Huduma za Afya nchini Madagaska Zinaweza Kukabiliana na Mlipuko wa Ebola?

Chauve souris à Madagascar - via wikipédia Public Domain

Popo anayepatikana Madagaska. Picha: Wikipedia kwa matumizi ya umma

Vita dhidi ya mlipuko wa Ebola inaendela kugeuka kuwa dharura ya kimataifa. Idadi ya wahanga wa ugonjwa huo inaongozeka kwenye nchi tatu zilizoathiwa zaidi huko Afrika Magharibi: Guinea, Liberia na Sierra Leone. Wagonjwa kadhaa wameripotiwa kupoteza maisha kwenye Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Najeria. Shirika la Afya Duniani linaripoti kwamba maradhi haya hatari zaidi kwenye historia ya homa inayosababishwa na virusi tayari imepoteza maisha ya watu zaidi ya 2,800 kati ya wagonjwa 5,833  kufikia tarehe 20 Septemba.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limefikia azimio 2177 la kupambana na janga hilo linalohatarisha afya ya jamii. Mnamo Septemba 18, nchi zipatazo 131 zilifadhili azimio hilo, linalotambua “kiwango kisichokubalika cha mlipuko wa Ebola barani Afrika ” na kueleza kuundwa kwa mpango maalum uitwao Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Kushughulikia masuala ya Ebola (UNMEER). Rais wa Marekani Barack Obama ametangaza kwamba anatuma vikosi 3,000 kwenda Afrika Magharibi, kwa lengo la kukabiliana na hali hiyo inayozidi kuwa mbaya, kufuatia kuenea kwa kasi kubwa kwa virusi vya ugonjwa huo.

Nchi nyingine Barani Afrika zina wasiwasi na uwezekano wa kuenea kwa maradhi hayo katika nchi zao, ingawa vifaa vya afya havionekani kuwa tayari kupambana na ugonjwa huo. Utafiti unaonesha kwamba nchi 15 ziko kwenye hatari sana ya kupata maradhi hayo , kwa sababu ya kuwa na mazingira yanayofanana na mazingira yaliyo kwenye nchi zilizoathirika.

Hali ni hiyo hiyo nchini Madagaska, ambako mashua kutoka Liberia ikidaiwa kubeba watu wenye virusi vya Ebola hivi karibuni ilitua kwenye bandari ya Toamasina. Mkutano wa dharura ulifanyika jijini Antananarivo tarehe 5 Agosti kutazama kwa karibu tahadhari zinazoweza kuchukuliwa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya nchini Madagaska Philémon Tafangy alitambua hatari: 

Un pays comme le nôtre n’est pas à l’abri des risques, même si la zone d’expansion du virus est assez éloignée de nous

Nchi kama yetu haiko salama na hatari hii [Ebola], pamoja na umbali wetu na eneo liloathirika

Waziri Mkuu Kolo Roger, hata hivyo, ameeleza kwamba mifumo ya afya iko imara kushughulikia majanga hayo kama yatajitokeza na mpango wa dharura  uko tayari

Ce plan contient les scénarios et les dispositions nécessaires pour faire face notamment aux épidémies de fièvres hémorragiques virales telles que la maladie à virus Ebola. 

Mpango huu unajumuisha maeneo na hatua zinazohitajika kwa ajili ya kupambana na magonjwa yanayoenezwa na virusi kama vile Ebola. 

Chambre d' hôpital à Mandritsara, Madagascar - CC BY 2.0

Chumba cha Hospitali huko Mandritsara, Madagaska – CC BY 2.0

Lakini inaonekana kwamba miundo mbinu ya afya nchini Madagaska haitaweza kuhimili mlipuko wa maradhi hayo kama utatokea. Waziri Mkuu ameamua kupuuza tahadharani za wanasayansi, akitegemea zaidi taarifa za sehemu za udhibiti kwenye viwanja vya ndege, akisema kwamba mazingira ya afya ya umma nchini Madagaska yamelindwa kwa sababu ya kutokuwepo kwa ndege zinazoingia nchi humo kutoka kwenye maeneo yanayokabiliwa na mlipuko wa maradhi hayo.

Wanasayansi wanasema kwamba virusi vya Ebola huenea kwa namna tofauti. Kwa hakika, chapisho la hivi karibuni  linaeleza namna gani ugonjwa unaweza kuenea kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu: popo walao matunda wanaweza kubeba virusi hivyo bila wao kuonesha dalili za maradhi hayo, na wanaweza kuhama na kueneza virusi hivyo kwenda kwa wanyama wengine, kama vile nyani na pimbi. Wakati mwingine nyani huliwa na watu waishio porini nchini Madagaska. Ingawa ulaji wa nyama si lazima uwe ni chanzo cha Ebola, uandaaji wa nyama mbichi ambazo zinaongeza uwezekano wa maambukizi. Ilaym, mwanablogu anayeishi Antananarivo anayeandikia blogu ya DailyMg, anaeleza kwa nini wa-Malagasi wako kwenye hatari ya maambukizi ya virusi vya Ebola. Anaorodhesha sababu chache : 1) Baadhi ya Walagasi huwinda na kula popo na wanyama wengine 2) kwa sababu ya famadihana, a mila ya kuwafukua wafu kutoka kwenye makaburi yao.

 Léa Ratsiazo wa Antananarivo alihoji kwenye safu yake iliyoko kwenye jarida la Madagascar Tribune kuhusu uwezo halisi wa nchi hiyo wa  kudhibiti uwezekano wa kuenea kwa Ebola nchini Madagaska, kufuatia matukio ya hivi karibuni kwenye hospitali iliyoko jijini Antananarivo:

On ne demande qu’à le croire car quasiment au même moment où il fait cette déclaration à la presse, une équipe de chirurgiens étrangers oeuvrant dans l’humanitaire le contredit involontairement. Il s’agit d’une équipe composée de 11 chirurgiens qui réalisent des œuvres humanitaires à travers plusieurs pays du monde dont Madagascar. Ils réalisent gratuitement des interventions chirurgicales en faveur des patients qui en ont besoin dans les pays qu’ils visitent en partenariat avec les hôpitaux locaux. L’hôpital HJRA d’Antananarivo, qui est le plus grand centre hospitalier de Madagascar est choisi pour ce partenariat sauf que les responsables de HJRA ont oublié de communiqué au public l’évènement. Résultat : aucun patient n’est venu. Ils ont quand même pu avoir 2 patients de HJRA au lieu des 25 prévus quotidiennement. Agacés, ces chirurgiens ont précisé qu’ils ne sont pas venus pour passer ici des vacances mais pour aider les autres, le moindre des choses serait de communiquer et de sensibiliser le public, d’ailleurs ils ne comprennent pas du tout que les patients à opérer prennent en charge tous les médicaments et autres outils nécessaires pour l’intervention. Ils notent aussi d’ailleurs que le HJRA manque cruellement de matériels de base pour des interventions chirurgicales.

Hiyo inahitaji kuamini kwa kiasi fulani, kwa sababu karibu wakati ule ule alipokuwa anatoa taarifa yake kwa waandishi wa habari, timu ya wapasuaji ya kigeni inayojihusisha na kazi za kibinadamu walisema jambo lililotofautiana na matamshi yake. Hii ilikuwa ni timu ya wapasuaji 11, wanaofanya kazi za kibinadamu katika nchi mbalimbali duniani, ikiwemo Madagaska. Walifanya upasuaji bure kwa wagonjwa waliokuwa na uhitaji katika nchi walizozuru, kwa ushirikiano na hospitali za wenyeji. Hospitali ya HJRA jijini Antananarivo, ambayo ni kituo kikuu cha afya nchini Madagaska, kilichaguliwa kwa ushirikiano huo, lakini maafisa wa HJRA walisahau kuwajulisha watu ukweli huu. Matokeo yake, hakuna mgonjwa alijitokeza. Madaktari hao wakaishia kupata wagonjwa wawili wa hospitali hiyo badala ya wagonjwa 25 kwa siku. Wapasuaji hao walifedheheshwa, wakisema kwamba hawakuwa wamekuja kwa likizo, ila kuwasaidia wananchi kupata uelewa. Vile vile waliokuwa na wasiwasi kwamba wagonjwa waliokuwa wanahitaji kufanyiwa upasuaji walitakiwa kulipia dawa zote na vifaa vyote vilivyohitajika kwa ajili ya upasuaji. Kwa yongeza, ilionekana kwamba hospitali ya HJRA ilikuwa na upungufu mkubwa wa vifaa vya msingi kwa ajili ya shughuli za upasuaji.

Le Mouvement des Citoyens Malagasy de Paris MCM (Muungano wa raia wa ki-Malagasi waishio Paris) kadhalika haukuelewa nani wa kumwamini kuhusiana na hatari ya mlipuko wa Ebola nchini Madagaska: Waziri Mkuu Kolo anayedai hakuna hatari yoyote au wanasayansi watafiti wanaoijumuisha Madagaska kwenye mataifa yenye hatari?

Kwa hiyo, wakati mpango wa dharura upo, bado inahitaji kuangaliwa ikiwa Madagaska imeweza kuandaa raslimali zinazohitajika kuutekeleza mpango huo.  

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.