Habari kuhusu Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kutoka Februari, 2015
Asasi ya Kiraia Inayofuatilia Bunge Yawaunganisha Wabunge Wanawake na Wananchi wa Uganda
Asasi ya Kiraia ya Parliament Watch Uganda iliandaa mjadala wa kujadiliana na wabunge wanawake kwenye mtandao wa Twita kuhusu mada 'Kuwafanya Wanawake Wathaminiwe Kwenye Shughuli za Kibunge'.
Ufisadi Uliofanywa na Makampuni Makubwa Katika Kupambana na Ebola Nchini Sierra Leone
Makampuni matano nchini Sierra Leone yanasemekana kutumia fedha zilizokusudiwa kupambana na Ebola kwa njia za kifisadi: Haya hapa makampuni matano yaliyokuwa yameingia mikataba mikubwa ya kusambaza vifaa na kutoa huduma...
Wanafunzi Nchini Tanzania Kufundishwa kwa Lugha ya Kiswahili, si Kiingereza
Rais Jakaya Kikwete amezindua sera mpya ya elimu nchini Tanzania juma lililopita, ambayo pamoja na mabadiliko mengine, inaingiza rasmi Kiswahili kama lugha ya kufundishia na kujifunzia katika mfumo wa elimu.
Mwanamke Atumia Mtandao wa Instagram Kubadili Mtazamo Kuhusu Somalia
Ugaaso Boocow anataka kubadili mtazamo wa watu kuhusu nchi ya Somalia. Lakini badala ya kuingia mitaani au kutumia radio, ameamua kuingia kwenye mtandao wa Instagram na anakuwa maarufu humo.
Mapendekezo Yanapokelewa kwa Ajili ya Mwezi wa Historia Nyeupe 2015
Likiwa limeandaliwa na blogu ya Africa is a Country [Afrika ni Nchi], tukio la Mwezi wa Historia Nyeupe linajongea mwezi ujao: Mwezi Machi mwaka jana ndio ulikuwa mwezi wa uzinduzi...
2015 Mwaka wa Kufanyika Chaguzi Huru na Haki Barani Afrika
Wekesa Sylvanus anataraji kwamba 2015 utakuwa mwaka wa chaguzi huru na haki barani Afrika: https://wekesasylvanus.wordpress.com/2015/02/18/will-2015-be-a-year-of-free-and-fair-elections-in-africa/ Tangu kurejeshwa kwa mfumo wa demokrasia ya vyama vingi barani Afrika, ushindani nyakati za uchaguzi...
Je, Kuahirishwa kwa Uchaguzi Mkuu Naijeria Kunatokana na Sababu za Kiusalama?
Jeshi la Nigeria litaendesha operesheni maalum ya wiki sita dhidi ya Boko Haram ili"kuepusha kuingiliwa na shughuli za uchaguzi." Baadhi ya watu wanatilia shaka kuwa, kuahiririshwa kwa uchaguzi ni mkakati wa kisiasa.
Wachoraji 10 wa Kiafrika wa Vitabu vya Watoto Unaopaswa Kuwajua
Jennifer Sefa-Boakye anasaili orodha ya washindani 10 bora zaidi wa tuzo ya Golden Baobab kwa Wachoraji wa Kiafrika: Mwaka jana shirika la Afrika lenye makazi yake nchini Ghana, Golden Baobab,...
Filamu: ‘Sanaa ya Ama Ata Aidoo’
The Art of Ama Ata Aidoo ni filamu iliyotayarishwa na mtayarishaji wa filamu Yaba Badoe: The Art of Ama Ata Aidoo, inasaili mchango wa kisanii wa mmoja wa waandishi wanawake...
Hofu ya Yaliyotokea? Likizo ya Rais Mpya wa Zambia Yaibua Mjadala wa Afya Yake
Raia wa Zambia wanajiuliza maswali kuhusu afya ya Rais Lungu, pamoja na cheti cha afya kuonesha yu mzima, kufuatia likizo yake majuma mawili tu tangu ashike madaraka kumrithi Michael Sata, aliyefariki akiwa madarakani.