· Julai, 2010

Habari kuhusu Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kutoka Julai, 2010

Niger: Njaa ya Kimya Kimya

  31 Julai 2010

Janga la njaa ambalo kwa kiasi kikubwa haliripotiwi ipasavyo huko Sahel limechukua sura kubwa ya kutisha kufuatia kiasi cha watu milioni 2.5 nchini Naija hivi sasa kuathirika na uhaba wa chakula. Wanablogu nchini Naija wanatafakari janga jingine la chakula baada ya lile la mwaka 2005.

Ivory Coast: Mwanablogu na Mwandishi wa Habari Théophile Kouamouo Akamatwa Pamoja na Timu Yake Tangu Julai 13

  19 Julai 2010

Waandishi wa habari watatu wa Le Nouveau Courrier d'Abidjan walitiwa mbaroni na polisi baada ya kukataa kueleza vyanzo vya habari vya uandishi wao wa kipelelezi kuhusu biashara ya usafirishaji kahawa na kakao kwenda nje ya nchi. Yafuatayo ni maoni kutoka kwa raia na vyombo vya habari nchini Ivory Coast huku wenzao watatu wakiendelea kupigania kuachiwa kwa wanahabari hao.

Afrika ya Kusini: Dakika 67 za Mabadikio – Siku ya Mandela

  18 Julai 2010

Nelson Mandela alitumikia kifungo cha miaka 27 jela kule katika Kisiwa cha Robben, Afrika Kusini. Kitu ambacho watu wengi hawajui ni kwamba Madiba (kama ambavyo wengi wanapenda kumwita huko Afrika ya Kusini) alitumia miaka 67 ya maisha yake katika kupiga vita ubaguzi wa rangi na umaskini. Jumapili hii Julai 18 2010, kutakuwa na maadhimisho ya miaka yake 92 - na pia Siku ya Mandela - siku ambayo watu duniani kote watajitolea dakika 67 ili kuifanya dunia iwe sehemu nzuri ya kuishi kwa wote.

Uganda: Wanablogu Washtushwa na Milipuko ya Mabomu

  15 Julai 2010

Mashabiki wa soka kote ulimwenguni walikusanyika kwenye kumbi za baa na migahawa ili kushuhudia mechi ya fainali za Kombe la Dunia usiku wa Jumapili iliyopita. Nchini uganda usherehekeaji huu ulikatishwa pale milipuko ya mabomu iliposambaratisha maeneo mawili maarufu kwa sherehe za mpaka majogoo jijini Kampala, mji mkuu wa nchi hiyo.

Naijeria: Nani Amemfanya Rais Abadili Msimamo — Facebook au FIFA?

  13 Julai 2010

Baada ya kupokea mamia ya maoni kwenye ukurasa wake wa Facebook page, Rais wa Naijeria alibadili uamuzi wake tata wa kuifungia timu ya taifa ya nchi hiyo. Lakini je ni kweli kwamba kubadilika huku kwa moyo wa Jonathan kulitokana na maoni ya raia waliopaaza sauti zao zenye hasira katika Facebook? Au ulitokana na msukumo wa shirikisho lenye nguvu la mpira wa miguu?

Nigeria: Nigerian President on Facebook

  9 Julai 2010

David Ajao anajadili Ukurasa wa Facebook wa rais wa Naijeria: “Kwa kupitia ukurasa wa Facebook uliofunguliwa tarehe 28 Juni 2010, amekuwa akieleza imani yake katika Naijeria na ndoto yake ya Naijeria.”