· Septemba, 2008

Habari kuhusu Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kutoka Septemba, 2008

Angola: MPLA Yashinda Zaidi Ya Asilimia 80 Ya Kura na Kutwaa Viti 191

  22 Septemba 2008

Tume ya taifa ya Uchaguzi nchini Angola imetoa matokeo ya mwisho ya Uchaguzi wa kwanza wa kitaifa katika miaka 16 na imethibitisha ushindi wa chama tawala, Chama Maarufu kwa Ajili ya Ukombozi wa Angola ambacho kimeshinda viti 191 katika ya viti 220 vya bunge. Angalia baadhi ya maoni.

Angola: Uchaguzi Katika Picha

  22 Septemba 2008

Waangola wako katika uchaguzi kwa mara ya kwanza katika miaka 16 - uchaguzi bado unaendelea Jumamosi hii katika vituo 320 jijini Luanda. Mpaka sasa, hakuna matukio yoyote yaliyoripotiwa, na moyo wa utu umedumu, kama ilivyoangaliwa na mpiga picha Jose Manuel da Silva.

Msumbiji: Mgogoro wa Kisiasa Katika Jimbo la Kati la Beira

  21 Septemba 2008

Waunga mkono wa Renamo wenye hasira walimwagika katika mitaa ya Beira ili kupinga uamuzi wa chama wa kumbadilisha Meya aliyeko madarakani Bwana Davis Simango na kumuweka Manuel Pereira kama mgombea wa kiti cha serikali ya manispaa katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Mwezi Novemba 2009. Mwanahistoria Egidio Vaz anaandika barua ya wazi kwa Rais wa Renamo, Bwana Alphonso Dhlakama katika blogu yake.

Nia ya Mwanablogu Mmoja Kumsaidia Mtoto Kamba huko Madagaska

Sauti Chipukizi  6 Septemba 2008

Ikiwa unataka kwenda sambamba na habari mpya mpya kutoka Madagaska, inawezekana kabisa ukawa ni msomaji wa Madagascar Tribune. Na kama wewe ni mdau wa gazeti hilo, hivi karibuni yawezekana ulishakutana na habari iliyoandikwa na mwandishi wa habari Herimanda R kuhusu upasuaji wa maradhi ya nadra na mafanikio yake ambao ulifanyika...