Taarifa Za Ndani Zinasema; Wanafunzi wasiopungua 15 ‘Walitiwa mimba na wakufunzi’ katika chuo cha Polisi Msumbiji

Picha ikionesha uhitimu wa mafunzo ya polisi huko Msumbiji | picha ya skrini ya Agosti 19,  STV – Youtube, ilipigwa na mmiliki  

Nyaraka  za jeshi la polisi  la Msumbiji zilizovujishwa katika vyombo vya habari mapema mwezi Agosti zilidhihirisha kwamba wanafunzi 15 walipata ujauzito wakiwa katika shule ya mafunzo ya polisi huko Matalane, wilaya ya  jimbo la Maputo.

 Nyaraka hizo zinasema  kuwa mimba hizo ni matokeo ya uhusiano wa kingono uliopo baina ya wanafunzi na wakufunzi bila kufafanua kama mahusiano hayo yalikuwa ya hiari.

Hata hivyo imeelezwa kwamba wanafunzi wajawazito hawataweza kumaliza mafunzo kwa sasa, na watasafiri kurudi makwao wakilipiwa usafiri na polisi. Mwisho taarifa hiyo ikasema kuwa wakufunzi waliohusika “watasimamishwa kazi.” 

Alipoulizwa na gazeti la O País hapo Agosti 8, Kamanda wa Jeshi la Polisi Jenerali Bernardino Rafael alisema kuwa wahusika wote watakutana na taratibu za kinidhamu.  

Haikuchukua muda mrefu kabla shauri hili kulaaniwa vikali katika mitandao ya kijamii. Watumiaji kadhaa wa mitandao walieleza wazi kutokufurahishwa na maamuzi ya shule hiyo na hivyo kutaka haki ifanyike kwa wanawake hao.  

Mwanaharajati Fátima Mimbire aliandika huko Facebook:

Tratem o assunto Matalane com a devida seriedade. Estou de coração partido com esta notícia de 15 instruendas grávidas no Centro de Treinos de Matalane. Isso é grave. É grave porque, como o próprio documento refere, envolve os instrutores.

Ora, uma pessoa que detém autoridade sobre outra a engravida e o fim é um “processinho”? Isso me lembra o professor que exige sexo às alunas em troca de notas ou para não serem humilhada na sala de aulas por serem, na visão do professor, “burras”, no lugar de ser processado é transferido para ir dar aulas em outro lugar. E lá, continua as suas façanhas.

Suala  la Matalane lichukuliwe kwa uzito. Nimevunjwa sana moyo na suala hili la ujauzito wa wanafunzi 15 wa kituo cha mafunzo cha  Matalane. Hili jambo kubwa sana. Ni jambo kubwa kwa sababu kama nyaraka zilivyoonesha wahusika ni wakufunzi.

Sasa mtu mmoja mwenye mamlaka juu ya mwingine anamtia mimba na matokeo yake ni “mchakato kidogo?” Hili linanikumbusha kuhusu mwalimu aliyedai rushwa ya ngono kwa wanafunzi wake ili awape maksi au ili asiwadhalilishe darasani kwa sababu kwa mtazamo wake wanafunzi hao ni “wajinga,” na badala ya kushtakiwa mwalimu yule alihamishwa akafundishe mahali pengine  na huko anaendeleza unyonyaji wake.

Txeka, mwanaharakati wa haki za wanawake pia alilaani jambo hili huko Twitter:

“Shauri la Matalane”

Kuunda jamii yenye usawa kijamii katika kulinda haki sawa kwa wananchi inahitaji elimu sawia pamoja na sera za maendeleo zinazojali maendeleo ya wananchi pamoja na maarifa ya kisayansi na maadili pamoja na elimu ya uzalendo.

Shauri la Matalane

Kulaumu ukatili dhidi ya wanawake ni jambo la kawaida kwa jamii zenye mfumo dume, zinazofahamika kwa kudhalilisha wanawake na kuwafanya kutii matakwa ya wanaume ikiletea kuhukumiwa kwa matendo ya wahanga na kupunguza hatia ya wanyanyasaji.

Profesa wa chuo kikuu Carlos Serra alisema:

Matalane? Apenas a ponta do Iceberg, somos formatados para reproduzir Matalane. Imagino o dia em que elas começarem a narrar as suas histórias, começando pela mais tenra infância.

Matalane? Ni kipande kidogo sana cha barafu kinachochungulia na Matalane ni zao letu. Ninafikiria siku watakapoanza kueleza masahibu yao, wakianzia tangu utoto wao.

Vile vile mwanahabari na mwanaharakati  Selma Inocência alisema:

Waalimu wachache sana wamefikishwa mahakamani, wakashtakiwa na kuhukumiwa. Wanahusika na kuwapotezea utoto wao maelfu ya wasichana. Shuleni sio sehemu salama.

Takwimu zinaonesha kwamba mamia ya wasichana hupata mimba shuleni na wahusika wengine wakiwa ni wakufunzi, walimu na wakuu wa shule.”

Ombi limepitishwa likitaka adhabu itolewe kwa maofisa wa polisi waliohusika. Mpaka sasa zaidi ya watu 3,8000 wameshasaini.  

Hapo Agosti 19, Rais Filipe Nyusi hatimaye aliongea kuhusu kesi hiyo na akasema kuwa polisi itafanya uchunguzi: 

Para o Governo, este caso é sério e está a ser investigado ao detalhe ao nível ministerial e do Comando-Geral da Polícia da República de Moçambique. O Estado não deve nem vai tolerar situações como esta. A lei deverá ser cumprida e ela é igual para todos nós. Ninguém está acima da lei.

Decorrem inquéritos para aferir os contornos de cada um dos casos, procurando salvaguardar o estado psíquico e emocional das gestantes, porque elas merecem respeito humano.

Kwa serikali suala hili ni la msingi na linafanyiwa uchunguzi wa kina katika ngazi ya wizara na mkuu wa jeshi la polisi la Msumbiji. Jamuhuri haiwezi na haitavumilia masuala kama haya. Lazima sheria ichukue mkondo wake na ni kwa kila mtu. Hakuna mtu aliye juu ya sheria.

Upelelezi unaendelea kwa kuchunguza kwa kina taarifa zote katika kesi hii na kuzingatia hali ya kisaikoloji na kihisia ya wanawake hao wajawazito kwasababu wanastahili kuheshimiwa utu wao.

Kesi Nyingine

Huu ni muendelezo wa kesi za ukatili wanaokumbana nao wanawake wa Msumbiji ambapo haziripotiwi katika vyombo vya habari. 

Moja kati ya kesi ambayo hivi karibuni ilishikilia vichwa vya habari ni ile ya Alberto Niquice, Kaimu wa chama cha Liberation Front of Mozambique (Frelimo), ambaye anakabiliwa na shauri la jinai  kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka 13 mwaka 2018.  

Mapema  mwaka huu, Taasisi 30 za kiraia nchini Msumbiji zilimtaka Niquice asiapishwe baada ya kuchaguliwa tena mwaka 2019.  Hata hivyo, makamu aliichukua ofisi na anafanya kazi kama kawaida katika bunge. 

Kesi  nyingine iliyo katika vyombo vya habari ni kuhusu ukatili aliofanyiwa Josina Machel, binti wa Rais wa kwanza wa Msumbiji, Samora Machel.

Oktoba mwaka 2015, Josina alipigwa na mpenzi wake wa miaka mitatu Rofini Licuco akiachwa na upofu wa jicho moja. Licuco alihukumiwa kwenda gerezani miaka 3 na miezi 4 pamoja na kulipa fidia ya metika milioni 300 (sawa na dola za Marekani milioni 4.2) kwa Josina.

Hata hivyo Rofino alikata rufaa na Juni mwaka huu Mahakama kuu ya Rufaa iliifutilia kesi hiyo mbali kwa madai kuwa hapakuwepo na “ushahidi wa kutosha” katika kesi hii.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.