Polisi wa Hong Kong Wawapiga Mabomu ya Machozi Waandamanaji Wanaodai Demokrasia

Protesters in Hong Kong are using umbrellas to shield themselves from tear gas.  Photo from Twitter @15MBcn_int

Waandamanaji jijini Hong Kong wanatumia miamvuli kujilinda na moshi wa mabomu ya machozi. Picha kutoka mtandao wa Twita @15MBcn_int

Waandamanaji waonadai uchaguzi wenye demokrasia kamili jijini Hong Kong walikumbana na nguvu za dola, mabomu ya machozi na maji ya kuwasha wakati wa siku ya pili ya mandamano hayo jijii humo.  

Kufuatia mapambano kati ya Polisi wa Hong Kong na waandamanaji wanfaunzi mnamo Septemba 27, maandamano ya kukaa yaliyofanyika katikati ya jiji kudai demokrasia yalianza saa 7:30 usiku siku iliyofuata kuishinikiza serikali ya China kuondoa dai kwamba mgombea wa uongozi wa juu kabisa Hong King lazima apate uungwaji wa walio wengi kutoka kwenye kamati ya uteuli ambao kimsingi inasimamia maslahi ya Beijing. 

Polisi wa kutuliza ghasia walianza kujaribu kuwatuliza waandamanaji waliokuwa wamejikinga na moshi wa mabomu ya machozi na maji ya kuwasha kuanzia saa 12 jioni tarehe 28 Septemba. Maelfu ya waandamanaji walikuwa bado mitaani kwenye eneo kuu la kiuchumi la jiji hilo wakipambana na polisi wa ghasia wakati makala hii ikichapishwa. 

Habari zisizothibitishwa za polisi kutumia risasi za mpira kuwatawanya waandamanaji zimeenea kwenye mitandao ya kijamii. Waandaaji wakuu wa maandamano hayo wamewasihi waandamanaji kurudi tena ifikapo saa 4 usiku.

China imeuahidi mkoa maalum wa kiutawala wa Hong Kong, ambao una uhuru wa aina fulani kutoka serikali kuu, uwezo wa moja kw amoja kupiga kura kwenye uchaguzi wa 2017 kmchagua kiongozi mkuu wa jimbo hilo, lakini wanaharakati wa demokrasia wanashikilia msimamo wao kwamba kamati ya uteuzi inapunguza haki za watu kumchagua kiongozi wao. 

Polisi wa Hong Kong waliyatangaza maandamano hayo ya kukaa kuwa batili na walifunga barabara na njia zinazoelekea kwenye makao makuu ya serikali. Polisi wengi zaidi waliwasili na kutawanywa kwenye wilaya za Admiralty na Kati wakati waandamanaji walipojaribu kwenda zilipo ofisi za kiutawala kwa kutembea kupitia barabara za Harcourt na Connaught. Mwisho wake barabara hizo mbili zilizopo kwenye eneo la kiuchumi la jiji hilo zilifungwa mwendo wa saa 9 mchana.

Mtawala Mkuu wa Hong Kong Leung Chun-ying alifanya mkutano na waandishi wa habari saa 9:30 alasiri akirudia msimamo wake kwamba mabadiliko ya uchaguzi yatafanyika kwa muundo uliowekwa na Beijing na kwamba Polisi watachukua hatua kwa maandamano yaliyo kinyume cha sheria, kwa mujibu wa sheria.

Maelfu ya waandamanaji walikuwa wamezunguka ofisi za serikali zilizopo kwenye maeneo mbalimbali ya wilaya za Admiralty na Kati, wakifunga baadhi ya barabara. Polisi waliinua bango la tahadhari lenye rangi ya machungwa, lililosema, “tawanyikeni, vinginevyo tunawapiga risasi”:

Sijawahi kuona ghasia na tahadhari hii ya polisi hapa Hong Kong kwa waandamanaji “TAWANYIKENI VINGINEVYO TUNAWAPIGA RISASI’

Saa 12 jioni, polisi wa kutuliza ghasia walianza kupiga mabomu ya kutoa machozi.
Watumiaji wa mtandao wa Twita waliweka picha za tukio hilo la ghasia hizo. @imrika1874 aliweka picha ikimwonesha polisi akimwelekezea bunduki kwa waandamanaji, waliokuwa wamenyanyua mikono:

Hii ni Hong Kong!!! Tafadhali iambieni dunia!!!

@jeromyu aliposti tukio hili:

[dharura] tafadhali sambaza: polisi wakatili wanarusha risasi na mabomu ya machozi kwa waandamanaji watulivu, wanatishia kuwapiga risasi!!!

Waandishi wa habari na wazee walikuwa shabaha ya maji ya kuwasha ya polisi:

Uso unaofahamika zaidi Hong Kong

Polisi wanamkamata mzee mwaandamanaji na kumnyunyuzia maji ya kuwasha usoni: kitendo cha kikatili namna gani

Badala ya kutoroka eneo hilo, watu wengi wanatawanyika na kurudi eneo hilo wakiwa na vifaa bora zaidi, kama vile makoti ya mvua, vifaa vya kujikinga na moshi wa mabomu na miwani ya kukinga macho:

Wanafunzi wanajiandaa kwa mkesha. Uratibu unaoshangaza sana

Umati unakasirishwa polisi zaidi wanapowasili! Wanapiga kelele, “Polisi ondokeni!”

Zaidi, polisi wametoa maagizo kwa kampuni ya treni kusitisha safari za kwenda Admiralty ili kuwaruhusu polisi zaidi kwenye eneo hilo. Lakini waandamanaji wamefunga lango la kuingilia ili kuwazuia plisi kuingia:

Wanafunzi wa Chui Hai walipiga picha ya polisi wakiingia kwenye treni kwenda eneo yaliko maandamano

Kituo cha treni cha Admiralty kimefungwa

Wakijibu ghasia zinazofaywa na polisi, Shirikisho la Vyama wa Wanafunzi wa Chuko Kikuu lilitoa wito wa mgomo wa kuingia madarasani wiki hii. Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Hong Kong kimetoa wito wa mgomo wa wafanyakazi, Chama cha Walimu Hong Kong na Chama Kikuu cha Wafanyakazi wa Jamii wa Hong Kong nacho kitazindua mgomo wa walimu.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.