Mabadiliko ya Mfumo wa Ustawi wa Jamii ya Kiafrika

Makala haya ni sehemu ya Habari zetu Maalumu za Maendeleo ya Kimataifa .

Kwa kuzingatia mjadala ulioanzishwa na Marekebisho ya sera ya huduma za afya ya jamii nchini Marekani na kujiondoa taratibu kwa nchi ya Ufaransa kutoka kwenye mipango ya jamii inayoendeshwa kwa kodi za wananchi, mtu anaweza kudhani kwamba hifadhi ya jamii ni dhana inayoanza kupitwa na wakati. Kinyume na matarajio, haki ya kuhakikishiwa hifadhi ni kipengele muhimu katika Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu (Ibara ya 22) na sehemu yenye unyeti katika of the utekelezaji wa Malengo Makuu ya Kimaendeleo ya Milenia (MDG), yaliyobuniwa na Umoja wa Mataifa.

Kwa nchi nyingi za ki-Afrika, mifumo ya ustawi wa jamii bado inaendelea kukua. Kila serikali ya nchi za Afrika imechagua mfumo mahususi unaoendana na utamaduni wake, wenye viwango tafauti vya mafanikio, lakini zikitambua umuhimu wa kulinda angalau kwa kiwango cha chini, idadi kubwa ya watu wanaokabiliwa na vitisho mbalimbali.

Mfumo wa hifadhi ya jamii usiokidhi haja

Assane Fall-Diop anaweka muhtasari wa jitihada ambazo bado zinahitajika kufikia mfumo wa kweli wa ustawi wa jamii barani Afrika: [fr]:

La protection sociale est devenue un thème obligé des débats électoraux en Afrique. En Côte d’Ivoire et en République démocratique du Congo, la Constitution ou la loi font même de l’assurance-maladie un objectif prioritaire. Cependant, l’essor de l’économie informelle et la faiblesse politique et financière des Etats handicapent les réalisations concrètes [..] En Afrique, « seulement 5 % à 10 % de la population active bénéficie d’une couverture sociale », selon l’Organisation internationale du travail (OIT), qui note une dégradation de la situation au cours des vingt dernières années. L’organisation souligne que « près de 80 % de la population n’a pas accès aux soins de santé de base ».

Ajenda ya Hifadhi ya jamii imekuwa sera muhimu kwa mijadala ya uchaguzi barani Afrika. Nchini Cote d’Ivoire na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ama katiba au sheria zinafanya bima ya afya kuwa kipaumbele katika mipango ya maendeleo. Hata hivyo, uchumi usio rasmi unaokua kwa kasi na udhaifu wa kifedha na kisiasa wa nchi za Afrika vyote kwa pamoja vinakwaza ufikiwaji wa maendeleo ya kweli. Barani Afrika, “ni asilimia 10 tu ya wafanyakazi wamejiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii,” kwa mujibu wa Shirika la Kazi la Umoja wa Mataifa (ILO), linabainisha kwamba hali imezorota katika miongo miwili iliyopita. Shirika hilo linasisitiza kwamba “karibu asilimia 80 ya watu hawapati huduma za afya ya msingi.”

 

End of the month pension queues. Clermont Township, Kwazulu-Natal, South Africa by HelpAge on Flickr (CC-license-BY).

Misururu ya kungoja mafao ya uzeeni mwisho wa mwezi. Mji mdogo wa Clermont, Kwazulu-Natal, nchini Afrika Kusini imewekwa na HelpAge kwenye mtandao wa Flickr (CC-license-BY).

Lambert Gbossa, naibu mkurugenzi wa Ofisi ya Kanda ya Afrika ya ILO, anaeleza kwa nini anadhani kwamba ustawi wa jamii unaendelea kuzorota barani kote. Kupanuka kwa uchumi usio rasmi, kwa maoni yake, ni moja ya sababu kuu [fr]:

d’abord, une poussée démographique galopante qui produisit chaque année des cohortes de primo-demandeurs d’emplois; ensuite, une crise économique grave proche de la récession qui a réduit à néant les capacités d’absorption du secteur moderne; enfin, la poussée de l’exode rural obligeant bon nombre d’individus à venir «bricoler» dans les villes. Ainsi, la population active atteint plus de 40 pour cent dans l’ensemble des pays, avec un taux d’accroissement de plus de 4,5 pour cent, légèrement supérieur à celui de la croissance démographique. Au rythme actuel d’évolution des données sur la population active et sur la population salariée, le taux d’occupation des travailleurs salariés pourrait n’être plus que 2 à 3 pour cent au maximum dans les 25 prochaines années. Comme cette population est la seule à bénéficier d’un système organisé de sécurité sociale, il y a ainsi une dégradation prévisible de la rentabilité sociale du système de couverture.

Kwanza, ongezeko kubwa la kila mwaka la idadi ya watu linalozalisha kundi kubwa la watafuta kazi ambao hawajawahi kuajiriwa; pili, mtikisiko mkubwa wa kiuchumi, unaosababisha kuanguka vibaya kwa uchumi, ambao umezorotesha uwezo wa kusharabu sekta ya kisasa; mwisho, kuhama kwa maelfu ya waty kutoka vijijini na kuja “kuzurura” mijini. Kwa namna hii, nguvu kazi imeongezeka kutoka asilimia 40 katika nchi zote, kwa kasi ya ukuaji inayozidi asilimia 4.5, ambayo ni juu kidogo kuliko kasi ya ongezeko la watu. Kwa ongezeko hilo, ongezeko la muda ambao walio na ajira wataendelea kubaki katika nafasi zao linaweza kuwa zaidi ya asimilia 2 mpaka 3 katika miaka 25 ijayo. Kwa kuwa idadi hii ya watu inaweza kuwa ile inayotarajiwa kufaidika na mifumo ya hifadhi ya jamii, kuna uwezekano dhahiri la kushuka viwango vya manufaa ya mifumo inayohusika kwa jamii.

Maendeleo yasiyolingana barani kote

Hatua zimechukuliwa kupunguza uduni huu wa maendeleo ya mfumo wa ustawi wa jamii kwa Afrika. Jukwaa la Afrika kwa Hifadhi ya Jamii (APSP) linataka kuona hatua madhubuti kukuza na kuimarisha mkataba wa kijamii kati ya nchi na wananchi wake. APSP inapendekeza [fr]:

tout programme doit être conçu à partir des structures existantes, y compris les systèmes classiques de protection sociale. En parallèle, la Plateforme insiste sur le fait que les défis de l’intégration régionale et notamment ceux liés à la portabilité des droits sociaux ne pourront être surmontés qu’à la condition que l’évaluation des réalités et opinions locales et nationales s’accompagne d’approches régionales et continentales

Kwa jukwaa hili la APSP, ubunifu wa mpango lazima ujengwe katika miundo iliyopo tayari, ukihusisha mifumo ya zamani na hifadhi ya jamii. Kwa wakati huo huo, jukwaa hili linasisitiza kwamba uzingativu huu wa hali ya kitaifa na maeneo mengine na utambuzi uendelee kwenda sambamba na mielekeo tofauti ya maendeleo ya kimaeneo na kwa bara zima kwa ujumla.

Hata hivyo, Lambert Gbossa anaguswa juu ya hatari inayoletwa na utayari wa kutoa mfumo bora wa ustawi bila kutazama masuala yanayohusiana na eneo moja moja na bila mjadala shirikishi
[fr]:

..la question de la réforme de la protection sociale dans les pays d'Afrique se pose avec acuité, elle s’est cantonnée à l'intérieur du système actuel et a rarement essayé de s'intégrer dans une politique globale. Le résultat de ce cantonnement est non seulement une marginalisation de l'immense majorité de la population mais surtout, la perpétuation d’un modèle extraverti et parfois incompris qui a fait de la protection sociale au profit du secteur formel l’essentiel et non le complément d’une problématique plus conforme aux identités. Les schémas très techniques et parfois très formels sont conçus en dehors des populations et n’ont pas été conformes au plan national de développement intégré..

…suala la kurekebisha mfumo wa ustawi wa jamii katika nchi za Afrika ni mujarabu. Suala hili limefungamanishwa na mfumo uliopo na mara chache sana umejaribu kujiweka katika sera pana. Matokeo ya mfungamanisho huu si tu kutengwa kwa idadi kubwa ya watu, lakini lililo muhimu zaidi ni kuendelea kwa mtindo usioeleweka mara nyingi kwamba kipaumbele kwenye hifadhi ya jamii ni kwa ajili ya sekta rasmi na sio kwa ajili ya matatizo yanayofanana. Mifumo yenye utaalamu sana na mara nyingi iliyo rasmi ilibuniwa nje ya watu hao na haikuwa sehemu ya mpango wa taifa wa maendeleo kamilifu

Sehemu ya utekelezaji wenye mafanikio

Kabla Mali haijatikiswa na migogoro ya sasa ya kisiasa , nchi hiyo ilipiga hatua kubwa za kimaendeleo katika suala la hifadhi ya jamii na utoaji huduma za afya. Video ya mpango wa kuboresha matibabu ya kisukari nchini Mali unaoendeshwa na AZISE iitwayo Santé Diabète Mali, inaonyesha mfano wa hatua yenye matokeo bora katika utoaji wa huduma ya jamii:


Bima ya lazima ya afya ilianzishwa nchini Mali mwaka 2010. Mpango huu uliowezesha hifadhi bora kwa watu masikini na walio pembezoni , lakini hata hivyo mpango huo haukuimarisha mihimili mingine miwili kwa ustawi wa jamii nchini Mali: maendeleo ya miundombinu ya uzalishaji na uimarishaji wa marekebisho ya kimfumo. Fedha inabaki kuwa moja ya vikwazo vinavyoathiri uendelevu wa mipango hii ya kijamii.

Hivi sasa, nchini Burkina Faso mifuko kwa ajili ya ustawi wa jamii inaendelea kuanzishwa. Kanuni kuu ya mfumo ya hifadhi ya jamii inategemea nyenzo mbili muhimu: huduma na hawilisho. Olivier Louis dit Guérin anatafsiri vyenzo mbili
[fr]:

- Accès géographique et financier aux services essentiels : eau, assainissement, santé, alimentation, éducation, logement, épargne, assurance
– Transfert sociaux versés aux enfants, personnes âgées et personnes actives disposant d'un revenu insuffisant pour les services essentiels mentionnés précédemment.

- Huduma: upatikanaji wa kifedha na kufikika kwa huduma muhimu kama maji, kuondoa uchafu, afya, chakula, elimu, nyumba, akiba, bima
– Hawilisho: ruzuku ya ustawi wa jamii kwa watoto, wazee na watu wenye uwezo wa kufanya kazi wapatao chini ya kiasi kinachotosha kupata huduma muhimu zilizotajwa hapo juu.

Katika utafiti unaolinganisha mifumo ya ustawi wa jamii nchi Rwanda na Burundi, Solidarité Mondiale anahitimisha kama ifuatavyo kuhusiana na ustawi wa jamii katika nchi hizi jirani [fr]:

L’étude comparative des systèmes de protection sociale du Rwanda et du Burundi a clairement montré que le Rwanda a déjà réalisé des pas importants dans ce secteur clé qui sont aujourd’hui portés par une forte volonté politique et bénéficient d’un encadrement soutenu de la Cellule Technique d’Appui aux Mutuelles de santé au sein du Ministère de la Santé. La complémentarité fortement encouragée par les pouvoirs publics entre le système étatique de protection sociale, actuellement en pleines réformes, et les systèmes communautaires des mutuelles de santé extrêmement avancés au Rwanda, constituent un atout très important du processus de renforcement et d’extension des systèmes de protection sociale [..] Le Burundi, à la suite d’une guerre prolongée, n’a pas pu renforcer les systèmes existants de protection sociale en vue de leur extension au secteur informel et rural. Néanmoins, à certains égards, certaines initiatives privées ont fait des avancées remarquables dans ce domaine. le Burundi devraient l’inciter à privilégier des systèmes de protection sociale à forte participation populaire, s’il veut en garantir l’appropriation et la durabilité. En effet, la tentation peut être très grande de mettre rapidement en place un système de couverture universelle largement soutenue par les bailleurs de fonds externes.Le retrait de tels bailleurs peut rapidement conduire à la catastrophe comme cela a déjà été le cas pour certaines provinces du pays.

Utafiti unaolinganisha mifumo ya hifadhi ya jamii nchini Rwanda na Burundi unaonyesha vizuri kwamba Rwanda tayari imepiga hatua kubwa katika sekta hii muhimu ambayo imewezeshwa na utashi thabiti wa kisiasa na unaonufaika na msaada wa wafanyakazi wa kitengo cha utaalamu cha (CTAMS—la Cellule Technique d’Appui aux Mutuelles de Santé) ndani ya Wizara ya Afya. Serikali inaunga mkono ushirikiano wa kitaalamu baina ya mfumo wa serikali wa hifadhi ya jamii, marekebisho yanayoendelea, na mfumo wa bima ya afya inayojikita kwa jamii. Ushirikiano huu ni dalili njema kwa maendeleo ya kuboresha na kupanua mifumo ya hifadhi ya jamii […] Burundi, kufuatia mapigano ya muda mrefu, haikuweza kusaidia mifumo iliyopo ili kuweza kuipanua kuzifikia sekta zisizo rasmi na vijijini. Hata hivyo, miradi fulani binafsi imefikia mafanikio makubwa katika tasnia hii. Kama inalenga kuhakikisha umiliki na uendelevu, Burundi ni lazima iruhusu kuweka kipaumbele katika mifumo ya hifadhi ya jamii kupitia ushirikishwaji imara na unaokubalika. Inaweza kuwa changamoto kurekebisha mfumo wa upatikanaji wa kimataifa, ambao kwa kiasi kikubwa umefadhiliwa na wahisani wa nje. Kutokupatikana kwa fedha ikiwa wahisani watajitoa kunaweza kusababisha janga kubwa, kama ambavyo tayari imetokea katika baadhi ya majimbo nchini humo.

Makala haya ni sehemu ya Habari zetu Maalumu za Maendeleo ya Kimataifa .

Picha inayoonekana inaonyesha uchunguzi hospitali kwa wanawake na watoto, nchini Cote d'Ivoire, imewekwa kwenye mtandao wa Flickr na Mkusanyiko wa Picha wa Benki ya Dunia (CC BY-NC-ND 2.0).

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.