Msumbiji: Polisi Washambulia Waandamanaji

Siku ya tarehe 6 Aprili, maofisa wa tawi la Polisi wa jamhuri ya msumbiji (PRM) – Kikosi cha Askari Maalum wa Dharura (FIR) – walitumia nguvu kusitisha maandamano ya wafanyakazi wa shirika binafsi la ulinzi Group Four Security (G4S).

inasemekana [pt] kampuni ya G4S kinyume cha sheria imekuwa ikipunguza mishahara ya wafanyakazi wake, na sasa walikuwa wakilalamika kuhusu hali inayozidi kuwa mbaya tangu mwezi Juni 2010. Katika maandamano hayo, wafanyakazi walidai malipo waliyokatwa kiholela na mwajiri, kadhalika malipo ya bonasi kwa ajili ya likizo na malipo ya kazi baada ya saa za kazi.

Screenshot from the video featuring FIRs violent intervention. Available on Youtube by verdadetruth.

Picha za skrini kutoka kwenye video inayoonesha vurugu zilizofanywa na FIR wakati walipovamia. Zinapatikana kwenye YouTube kwa kupitia verdadetruth.

Kwenye Facebook, mwanasheria Hbro Chipas anasema mgomo huo wa wafanyakazi ulikuwa kinyume cha sheria, kwani haukuitishwa kwa mujibu wa “kile kinachohitajiwa na sheria”. Chipa anachambua shauri hilo, na kudai kuwa kuna “mitazamo miwili” [pt] juu ya shambulio lile:

a da violência gratuita protagonizada pelos agentes da FIR, e a outra, os estragos perpetrados pelos seguranças

Ule wa vurugu zisizo na sababu za Askari Maalum wa Dharura, na mwingine, ule wa hasara zilizosababishwa na wafanyakazi wa ulinzi (wa Group 4).

Katika maoni kwenye ukurasa waFacebook wa gazeti la @Verdade, mpiga picha Hugo Costa anaafiki maono ya Chipas.

Uns acham que “fazer greve” significa que têm o direito de agir como selvagens e vandalizarem tudo o que encontram pela frente destruindo propriedade privada e agredindo quem não tem nada a ver com o que reivindicam; e os outros acham que “intervenção policial” significa ter luz verde para demonstrações de violência gratuita e abuso de autoridade gozando de plena imunidade!!

Wengine wanafikiri kwamba kugoma (kuandamana) kunamaanisha kwamba wana haki ya kutenda kama watu wasistaarabika na kuharibu kila kitu kilicho mbele yao kuharibu mali binafsi za watu ambazo hazina uhusiano wowote na madai yao; na wengine wanafikiri kwamba “Kuhusika kwa Polisi” kunamaanisha taa ya kijani kwa waandamanaji inayoruhusu vurugu zisizo na sababu na kutusi mamlaka huku wakifaidi kinga (ya sheria)!!

Kando ya “mitazamo hiyo miwili” iliyotolewa, Chipas aliona kuwa vitendo vya askari polisi dhidi ya waandamanaji kuwa ni vya kikatili na kuongeza:

espero que as autoridades competentes nao fiquem impávidas e serenas perante essa situação deveras chocante. Aquele senhor  nao constituía nenhum perigo futuro nem iminente, não fornecendo qualquer tipo de resistência.

Natumaini kuwa vyombo vyenye uwezo havitabaki kimya bila ya kusukumwa na hali hii kusitusha. Mtu yule hakuwakilisha hatari yoyote wakati wa baadae, na hakufanya kitendo chochote cha kupinga (kukamatwa).

Katika video ya TVM, unaweza kuona vitendo vya vurugu vya maofisa wa kikosi cha Askari Maalum wa Dharura ambao walimvamia mlinzi wa G4S ambaye alikuwa tayari amekwisha zidiwa nguvu na kuwekwa kwenye gari ya polisi.

Video hii ilizusha maoni kadhaa ya kuchukizwa kwenye vyombo vya habari vya kiraia, na kwa kiasi kikubwa kupitia Facebook ndio watu wengi wa Msumbiji, na wageni, walipoonesha kuchukizwa kwao na vitendo vile vya nguvu na vurugu.

Akirejea tamko [pdf] la Liga Moçambicana de Direitos Humanos (LDH) [Jumuiya ya Haki za Binadamu] – ambayo inadai ufanywe uchunguzi wa wale waliohusika na shambulio na kufukuzwa kazi kamanda wa kikosi cha Askari Maalum wa Dharura, Jenerali Binda – mwanasaikolojia Linette Olofsson aliandika:

inaceitável num Estado de Direito! Faz-me lembrar dos tempos da ditadura em Moçambique, 1975-1994 onde não se respeitava os Direitos Humanos; (ainda hoje são violados com se vê) O comandante da FIR deve ser demitido imediatamente. Segundo a LDH, este mesmo Comandante fez estragos na Província de Nampula. O nosso Estado ainda é dominado por militaristas camuflados de democratas! São horríveis estas cenas.

Haikubaliki chini ya utaratibu sheria! Inanifanya nikumbuke wakati wa utawala wa kidikteta nchini Msumbiji, 1975-1994 ambapo haki za binadamu zilikuwa hazishemiwi; (na hata leo tunaona zinavyokiukwa). Kamanda wa kikosi cha Askari Maalum wa Dharura anatakiwa afukuzwe kazi mara moja. Kwa mujibu wa LDH, kamanda huyu huyu ndiye aliyefanya uharibifu kule Nampula. Jimbo letu bado linatawaliwa na wanajeshi wanaojionesha kama wanademokrasia. Picha hizi ni za mbaya mno.
Relatório da Amnistia Internacional "Licença Para Matar - Responsabilização da Polícia em Moçambique" (2008) .pdf

Watu wanaogopa polisi zaidi ya wanavyoogopa wahalifu”, Ripoti ya Shirika la Kimataifa la Haki za Binadamu (Amnesty International report) “Leseni ya Kuua – Uwajibishwaji wa Polisi nchinin Msumbiji” (2008).pdf

Nchini Msumbiji vurugu zinazofanywa na maofisa wa polisi ambao wanapaswa kutunza sheria na amani si jambo geni, kama inavyooneshwa katika ripoti ilichapishwa mwaka 2008 na Shirika la Msamaha la Kimataifa – Kibali cha Kuua. Mwaka mmoja baadaye, 2009, taarifa nyingine ya Shirika hilo – Siamini Tena Katika Haki (Já não acredito na Justiça [Pt])- inaorodhesha ‘kesi mbalimbali za mauaji yaliyofanywa na polisi nchini Msumbiji”.

Kesi nyingine inayofanana na hii ya wafanyakazi wa G4S ilitukia mwezi Aprili 2009, wakati askari polisi alipowafyatulia risasi wafanyakazi wa ujenzi waliogoma [Pt]. 

Kadhalika wakati wa mapinduzi ya umma ya Septemba 1 na 2 ya 2010 (yaliyoripotiwa na Global Voices) polisi walifyatua risasi dhidi ya waandamanaji, na kuua watu 11, kwa mujibu wa taarifa [Pt] iliyotolewa na Kituo Cha Maaadili ya Umma.

Mwanafunzi, Oflia Macie, alitoa maoni haya:

Estes polícias pensam que podem fazer o que quiserem e nada é feito por eles…eu pessoalmente ja vi 2 polícias em Tete agora em fevereiro batendo em dois miudos dos seus 12 e 13 anos de idade so porque não tinham BI, aí sairam chapadas, murros, pontapés e ate bateram-lhes com a própria AKM, quando viram que os miudos ja estavam a sangrar levaram-nos para a 1ª Esquadra… eu pergunto eles estao para proteger, fazer justiça? ou para pôr terror a população?? E estes da FIR são os piores selvagens!!

Hawa polisi wanafikiri wanaweza kufanya lolote wanalotaka na hakuna litakalofanyika dhidi yao… Mimi binafsi niliwaona polisi 2 kule Tete mwezi Februari wakiwapiga watoto wawili wenye umri wa miaka 12 na 13 kwa sababu tu hawakuwa na kadi za vitambulisho, kwa hiyo waliachwa wapigwe, masumbwi, mateke na pia walipagiga hata na bunduki zao za AK, na walipoona watoto wale wanatoka damu, waliwapeleka kituo cha polisi… Ninauliza wapo hapa ili kutoa kulinda au kutoa hukumu? Au kutisha watu? Na hawa FIR ni wabaya zaidi kuliko watu washenzi!!

Wakati wa shambulio la polisi dhidi ya wafanyakazi wa G4S, waandamanji 24 walitiwa nguvuni na wamefungwa ndani ya mahabusu ya kata ya 18 ya polisi. Habari ambazo hazijathibitishwa [Pt] zinaashiria kuwamfanyakazi mmoja wa G4S amepoteza maisha wakati alipokumbwa na vipigo wakati wa shambulio lile la kikatili. Mpaka sasa, maofisa wote wa FIR wapo huru.

Juu ya habari za kifo cha mlinzi wa shirika hilo, kwenye Facebook Inusso Mario Jojo Mutambe alitoa rai ya kuhamasisha umma

toda G4S a nível nacional deveria fazer uma marcha atê a FIR

Wafanyakazi wote wa G4S kitaifa waandamane dhidi ya FIR

Mtaalamu wa mawasiliano na masoko Celso Miguel alielezea kuchukizwa kwake

até quando teremos de viver com essas impunidades??? uma vida se foi, uma mulher ficou viúva, crianças ficaram sem pai, o país perdeu um cidadão… esses polícias se esquecem que os impostos que aquele indivíduo descontava, todo santo mês, servia também para pagar o salário dele??? nunca soube! sinceramente, quem se responsabiliza????? QUEM????… é revoltante ver uma coisa destas acontecer no nosso país!!!! Quem nos devia defender é quem nos mata!!!!

Je kwa muda gani tuishi na hali hii ya (polisi) kutoadhibiwa ??? Maisha yamepotea, kuna mwanamke aliyefanywa mjane, watoto waliochwa bila ya baba, nchi imempoteza raia… hawa polisi wanasau kuwa kodi alizolipa mtu huyu, kila mwezi wenye Baraka, ndio pia zilizolipa mishahara yao??? Sijui! Kwa dhati, ni nani atakayewajibika???? NANI????… inakera sana kuona kitu kama hiki kinatukia nchini kwetu!!!! Wale wanaotulinda ndio wanaotuua!!!!

Kwa Ivone Gonçalves bado kuna vizingiti vingi katika utekelezaji wa haki za binadamu nchini Msumbiji. Hana matumaini katika yale yanahusiana na haki, analalamika:

Infelizmente o Ministro do Interior nada vai fazer para punir os agressores e como sempre vão ficar impunes porque não existe justiça no nosso País. A justiça só funciona para o ladrão de galinha!

Kwa bahati mbaya Wizara ya mambo ya Ndani haitafanya lolote kuwaadhibu washari na kama kawaida (washari hao) watafaidi hali ya kutoadhibiwa kwa sababu hakuna haki nchini. Sheria inafanya kazi kwa wezi wa kuku tu!

Kuhitimisha, Boa Matule anatoa wito wa kuungana dhidi ya vitisho:

Isto é resultado de uma força politizada e cujo único objectivo é intimidar as pessoas! Mas a verdade é que nós somos maiores que eles! Unidos podemos revolutionar Moz [Moçambique].

Haya ni matokeo ya jeshi la kisiasa lenye lengo pekee la kuwatisha watu! Lakini ni kwamba sisi wakubwa zaidi yao! Pamoja tunaweza kuikomboa Msumbiji.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.