Kimbunga Chasababisha Uharibifu Mkubwa Zimbabwe na Nchi za Kusini mwa Afrika

Kimbunga Idai kimefanya uharibifu Zimbambwe,, Malawi, Mozambique na Afrika Kusini kikisababisha mafuriko makubwa, kung’oka mawena matope kuporomoka. Picha ya mafuriko katika nchi ya Msumbiji, iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii.

Kimbunga aina Idai kinachosababishwa na hali ya kitropiki kimeacha uharibifu mkubwa na vifo baada ya kuzikumba nchi za kusini mwa Afrika za Msumbiji, Malawi na Zimbambwe.

Hadi sasa inakadiriwa katika nchi hizo watu 162 wamepoteza Maisha katika kimbunga hicho. Kimefanya uharibifu mkubwa karibu jiji lote la Beira, nchini Msumbiji.

Shirika la Msalaba Mwekundu limesema, kimbunga ambacho kilichopiga Msumbiji wiki iliyopita kimeharibu asilimia 90 ya mji wa Beira, na vifo vinaendelea kuongeza katika nchi hiyo na nchi jirani ya Zimbabwe vimefikia hadi vifo 157

Hii ni ramani ya mahali ambapo kimbunga hicho kimeharibu:

Inakadiliwa watu 89 wamekufa katika nchi ya Zimbabwe tu, huku kukiwa na hofu ya takwimu ya juu katika eneo la Manicaland ya wilaya Chimanimani ambayo ipo kilometa 406 mMashariki mwa mji mkuu wa Harare, Zimbabwe huku nyumba na madaraja yakiwa yamebebwa na dhoruba iliyoanza Ijumaa.

Kutokana na taarifa ya serikali zaidi ya watu 300 hawaonikani

Umoja wa Mataifa katika Zimbabwe ulisema kuwa zaidi ya watu 8,000 wameathiliwa na mafuriko katika pande za mashariki mwa nchi hiyo.

” Inasikitisha Maisha ya wtu yamepotea na mali zimeharibiwa,” Umoja wa Mataifa Zimbambwe ulituma ujumbe wake kupitia twiita:

Kutokana na taarifa ya serikali, kimbunga Idai kilipiga sana mji wa Ngangu katika Chimanimani ambapo watu wengi wamepoteza maisha. Zaidi ya nyumba elfu moja ziliharibiwa kwa kuangukiwa na udongo na mawe.

Kimbuka hicho kilitokea katika bahari ya Hindi na kuambatana na mvua nyingi iliyoanza kunyesha Msumbiji Alhamisi ikiambatana na upepo uliovuma kwa mwendokasi wa kilometa 160 kwa saa, inalipotiwa ulisababisha mawimbi ya bahari yenye ukubwa wa meta kwenda juu.

Jeshi na polisi vimetumika kusaidia katika uokoaji wa majeruhi.

Kutokana na taarifa ya Waziri, mvua imeacha kuonyesha na hali ya kuonekana wazi ni nzuri na hii itasaidia jeshi la anga kutumia helikopita kuokoa watu zaidi,

July Moyo, Waziri wa mambo ya ndani alisema kwamba miili inaonekana ikiwa inaelea katika mito na hakuna linguine linaloweza kufanyika kwa sasa.

Barabara, madaraja na miundombinu ya simu kwa sasa vimekatika na mamia ya nyumba zimeharibika.

Paolo Cernuschi, Mkurugenzi wa nchi wa shirika la msalaba mwekundu International (IRC) katika Zimbabwe alisema timu ya IRC katika Zimbabwe inajaribu kuzifikia jamii zilizoathiriwa na Kimbunga lakini uharibifu wa miundombinu ni mkubwa sana na timu hiyo imeshindwa kufika Chimanimani au Chipinge.

“Kuna matengenezo ya haraka ya barabara yanaendelea, kwa hiyo tutajaribu tena kesho Asubuhi,” alisema Cernuschi.

Siku ya Jumapili asubuhi, serikali ya Zimbambe ilikutana na Kamati ya wizara zote, na baadayae iliunda Kamati ndogodogo 10 zitakazoshughulikia maeneo yaliyoharibiwa sana.

Kamati zitashughulikia maeneo ya chakula, rasilimali fedha, usalama na malazi, usafiri, maji na usafi wa mazingira.

Afisa wa Idara ya huduma za hali ya hewa alisema kwamba kimbunga kilidhoofishwa na kuhamia kutoka mashariki kuelekea maeneo ya kusini ya Zimbabwe.

“Hadi mililita 200 za mvua zimenyesha Chipinge [eneo lililopo mashariki mwa Zimbabwe], 118 mililita kaskazini mwa Chipinge, na 102 mililita katika Buhera [eneo la kusini mwa Zimbabwe],” Afisa alisema .

Alitahadharisha kuwa nyanda za juu mashariki mwa nchi bado zinategemewa kuwa na mafuriko kutokana na mvua nyingi inayonyesha na alishauri umma kuepuka kusafiri kule

Hakuna ukungu wala mvua vilivyotegemewa siku ya Jumatatu hata hivyo hali ya hewa nzuri inategemewa kuanza.

Juhudi za kurekebisha uharibifu zitahitajika kwa muda mrefu na harakati za kutoa misaada kwa waathirka zinaendelea.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.