du Maroc, Mountaga Cissé du Sénégal qui s’exprimeront sur la thématique « Comment réussir  sur internet ? Les possibilités de métier dans l’univers IT. » Annie Payep du Cameroun, Ameyaw  du Ghana, Alexandre Lette et NK Thiat du Sénégal animeront l’atelier sur « Quelle politique  pour un contenu de qualité ? »

Le deuxième jour du festival sera consacré à l’avenir de la vidéo en Afrique. Une meilleure visibilité sur le web passe nécessairement par une bonne connexion internet.  Merouane Boudiab de l’Algérie, El Oumar Diop du Sénégal et Aphtal Cissé du Togo tableront sur « Quelle stratégie pour une meilleure connectivité en Afrique ? » Produire une vidéo c’est bien. Gagner e l’argent à travers cette dernière c’est encore mieux. Comment gagner de l’argent et promouvoir ses vidéos sur YouTube? Les réponses à cette question seront données par Nancie Mwai du Kenya, Lamine Mbengue et Assane Mbengue du Sénégal.

Des exemples de réussite  sur le continent africain tels Aisha Dème de Agendakar seront présentés au public. Le FABY, 1ère édition, sera également un moment d’animation à travers les stands make up – fashion de Sylvia Njoki (Kenya), mode & beauté de Aba du Sénégal. La cuisine, les jeux vidéo, l’éducation et l’humour seront également de la partie.

Zilikuwa siku mbili za majadiliano zilizoandaliwa katika makundi mawili ya majadiliano: “Data Kubwa: Bara la Afrika lina nafasi gani? Kundi hili liliongozwa na mshauri wa Web 2.0 Aboubacar Sadikh Ndiaye, na Kundi lingine lilijadili mada, “Hatima ya Video  Barani Afrika” liliongozwa na Mountaga Cissé  kutoka Senegal.

Makundi haya ya majadiliano yalikuwa yameundwa na wanablogu na vilogu wengi maarufu kama vile Edith Brou wa Ivory Coast, Yassine Massouath kutoka  Morocco, na Mountaga Cissé kutoka Senegal. Mountaga Cisse aliongelea mada iliyokuwa na kichwa cha somo “jinsi ya kufanikiwa kupitia mtandao wa Intaneti: Nafasi za kazi katika Ulimwengu wa Teknolojia”  Wakati huo huo Annie Payep kutoka Cameroon, Ameyaw kutoka  Ghana, Alexandre Lette na  NK Thiat kutoka  Senegal waliongoza warsha iliyobeba dhima ya “Udhibiti Viwango”

Siku ya pili ya tamasha ilielekezwa katika kujadili hatma ya video Barani Afrika ambapo ilijadiliwa na kuonekana kuwa muonekano mzuri wa video katika tovuti inahitaji na kutegemea sana mtandao mzuri. Marouane Boudiab kutoka  Algeria, El Oumar Diop kutoka Senegal na Aphtal Cissé kutoka  Togo walijadili kuhusu  “Kuboresha Mtandao Barani Afrika”. Uzalishaji wa video bora ni vizuri, ila ni vizuri zaidi hata kuliko kupata fedha zitokanazo na video hizo. Unawezaje kupata fedha huku ukiitangaza video yako katika Vilogu? Swali hili lilijibiwa na Nancie Mwai kutoka Kenya akishirikiana na Lamine Mbengue and Assane Mbengue kutoka Senegal.

Masimulizi ya kufanikiwa kwa Waafrika kama ile ya Aisha Dème wa wavuti ya Agendakar, yalijadiliwa na kushirikishwa kwa hadhira. Pia kulikuwa na maonesho ya mitindo na upambaji kutoka kwa Sylvia Njoki wa Kenya na Mode & Beauté kutoka kwa Aba wa Senegal. Shughuli za mapishi, michezo, mijadala ya elimu pamoja na sanaa za vichekesho navyo pia vilipata nafasi katika tamasha hilo kubwa la kwanza Barani Afrika lililowashirikisha Wanablogu na Wanavilogu hao waliotoka sehemu mbalimbali humu Barani.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.