· Oktoba, 2013

Habari kuhusu Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kutoka Oktoba, 2013

Kampeni ya Mtandaoni ya Kudai Amani Nchini Msumbiji

  24 Oktoba 2013

Blogu ya Mozmaniacos [pt] imezindua kampeni ya mtandaoni ya kudai amani nchini Msumbiji, kufuatia tishio la kuhatarisha amani iliyodumu kwa miaka 20 . Kwa kutumia kiungo habari #MozQuerPaz (#MozWantsPeace), watumiaji wa Facebook, Twitter, na Instagram waanza kuchangia picha zao pamoja na maoni yao kuhusiana na kampeni hii.

Fuatilia SafariYaGariAfrika Mtandaoni

  7 Oktoba 2013

Kikundi cha watengenezaji na wabunifu wa teknolojia kutoka Ulaya ambao wanadadisi ukuaji wa vituo vya teknolojia barani Afrika wanaendelea na safari yao ya gari barani humu. Tazama blogu yao au Tumblr na ufuatilie mjadala kuhusu safari yao kwenye mtandao wa Twita.

Mwenendo wa Mashitaka ya Wanasiasa wa Kenya Mjini Hague

  7 Oktoba 2013

Mashitaka ya Kenya Hague ni mradi wa Dawati la Afrika la Radio Netherlands Worldwide kwa ushirikiano na This is Africa (Hii ni Afrika): Namna gani ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya mwaka 2007 na 2008 ziliathiri maisha yako? Unataka kufahamu nini kuhusu haki ya kimataifa? Changia habari ulizonazo, mawazo...

Hong Kong: Pinga Biashara ya Pembe za Ndovu

  6 Oktoba 2013

Muungano wa watu binafsi na Asasi Zisizo za Serikali zinazoguswa na tatizo la ujangili wa tembo, Hong Kong kwa Tembo, uliandamana Oktoba 4, wakiitaka Hong Kong kuteketeza hifadhi yake ya tani 25 za pembe za ndovu.

#EauSecours: AlamaHabari ya Kufanyia Mzaha Tatizo la Maji Dakar, Senegal

  4 Oktoba 2013

Dakar, mji kuu wa Senegal, umekumbwa na uhaba wa maji kwa siku 15 zilizopita  [fr]. Wa-Senegali katika mitandao ya kijamii wanazoea tatizo hili kwa kufanyiana utani na uvumilivu. AlamaHabari (Hashtag) #eausecours (#H2OUT) inatumika hivi sasa kwneye mtandao wa twita na  Facebook kutaniana kuhusiana na ukosefu wa maji safi unaoendelea, kama ilivyoonekana...

Zana ya Mtandaoni ya Kuwapima Wagombea Urais Nchini Madagaska

  3 Oktoba 2013

Tovuti ya ki-Malagasi iitwayo Madatsara imetengeneza tovuti utakayotumika kama majukwaa ya kuwapima wagombea wote wa Urais [fr]. Majukwaa yote yametengwa katika mada tisa kuwasaidia wananchi kufanya maamuzi ya busara wakati wa uchaguzi. Uchaguzi wa Rais umepangwa kufanyika tarehe 25 Oktoba, 2013 :