Tarehe 17 Aprili, mwanariadha raia wa Msumbiji Bruno Saraiva aliishinda mashindano ya kimataifa ya kutunisha misuli nchini Hong Kong.
Baada ya kuwashinda wapinzani watano, mwanariadha huyo alishinda nafasi ya kwanza katika kundi la watunisha misuli bora kundi ambalo ni muhimu na linapendwa na watu wengi ambalo alikuwa anatafutwa mwanariadha mzuri ambaye huonesha maumbo yake katika mikao mbalimbali .
Pia, Bruno alishinda tuzo ya “ujumla” kwa wanariadha bora katika kundi la pili.
Alishiriki katika makundi matatu kushindana na watunisha misuli wa kiume katika shindano la watunisha misuli nchini Hong Kong: Wanaume wenye maungo ya kimwanariadha, wanaume wenye maungo thabiti na wanaume wenye maungo ya kimichezo mashindano yaliyopangwa kufanyika tarehe 23 Juni.
kama mrejesho wa maombi yetu yaliyotumwa kupitia mazungumzo ya Facebook kuhusu mashindano yalivyokwenda Saraiva alieleza kuwa yalikuwa ni mashindano ya kwanza ambayo yalikuwa na muda mfupi wa maandalizi:
Eu fui preparado pelo Castro Cazé em apenas poucos dias e lá fomos fazer as inscrições, e ele disse Bruno tu vais fazer a categoria que eu sempre quis que fizesses: a mais conhecida por Classic Physique e logo na minha primeira aparição ganhei na minha categoria e fui ganhar ainda o overall, como se fosse chamar todos os primeiros lugares da tua categoria.
Tafsri: Nilifanyiwa mazoezi na Castro Cazé kwa siku chache sana na kisha tukaenda kujisajili. Bruno alisema alishindana katika kundi ambalo huwa anataka kushindana ambalo linajukana kama ni kundi la watusha msuli bora na nilivyotokea tu kwa mara kwanza nikashinda katika kundi langu na kisha nikashinda kwa ujumla kwa sababu ya kushika nafasi ya kwanza katika kila kundi.
Watu wapatao elfu 24 walimfuatilia kwenye akaunti yake ya Instagram, Bruno ambaye anaishi mji mkuu Maputo ana umbo la pekee kwa watunusha misuli katika Msumbiji.
Kutokana na Wikipedia kiingilio katika shindano la kutunisha misuli:
Kunisha msuli ni zoezi endelevu la ukinzani kutawala na kuendeleza misuli kwa madhumuni ya uzuri. Mtu anayejiunga katika shughuli hiyo anaitwa mtunisha misuli. Katika mashindano mtunisha misuli husimama katika mstari na kuonesha mikao mbalimbali ili jopo la waamuzi liwapime na kuwaweka katika matabaka ya uzuri kwa kuzingatia vigezo kama hali zao, misuli na ulinganifu.
Saraiva alielezea furaha yake ya kushinda tuzo huko Hong Kong kwa kutuma ujumbe kupitia Instagram:
Obrigado pela vitória senhor. É com muita alegria que tenho o prazer de anunciar e compartilhar com todos vocês a minha vitória na categoria Classic Physique e tendo vencido o overall na competição global clássica em Hong Kong.
Tafsiri: Nakushukuru kwa ushindi, Bwana. Ninayo furaha kubwa ya kutangaza na kushirikiana nanyi kwa ushindi wangu katika kundi bora la watunisha misuli na kushinda ushindi wa jumla katika mashindano ya kimataifa ya kutunisha misuli nchini Hong Kong.
Katika ujumbe mwingine , Bruno alielezea vikwazo au ugumu aliokutana nao kabla ya kwenda nchini Hong Kong:
Por favor meu amigo/a leia esta mensagem com muito carinho, porque essa é a mais pura realidade, não tenho vergonha de dizer e sei que muitos vão se emocionar: quando estava pra vir a Hong Kong pra competir andei em vários sítios batendo as portas pedindo apoio, falei com varios amigos que alguns eu tinha a certeza que pudessem ajudar, e as respostas de alguns eram:
1. Bruno tu não vas conseguir ou seja não tens chances de ganhar e nem de ficar entre os melhores;
2. Outros diziam que não me podiam ajudar porque seria deitar fora o dinheiro;
3. Outros ate disseram Bruno você deve fumar muita maconha.
Tafsiri; Tafadhali rafiki yangu soma ujumbe huu kwa ukarimu kwa sababu ni uhalisia. sina soni kuuelezea na najua wengi watahamaki sana. Nilipokuwa nakaribia kuja Hong Kong kumalizia nilipita sehemu nyingi nikipiga hodi na kuomba msaada, niliongea na marafiki zangu wengi ambao wengi niliamini watanisaidia na majibu yao yalikuwa haya:
1. Bruno, hutashinda na huna nafasi ya kushinda au kumaliza miongoni mwa wale bora;
2. Wengine walisema hawawezi kunisaidia kwa sababu watakuwa wanapoteza fedha yao;
3. Wengine hata waliniambia Bruno, lazima unavuta bangi.