Rais Wa Umoja Wa Wanafunzi Wa Thailand Akamatwa Kwa Kushiriki Maandamano Ya Kuipinga Serikali

Kiongozi wa wanafunzi Jutatip Sirikhan akiwa amefunikwa kwa rangi nyeupe ikiwa ishara ya mgomo baada ya kuachiliwa kwake. Picha na maelezo kutoka kwa Prachatai

Makala hii ni kutoka kwa Prachatai, chanzo huru cha habari huko Thailand, ikiwa imehaririwa na kuchapishwa na Global Voices kama sehemu ya makubaliano ya kushirikishana mahudhui.

Raisi wa Umoja wa wanafunzi wa Thailand Jutatip Sirikhan amekamatwa akiwa njiani akielekea chuoni hapo Septemba 1, kwa sababu ya kushiriki katika maandamano makubwa ya Julai 18.

Jutatip alikamatwa akiwa ndani ya gari akielekea darasani katika chuo kikuu cha Thammasat kampasi ya Tha Prachan huko Bangkok. Aliingia mubashara katika ukurasa wake wa Facebook mnamo saa 07:50 mchana hapo Septemba 1, wakati askari waliovalia kiraia waliposimamisha taksi aliyokuwa amepanda na wakamwonesha hati ya kumkamata.

Jutatip alipelekwa kwenye kituo cha polisi cha  lSamranrat. Afisa wa polisi aliambatana naye kuelekea kituoni akiwa kwenye taksi nyingine kwa sababu hakujisikia kuwa salama kupanda gari binafsi walilokuja nalo askari waliokuja kumkamata. Aliendelea kuwa mubashara katika ukurasa wake wa Facebook, akisoma kifungu cha habari  Ufahamu wa Kawaida kilichotafsiriwa kwa Kithailand na Thomas Paine.

Alipelekwa katika mahakama ya kihalifu ya Bangkok na alipewa dhamana na kuachiliwa saa 11.20 jioni akiwa chini ya uangalizi wa Mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Thammasat. Mahakama haikumtaka alipe papo hapo kiasi cha baht 100,000  (sawa na dola za Marekani 3,190) kwa ajili ya dhamana, lakini aliwekewa masharti kwamba hatakiwi kurudia tena makosa aliyoshtakiwa kwayo – masharti hayo hayo yalitolewa kwa kila mmoja aliyekamatwa na kuachiliwa kwa mashtaka hayo.

Jutatip ni mwanaharakati wa 14 kukamatwa kwa kushiriki maandamano makubwa ya Julai 18. Washiriki wengine 15 wa maandamano hayo wamepokea wito na wameripoti katika kituo cha polisi cha  Samranrat kusikiliza mashtaka yao hapo Agosti 28. Jutatip alishtakiwa kwa uchochezi, kukaidi Amri ya Dharura na Sheria ya Magonjwa ya Kuambukiza, pamoja na mashtaka mengine.

Jutatip alitoka mbele ya mahakama ya kihalifu baada ya kuachiliwa huru na alifanya mkutano mfupi na vyombo vya habari.

“Rangi inaweza kusafishwa, lakini hatuwezi kusafisha uonevu”

I didn’t intend to run away to begin with. I know I have an arrest warrant. I have been waiting to be arrested for a very long time, but it didn’t happen until today. Each time someone gets arrested, there will be slurs against our side that we did not protest peacefully.

I am a student and I have been harassed by the police for months, for years. Why is there no compensation for me? Why must there be compensation for the police who are servants of the dictatorship?

There should actually be a summons first, but what happened was that the police brought the arrest warrant and arrested me. It’s extremely unfair to a student. They followed me with my phone signal, followed me from where I’m staying. They threatened my home, they threatened my family, they took a warrant to my house, so now we have to escalate our protest. Everything is supported by the Constitution.

We pay our taxes. We must receive protection from the state, not harassment from the state. So today I have to express myself symbolically that we can do this. We must stand by our rights and freedoms. Throwing paint is also something that can be done.

Sikupanga kukimbia tangu awali. Nilifahamu kuwa nina hati ya kukamatwa na nimekuwa nikisubiri kukamatwa kwa muda mrefu, lakini haikutokea mpaka leo. Kila mara anapokamatwa mtu mmoja lazima yatokee maneno mabaya kwamba hatukuandamana kwa amani.

Mimi ni mwanafunzi na nimekuwa nikisumbuliwa na askari kwa miezi, kwa miaka kadhaa. Kwa nini hakuna fidia kwangu? Kwa nini iwepo fidia kwa polisi tu ambao ni watumishi wa udikteta?

Ingetakiwa uwepo wito kwanza, lakini kilichotokea ni kwamba polisi walikuja na hati ya kunikamata moja kwa moja. Ni uonevu wa hali ya juu kwa mwanafunzi. Walinipata kwa kufuatilia mawasiliano yangu ya simu kuanzia ninapoishi. Wametishia watu nyumbani kwangu, familia yangu na waliipeleka hati ya kunikamata nyumbani  kwa hiyo sasa inabidi tuyaimarishe maandamano yetu. Kila kitu kipo kulingana na katiba.

Tunalipa kodi zetu, lazima tulindwe na serikali sio kudhalilishwa na serikali. Kwa hiyo leo, nimejieleza kwa kuashiria kwamba tunaweza tukalifanya hili. Lazima tusimame kwa ajili ya haki zetu na uhuru wetu. Kujimwagia rangi pia ni kitu kinachoweza kufanyika.

Kisha Jutatip alijimwagia ndoo ya rangi nyeupe mwilini mwake huku akiwa ameinua mkono wake juu huku akiwa amenyoosha vidole vitatu saluti  ya ‘Mchezo wa Njaa’. Alisema kuwa rangi nyeupe inawakilisha usafi na haki, na wanadai urejesho wa haki.

We are showing that this is freedom, this is the kind of expression we can do. Even if now it is throwing paint over ourselves, it is a way of showing that we can throw paint at any time. We can throw paint over those with power, because those with power throw legal charges over us, throw bullets at us without exception.

Paint can be washed out, but we can’t wash out injustice.

Tunaonesha kuwa hii ni haki, hii ni aina ya kielelezo cha kwamba tunaweza kufanya. Hata kama ni kujimwagia rangi kwa sasa, ni njia ya kuonesha kuwa tunaweza kujimwagia rangi saa yoyote. Tunaweza kuwamwagia rangi hao walio na mamlaka kwa sababu wanatutia hatiani na kuturushia risasi saa yoyote bila kujali, kwa kuwa wana mamlaka.

Rangi inaweza kusafishwa lakini uonevu hauwezi kusafishwa.

Baada ya hapo, Jutatip alimshukuru Mhadhiri ambaye alimuwekea dhamana na watu waliokuja kumuunga mkono na kusaidia umati kusafisha rangi iliyokuwa imetapakaa katika njia ya waenda kwa miguu mbele ya mahakama.

“Hatutaacha kupambana mpaka tushinde kila kitu, ikiwemo marekebisho ya ufalme na  katiba mpya,” alisema Jutatip.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.