#MwachieniAmade: Mwandishi wa Habari Akamatwa na Kuteswa kwa Kuripoti Vurugu Kaskazini mwa Msumbiji.

Manusura waliopoteza ndugu zao na nyumba zao wakiwa wamejipumzisha kufuatia shambulizi la Juni 5 katika kijiji cha Naunde huko Cabo Delgado, Msumbiji. Picha na Borges Nhamire, imetumika kwa ruhusa.

Mwandishi wa habari wa Msumbiji Amade Abubacar alikamatwa hapo Januari 5 wakati akiripoti kuhusu mashambulizi na vurugu katika vijiji vidogo vya jimbo la Cabo Delgado huko Msumbiji.

Ukiwa Kaskazini mwa Msumbiji, Cabo Delgado ina ukwasi wa mali asilia kama vile makaa ya mawe, rubi na gesi asilia vinavyopatikana huko bonde la Rovuma. Baadhi ya waangalizi wanasema kuwa kikundi kinachoendesha mashambulizi hayo walikusudia kuchukua mali hizo.

Tangu Oktoba 2017, mashambulizi kadhaa yameshafanywa katika wilaya tofauti za Cabo Delgado na inayodhaniwa kuwa yanafanywa na kikundi hicho hicho cha waasi. Vyombo vingi vya habari vimeripoti kuhusu mashambulizi hayo lakini viongozi wa serikali wameshindwa kutoa maelezo kuhusu jambo hilo au kuthibitisha ushahidi wa matukio haya.

Mwaka 2018, zaidi ya watu mia moja walishitakiwa pamoja kwa kuhusishwa na matukio hayo ya kihalifu. Kesi zao zinatarajiwa kufikia mwisho mwaka huu.

#MwachieniAmade: Ni kampeni inayotaka mwandishi wa habari wa Msumbiji kuachiliwa huru.

Amade Abubacar anafanya kazi na Chuo cha Mawasiliano ya Jamii cha Msumbiji na ni mwandishi wa habari wa tovuti ya habari ya Zitamar na kituo cha redio cha Nacedje.

Mwandishi huyo alikamatwa na kuwekwa kizuizini na Jeshi la Polisi la Msumbiji hapo Januari 5 wakati akiwapiga picha manusura wa mashambulizi huko Cabo Delgado.

Amade alipelekwa kwenye kambi ya jeshi la ulinzi la Msumbiji katika wilaya ya Mueda, pamoja na kwamba yeye sio mwanajeshi. Baada ya wiki chache, alihamishiwa katika gereza la kiraia kuhalalisha kuwepo kwake kizuizini huko Pemba, makao makuu ya Cabo Delgado .

Baada ya kufikishwa kwenye gereza la kiraia, Amade aliwasiliana na Chama cha wanasheria wa Msumbiji na kutoa taarifa kuwa amekuwa akiteswa mikononi mwa wanajeshi, ambapo alisema humpiga na kumnyima chakula.

Watu wengi na vikundi huru vya vyombo vya habari vimepaza sauti kumtetea Abubacar wakisema kuwa kukamatwa kwake na kuwekwa kizuizini ni kutishia na utekelezaji wa uhuru wa kujieleza.

Taasisi ya Habari Ukanda wa Kusini mwa Afrika ambayo husimamia haki na shughuli za vyombo vya habari katika Ukanda huu, imelaani vikali kushikiliwa kwa Amade:

Kuendelea kushikiliwa kwa Abubacar Na jeshi ni uvunjaji wa haki zake pia kukamatwa kwake bila mashtaka rasmi. Serikali ya Msumbiji inaweka historia mbaya ya kuvunja haki za uhuru wa kujieleza na Uhuru wa kupata habari katika ukanda huu.

Shirika la haki za Binadamu Pia walitoa tamko:

Amade Abubacar é um respeitado jornalista que estava a gravar depoimentos de pessoas que fugiram de ataques mortais em Cabo Delgado quando foi preso pela polícia. Esta é a mais recente demonstração de desprezo pela liberdade de expressão e liberdade de imprensa por parte das autoridades moçambicanas, que veem os jornalistas como uma ameaça e os tratam como criminosos.

Amade Abubacar ni mwandishi anayeheshimika ambaye alikuwa akirekodi shuhuda za watu waliokimbia mashambulizi huko Cabo Delgado alipokamatwa na polisi. Hii ni dharau ya hivi karibuni kutoka kwa mamlaka za Msumbiji na zimeelekezwa katika uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari… [mamlaka] zinawaona wanahabari kama maadui na hivyo wanatendwa kama wahalifu.

Kampeni hii imeenea pia huko Twita na imeundiwa hashtagi kama vile #MfungueniAmade kutaka uhuru wa Amade.

Angela Quintal, coordinator wa Mpango wa Afrika kwa Kamati ya Kuwalinda Wanahabari, alimtupia lawama Rais wa Msumbiji:

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.