Kwa Mara ya Kwanza katika Historia ya Nchi, Mwanamke Aongoza Chuo Kikuu cha Umma Msumbiji

Emília Nhalevilo, Mkuu wa chuo kikuu cha Púnguè. Picha na Emília Nhalevilo, na imetumiwa kwa idhini .

Mwezi Machi 2019, Profesa wa Msumbiji Emília Nhalevilo aliteuliwa kuwa mkuu wa chuo kikuu kilichoanzishwa hivi karibuni cha Púnguè , hivyo kuwa mwanamke wa kwanza kabisa kuongoza chuo kikuu cha umma katika nchi hii ya kiafrika.

Aliteuliwa na Rais Filipe Nyusi, lakini maamuzi hayo juu ya chuo hicho kilichoanzishwa hivi karibuni yalitangazwa na halmshauri ya mawaziri tarehe 29 mwezi Januari. Kisheria, Nhalevilo ataendelea kuwepo ofisini kwa muda wa miaka minne.

Nhalevilo ambaye ni Daktari alizaliwa Nampula ambalo ni jimbo maarufu Msumbiji. Ana shahada ya uzamili ya Elimu kutoka chuo kikuu cha Perth, Uastralia na shahada ya elimu ya sayansi kutoka chuo kikuu cha Pedagogical (UP).

Kuanzia mwaka 2005 hadi 2007, alifanya kazi kama Profesa katika Chuo kikuu cha Teknolojia cha Curtin kilichopo Australia. Mwaka 2008, Nhalevilo alikuwa mkuu wa idara ya kemia pale Chuo kikuu cha Pedagogical, na halafu akateuliwa kuwa mkurugenzi msaidizi wa kituo cha mafunzo ya Msumbiji na elimu ya dunia, kituo cha utafiti katika taasisi hiyo.

Mwaka 2017, alikuwa mjumbe wa program ya matembezi ya wanafunzi ya Fulbright katika shule ya utamaduni, elimu na Maendeleo ya rasilimali watu cha chuo kikuu cha New York, Marekani.

Nhalevilo alikuwa mkuu wa kitivo cha utafiti na ugani katika chuo kikuu cha Pedagogical tangu mwaka 2018.

Nafasi aliyonayo ya Mkuu wa chuo kikuu cha umma ni sawa na nafasi ya waziri katika nchi ya Msumbiji.

Eliana Nzualo, mwanaharakati na feministi bloga , anasema kuteuliwa kwa Nhalevilo ni kwa kihistoria:

UM DIA NA HISTÓRIA

Professora Doutora Emília Nhalevilo é a primeira mulher na liderança de uma Universidade Pública em Moçambique. Parabéns à Magnífica Reitora!

Por mais mulheres nas Universidades,
Por mais mulheres na liderança!

SIKU YA KIHISTORIA

Profesa Emília Nhalevilo ni mwanamke wa kwanza kuongoza Chuo kikuu cha umma katika Msumbiji.

Hongera Mkuu wa Chuo Adhimu!

Kwa wanawake wengi katika vyuo vikuu,

Kwa wanawake wengi kuongoza!

Katika Msumbiji wanawake bado wanakabiliana na changamoto ya kuingia katika nafasi za uongozi na utawala. Lakini kumekuwepo na uboreshaji: katika bunge la sasa, kwa mfano Rais wa bunge na viongozi wa taasisi kubwa pili za kisiasa vyote vinaongozwa na wanawake.

Lakini kuna tofauti ya kijinsia inayoendelea katika nchi hii ya kusini mwa Afrika.

Ripoti ya UNDP ya mwaka 2016 ya Maendeleo ya rasilimali katika Afrika , yenye kichwa cha habari “kuongeza usawa wa kijinsia na Kuinua wanawake katika Afrika,” ilionesha kuwa wanawake na mabinti wa Msumbiji wanaendela kuteseka na tofauti iliyopo kama vile kunyimwa haki zao, ukosefu wa elimu na matibabu na kuendelea kwa vitendo vya kikatili.

Mwaka 2018 katika Msumbiji, kulikuwa na matukio yapatayo 25,356 ya vitendo vya kikatili majumbani ambapo matukio 12,500 yalikuwa dhidi ya wanawake na 9,000 dhidi ya watoto.

Msumbiji inashika nafasi ya 10 ulimwenguni kwa ndoa za utotoni kutokana na taarifa ya UNICEF ya mwaka 2015. Shirka hilo hutafsiri “ndoa za utotoni” kama muungano wa ndoa ambapo angalau mmoja wa wanandoa hao ana miaka chini ya 18.

Katikati ya mwaka 2018, rubani Admira António alikuwa mwanamke wa kwanza kuwa rubani wa ndege katika Msumbiji wakati mwezi Desemba 2018, ndege yenye wahudumu wa kike wote iliruka kwa mara kwanza.

Mwaka 2014, wakati askari polisi wa Jamhuri ya Msumbiji ilipopandisha vyeo askari 39, Arsenia Massingue aliteuliwa kuwa mwanamke wa kwanza kuwa jenerali katika jeshi hilo.

1 maoni

  • Namfahamu Profesa Emilio Nhalevilo kibinafsi. Nilikutana naye mwaka jana kwenye mkutano wa kitaaluma. Kwa kweli ni mwanamke mwenye uwezo mkubwa na mnyenyekevu. Kwamba amekuwa Mkuu wa Chuo ni jambo kubwa. Tunamtakia kila la heri katika majukumu yake mapya.

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.