Habari kuhusu Msumbiji

Kampeni ya Mtandaoni ya Kudai Amani Nchini Msumbiji

Blogu ya Mozmaniacos [pt] imezindua kampeni ya mtandaoni ya kudai amani nchini Msumbiji, kufuatia tishio la kuhatarisha amani iliyodumu kwa miaka 20 . Kwa kutumia kiungo habari #MozQuerPaz (#MozWantsPeace), watumiaji wa Facebook, Twitter, na Instagram waanza kuchangia picha zao pamoja na maoni yao kuhusiana na kampeni hii.

Timu ya wanawake ya Mpira wa Kikapu ya Msumbiji Yafika Mbali

  29 Septemba 2013

Kufuatia ushindi wa kishindo kwenye mashindano ya robo fainali (tazama habari zetu ), yaliyofanyika usiku wa jana timu ya mpira wa kikapu ya Msumbiji, wanawake, ilishinda nafasi ya kuingia kwenye Fainali za Mashindano ya Afrobasket usiku wa leo dhidi ya washindi watetezi Angola. Kwa staili nyingine ya kurudi kwa ushindi...

Wafanyakazi wa Sekta ya Afya Nchini Msumbiji Wagoma Kudai Maslahi

  1 Juni 2013

Wafanyakazi wa sekta ya afya nchini Msumbiji wamekuwa katika mgomo uliodumu kwa siku kumi na kusababisha kusimama kwa huduma katika vitengo vingi vya kutoa huduma za afya kote nchini humo. Mgogoro wao na serikali umetokana na madai yao ya kuboreshewa maslahi na mazingira ya kazi pamoja na kurekebishwa kwa gharama za chumba cha wagonjwa mahututi katika mahospitali yote nchini humo.