Waandamanaji Wanaodai Demokrasia Wageuza Hong Kong Kuwa Bahari ya Miamvuli

Protesters used umbrellas to shield tear gas. Photo from Facebook group: Hong Kong Demo Now,

Waandamanaji wakitumia miamvuli kujikinga na moshi wa mabomu ya machozi. Picha imepigwa na Yang.

Je, mwamvuli unaweza kutumiwa kama kifaa cha kupigania demokrasia? Ndio. Nchini Hong Kong, waandamanaji wa amani wanaodai uchaguzi huru wa kidemokrasia halisi wanatumia miamvuli kujilinda na mabomu na kujizuia kulowa na maji ya washawasha kutoka kwa polisi.

Picha ya kuvutia iliyopigwa wakati wa maandamano ya kukaa karibu na makao makuu ya serikali mnamo Septemba 28 iliwaonesha umati wa watu waliokuwa wakiandamana wakiwa wamebeba miamvuli yenye rangi tofauti, ikitofautiana sana na mavazi ya polisi wa kuzuia fujo.

Carol Chan designed the poster for the "umbrella movement" in Hong Kong.

Carol Chan alibuni bango la “Vugu vugu la Miamvuli” nchini Hong Kong. Linasema, “Taiwani ina vugu vugu la alizeti, Hong Kong ina vugu vugu la kivuli”

Vyombo vya habari vya kigeni vimeyapa maandamano hayo ya amani jina la utani “mapinduzi ya miamvuli”. Kundi la mtandao wa Facebook, “Demokrasia ya Hong Kong Sasa” lilibadili jina la kundi lao kuwa “Vugu Vugu la Miamvuli” na kuandika ujumbe wa maelezo kwenye kundi hilo:

Vyombo vya habari vya kigeni vimeyaita maandamano haya kuwa “Mapinduzi ya Miamvuli”. Haya sio mapinduzi kwa maana halisi. “Vugu vugu la Miamvuli’ ni jina sahihi kwa mukhtadha huu.

“Silaha” pekee tulizonazo, mara nyingi, ni miamvuli tunayoibeba kwenye mabegi yetu kwa ajili ya kukabiliana na hali ya hewa isiyotabirika. Wananchi wa Hong Kong hawahitaji kingine chochote isipokuwa utengamano. Hata hivyo, kwa namna ile ile tusivyoweza kuona kupitia kwenye wingu zito angani, hatutamani kupatwa dhoruba.

“Vugu vugu la Miamvuli’ linawakilisha kampeni nyepesi lakini iliyodhamiriwa sana: Katikati ya dhoruba, hatutarudi nyuma!

Maandamano ya kukaa, yanayoitwa Occupy Central, yanadai kuwa Beijing ijitole kwenye mpango wake wa kuingilia uchaguzi wa mtawala wa juu kabisa wa Hong Kong, anayeitwa kiongozi mkuu, ambao unamtaka yeyote anayegombea madaraka apate uungwaji mkono na walio wengi kutoka kwenye kamati ya uteuzi iliyojaa mashabiki wa Beijing (ambao ni watu wenye mrengo wa chama cha Kikomunisti cha China). Maandamano ya kukaa yameenea kuanzia wilaya ya kiuchumi ya Admiralty mpaka wilaya ya kibiashara kwenye ghuba ya Causeway Bay na Mongkok. Idadi kubw aya watu kwenye kisiwa cha Hong Kong imeendelea kuwepo mtaani siku nzima ya Septemba 29.

Gazeti linaloisemea Beijing , Global Times lilikuwa nasehemu ya maoni kuhusu maandamano hayo ya Occupy Central, yaliyoanza Septemba 28, likilituhumu vuguvugu hilo kwa kuchafua sura ya Hong Kong. Hivi kweli miamuvuli inaharatibu sura ya jiji kuliko polisi waliobeba silaha na mabomu ya kutoa machozi?

Screen capture from local Television - TVB.

Picha ya mnato iliyopigwa kwenye runinga ya TVB.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.