Wafanyakazi wa Sekta ya Afya Nchini Msumbiji Wagoma Kudai Maslahi

Francisco J. P. Chuquela, anayefanya kazi na mshirika wa Global Voices @Verdade Newspaper nchini Msumbuji, aliripoti habari hii kwa ajili ya Global Voices

Wafanyakazi wa sekta ya afya nchini Msumbiji wamekuwa katika mgomo uliodumu kwa siku kumi na kusababisha kusimama kwa huduma katika vitengo vingi vya kutoa huduma za afya kote nchini humo. Mgogoro wao na serikali umetokana na madai yao ya kuboreshewa maslahi na mazingira ya kazi pamoja na kurekebishwa kwa gharama za chumba cha wagonjwa mahututi katika mahospitali yote nchini humo.

Huu ni mgomo wa pili katika sekta hiyo kufanyika nchini humo kwa mwaka 2013,  isipokuwa tu wakati huu mgomo wa madaktari umepanua wigo wake na kujumuisha wataalamu zaidi wa afya na umeendelea kwa juma la pili sasa.

Hisia za hasira zilipanda Jumapili usiku, Mei 26, 2013 wakati Rais wa Associação Medica de Moçambique, Daktari Jorge Arroz, alipokamatwa na polisi akishitakiwa kwa makosa ya uchochezi (kitendo cha kuonyesha kutoridhika au uasi dhidi ya serikali). Kuachiliwa huru kwa Arroz saa chache baadaye kulichochewa kwa kiasi kikubwa na uhamasishaji mkubwa wa watu mbele ya kituo cha polisi ikichangiwa pia na kuwepo kwa vyombo vikuu vya habari na hatua ya wanasheria kuingilia kati.

Tomás Queface, mwanafunzi wa sosholojia, alitoa muhtasari kwenye blogu yake [pt] aiitayo Política e tecnologia jinsi wananchi wa Msumbiji walipohoji haraka sana kwenye vyombo vya habari vya kijamii sababu ya Arroz kutiwa kizuizini na kutoa maoni juu ya ukosefu wa uhuru wa kujieleza nchini humo.

On Monday morning, May 27, health professionals met at the cinetheatre Gilberto Mendes, holding empty plates on their hands.

Siku ya Jumatatu asubuhi, Mei 27, wataalamu wa afya walikutana katika jengo la Cineteatro Gilberto Mendes, huku wameshika sahani tupu kwenye mikono yao. Picha kwa hisani ya Canal Moz.

Serikali yadhibiti habari

Wachambuzi wanaamini kwamba kukamatwa kwa Arroz kulichochea ushiriki [pt] wa wafanyakazi zaidi wa afya katika mgomo huo. Taarifa kuhusu asilimia ya wafanyakazi walioshiriki mgomo ni kati ya asilimia 90 hadi 95 ya wafanyakazi wote wa afya”, kipindi cha The stream cha Aljazeera kiliripoti tarehe 28 Mei.

Health professionals meet in Beira´s Central Hospital.

Mei 28, raia alitoa taarifa kwamba wataalamu wa afya walikuwa wanakutana katika Hospitali ya Beira ya kati.

Katika wiki ya kwanza ya mgomo, wakati msemaji wa Wizara ya Afya akisema kuwa vitengo vyote afya vilirejea hali ya kawaida, waandishi wa habari za kiraia na wale wa kujitegemea walisema kuwa kulikuwa vikwazo vingi katika baadhi ya vitengo vikubwa vya matibabu.

Raia na waandishi wa habari mjini Maputo walituma ripoti zao kutoka hospitali kadhaa na  vitengo vya afya: kulikuwa na kuchelewa kwa ushauri wa kitabibu, na wagonjwa walikuwa wanapokewa na kupimwa na wanafunzi, madaktari wa kijeshi, wageni na mashirika ya kimataifa kama vile Shirika la Msalaba Mwekundu. Wataalamu wengine, ambao kwa kawaida huchukua nafasi ya uongozi wa nje vitengo, walikuwa wanafanya huduma fulani mahususi.

Vitendo vya vitisho

Wakurugenzi wa hospitali walijaribu kuhamasisha wataalamu wa afya kufanya kazi, lakini hawakufanikiwa. Rekodi ya sauti [pt] iliyotumwa na Chama cha Madaktari cha Msumbiji katika Mtandao wa Facebook mnamo Mei 21 imefunua kitendo cha Mkurugenzi wa hospitali kubwa Msumbiji akiwatisha wataalamu wa afya:

…no dia em que o Ministério da Saúde começar a usar toda a máquina que tem por trás, vocês vão chorar …

… siku ambayo Wizara ya Afya itaanza kutumia mashine [za kutesa] ambazo zipo, mtalia…

Mei 22, Polisi wa Jamhuri ya Msumbiji (PRM) Wakifuatana na Jeshi la Rapid Intervention (FIR) walizuia watu kuingia kwenye bustani ya Nangade, eneo wazi katika mji mkuu wa Msumbiji, ambako wafanyakazi wa afya walipanga kukutania hapo.

Access to Nangade park blocked by the police.

Zuio la kuingia kwenye bustani ya Nangade likisimamiwa na polisi.

Mgomo unaendelea, vipi kuhusu afya?

Wakati Wizara ya Afya bado haijaweza kutatua tatizo la madaktari, wauguzi na watumishi, hali ya huduma ya afya inazidi kuwa mbaya zaidi.

Katika blogu inayokusanya habari za moja kwa moja iliyotengenezwa na @ Verdade kukusanya habari za kiraia kuhusu mgomo katika sekta ya afya, kuna shuhuda za ukosefu wa usafi, madawa, na mahitaji mengine ya msingi. Asubuhi ya Mei 28, mtandao wa raia uliripoti kupitia SMS:

Numa reunião serviço esta manhã Hospital Central #Maputo “nao ha roupa,comprensas,anestesico. Assim esta impossivel trabalhar.

Katika huduma ya mkutano leo asubuhi katika Hospitali Kuu ya Maputo, “hakuna mavazi, bandeji, dawa za ganzi. Ni vigumu kufanya kazi katika mazingira kama haya.”

Wagonjwa waliolazwa kwa sababu ya ugonjwa wa kifua kikuu katika Hospitali kuu ya Mavalane katika mji mkuu wa nchi hiyo hawajapata dawa tangu siku ya kwanza ya mgomo.

Chama cha Madaktari cha Msumbiji na Tume ya Watumishi wa Afya walisisitiza kwamba mgomo utasitishwa tu endapo serikali itaacha kuwatishia wataalamu wa afya na wafanyakazi wengine ambao walijiunga na mgomo huo, na pia ikiwa madai yao yatatimizwa. Wafanyakazi wa afya wanapinga jinsi marekebisho ya mshahara yanavyofanywa, katika ukiukaji wa mkataba wa maridhiano kati ya chama hicho na serikali mwezi Januari.

Serikali, kupitia mkurugenzi wa kitaifa wa uongozi wa kimkakati wa rasilimali-watu katika Wizara ya Utumishi wa Umma, alisema kwamba tayari imefikia kikomo katika uwezo wake wa kulipa marekebisho ya mshahara. Wizara ya Afya ilishtaki chama kwa kutokuwa wazi katika mazungumzo.

Lakini @ Verdade ina nakala ya mawasiliano rasmi yaliyokuwepo kati ya chama na Wizara ya Afya ambapo yeyote anaweza kusoma, katika barua ya tarehe Mei 21, kwamba wataalamu wa afya waelezea uwazi wao wa muendelezo wa mazungumzo, katika kujibu barua kutoka kwa Wizara.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.