Habari kuhusu Hong Kong (China)
Mshindani wa Msumbiji Ashinda Mashindano ya Kimataifa ya Kutunisha Misuli nchini Hong Kong
Saraiva ni mtu mashuhuri kwa kutunisha misuli nchini Msumbiji.
Polisi wa Hong Kong Wawapiga Mabomu ya Machozi Waandamanaji Wanaodai Demokrasia
Polisi walipambana na waandamanaji baada ya maandamano ya kukaa katikati ya jiji la Hong Kong kudai uchaguzi wa demekrasia halisi.
Hong Kong: Mfanyakazi wa Ndani Apigwa Makofi, Mateke na Kulazimishwa Kufanya Kazi Masaa 21 kwa Siku
Kesi nyingine ya unyanyasaji wa mtumishi wa ndani wa kigeni imefichuliwa. Mhanga huyo Rowena Uychiat inadaiwa alilazimishwa kufanya kazi masaa 21 kwa siku (6:00 mpaka 03:00) bila kupewa siku ya...
Hong Kong: Video Inayosambazwa Mtandoni Yamwonyesha Jamaa Akipigwa Makofi Mara 14 na Rafiki Yake wa Kike
Kama inavyoelezwa na Tom Grundy, mpita njia aliwaita polisi na mwanamke huyo aliwekwa chini ya ulinzi kwa kumpiga vibao rafiki yake wa kiume aliyekuwa amepiga magoti mbele yake akimwomba msamaha...
Hong Kong: Pinga Biashara ya Pembe za Ndovu
Muungano wa watu binafsi na Asasi Zisizo za Serikali zinazoguswa na tatizo la ujangili wa tembo, Hong Kong kwa Tembo, uliandamana Oktoba 4, wakiitaka Hong Kong kuteketeza hifadhi yake ya tani 25 za pembe za ndovu.
Maandamano Yasitisha Ujenzi wa Mtambo wa Nyuklia Kusini mwa China
Kufuatia siku tatu mfululizo za maandamano, inaonekana kuwa serikali ya Manispaa ya Heshan katika jiji la Jiangmen imesitisha mpango wake wa ujenzi wa mtambo mkubwa wa nishati ya Nyuklia. Baadhi ya watu wanaamini kuwa ushindi huu ni wa muda mfupi tu. Wana wasiwasi kuwa, mradi huu unaweza kuibukia sehemu nyingine karibu na Delta ya mto Pearl, Kusini mwa China mahali palipo na idadi kubwa sana ya watu.
China na Hong Kong: Walinzi na Wauaji
Bodyguards and Assassins (Walinzi na Wauaji) ni filamu ya kuchangamsha iliyotolewa wakati wa Krismasi huko China, Hong Kong na Taiwan. Ikiwa ni filamu ya kizalendo, awali ilipangwa kutolewa mwezi Oktoba...