· Januari, 2013

Habari kuhusu Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kutoka Januari, 2013

Msumbiji: Uhamasishaji wa Kiraia Kuwasaidia Waathirika wa Mafuriko

  29 Januari 2013

Baada ya mvua kubwa iliyosababisha mafuriko kusini mwa Msumbiji yaliyowaacha maelfu ya raia bila makazi na wengi kupoteza maisha, kikundi cha kiraia cha Msumbiji Makobo kimeanza kampeni ya mshikamano inayoitwa “S.O.S. Chókwè” kukusanya misaada ya hisani kwa ajili ya waathirika.

Jukwaa la Kiafrika Lenye Makala za Bure za Kitaaluma

  22 Januari 2013

Januari 24, ni siku ambayo inategemewa kuwa ya kuzindua rasmi Hadithi, ambalo ni jukwaa la kuhifadhia zana za bure za kitaaluma mjini Nairobi, Kenya. Wasomi mbalimbali na wadau wa mitandao watakusanyika pamoja kujadili upatikanaji wa zana huru za kitaaluma katika elimu ya juu nchini Kenya. Hadithi itasaidia kutafuta, kuona na kushusha...

Mashoga Washambuliwa Kaskazini mwa Kameruni

  11 Januari 2013

Oscarine Mbozo’a anaripoti [fr] katika blogu ya L'Actu kuwa shoga mmoja akiwa ameambatana na mwenzi wake walizomewa karibu na soko mnamo tarehe 6, Januari 2013, mjini Maroua, Kaskazini mwa Kameruni: Goche Lamine, mfanyabiashara wa madawa, alikamatwa na mwanafunzi wa shule ya sekondari aitwaye Sanda, mwenye umri wa miaka 17. Umati wa...

Rais wa Chadi Awateua Wanawe Kushika Nafasi Nyeti

  11 Januari 2013

Djamil Ahmat anaripoti kuwa rais Déby wa Chadi amemteua mwanae wa kiume Mahamat Idriss Déby, 24, kuwa brigedia jenerali  [fr] pamoja na maafisa wengine wanne. Tchadanthopus anaongeza kuwa mwanae mwingine Zackaria Idriss Deby alisemekana kukabidhiwa umakamu wa rais [fr]  nafasi ambayo inampa madaraka yote wakati baba yake anapokuwa nje ya...

Watu 60 Wauawa kwa Msongamano nchini Abidjan

  2 Januari 2013

Magogo ya miti yaliyokuwa yameanguka barabarani yanaonekana kusababisha msongamano mkubwa na ulioua watu 60 na kujeruhi wengine 49 wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya mjini Abidjan, Côte d'Ivoire. Kutokana na ukweli kuwa eneo hilo halikuwa na mwanga wa kutosha inawezekana ndio sababu iliyochangia tukio hilo la msongamano ulisababisha mkanyagano...