Senegal Yatoa Ardhi ya Bure kwa Walionusurika na Tetemeko la Ardhi

Rais Wade, akiwa katika Mkutano wa Dunia wa uchumi 2002, anataka kuwapatia ardhi ya bure walionusurika na tetemeko la ardhi (picha na: Wikipedia)

Rais Wade, akiwa katika Mkutano wa Dunia wa uchumi 2002, anataka kuwapatia ardhi ya bure walionusurika na tetemeko la ardhi (picha na: Wikipedia)


Baada ya tetemeko la ardhi, wanasiasa na raia duniani kote wanagombania kujiunga na harakati za mshikamano zinazomiminika kwa ajili ya Haiti, na nchi maskini, zikijumuishwa nyingi zilizoko barani Afrika, hazijapitwa. Rwanda, Liberia, Afrika Kusini, Gabon, Naijeria na nyingine nyingi zimekwishatoa ahadi za misaada ya fedha. Hata hivyo, ni rais wa Senegal mwenye umri wa miaka 84, Abdoulaye Wade, ambaye anatawala vichwa vya habari. Kwa mujibu wa msemaji, Wade ametoa ardhi ya bure kwa Mu-Haiti yeyote aliyenusurika na tetemeko na ambaye “atapenda kurejea kwenye asili yake.” Kwenye wavuti, tangazo hilo limepokelewa na watu wengi kwa kejeli.

Japokuwa blogu ya Blog Politique au Senegal haijatoa maoni yake kuhusu pendekezo la rais Wade wala kuhusu tetemeko la ardhi, blogu hiyo ilituma maoni ya Dkt. El hadji Malick Ndiaye [Fr] juu ya umuhimu wa mshikamano baina ya nchi za kusini, ambayo yalichapishwa kabla ya Wade kutoa tangazo lake:

Il arrive des moments dans l’histoire d’un pays où les citoyens ont l’occasion de donner une leçon d’éthique à leurs élites. Il arrive des moments qui sonnent comme des opportunités pour un peuple de montrer sa grandeur morale. Nous ne pouvons pas nous complaire dans le fatalisme et la position de l’eternel assisté. A nous seuls, le Sénégal, nous ne mettrons pas fin aux souffrances du peuple haïtien. Cela ne nous dispense pas d’agir, cela n’excuse pas notre indifférence en acte. En ce moment même en Haïti des gens sont en train de crever et c’est cela réalité profonde de ce tremblement de terre. Tous les discours de solidarité sont bien dérisoires à cet instant, si on ne fait pas notre possible pour nous rendre utiles. Donnons un peu au reste du monde, car nous avons déjà beaucoup reçu du monde et nous en aurons peut-être besoin un jour. Les citoyens des grandes puissances qui se tournent aujourd’hui vers Haïti, au-delà de la simple valeur éthique de leurs actions, nous donnent une leçon de plus sur le sens de l’intérêt collectif. C’est moralement indigne de prétendre être un peuple magnifique, avec des valeurs magnifiques, un peuple prompt à fustiger les tares de l’Occident, à brandir les valeurs de solidarité religieuse, et de ne jamais lever le moindre petit doigt pour diminuer arithmétiquement la souffrance du monde.

Kuna nyakati katika historia ya nchi ambapo wananchi wake hupata fursa ya kuwafundisha watu wenye uwezo na nafasi somo la maadili. Kuna nyakati ambazo hujitoa kama fursa kwa watu kuonyesha uwezo wao katika maadili. Hatuwezi kutitia kwenye hali ya kukubali hatima yetu na daima kuwa katika hali ya kupokea [misaada]. Senegal pekee haiwezi kusitisha mateso ya watu wa Haiti. Lakini ukweli huo hauwezi kututoa katika kitanzi cha kutenda, ukweli huo hauwezi kuwa kisingizio cha kutojali kwetu. Katika dakika hii, nchini Haiti kuna watu wanakufa na huo ndio ukweli wa tetemeko la ardhi. Kauli zetu zote kuhusu mshikamano hazitakuwa na maana wakati huu ikiwa hatutafanya kila linalowezekana ili tuwe na msaada. Hebu tutoe kidogo kwa ajili yaw engine duniani, kwani tumekwishapokea sana kutoka kwa wengine duniani na tunaweza kuwa na shida siku moja. Raia wa nchi zenye nguvu, ambao wanaigeukia Haiti, zaidi ya thamani ya vitendo kama hivyo vya kimaadili, pia wanatupatia somo juu ya maana ya utu. Ni jambo la aibu na kuudhi kujifanya kuwa sisi ni watu tunaovutia, wenye maadili yenye kuvutia, watu ambao tu wepesi kukosoa mapungufu ya Wamagharibi, kuonyesha thamani ya mshikamano wa kidini, na kushindwa kunyanyua kidole ili kupunguza, kwa hesabu, mateso ya dunia

.

Hata hivyo, pendekezo la kuwahamisha Wahaiti wasiokuwa na ardhi haukuwa mshikamano ambao wengi waliufikiria.

Serigne Diagne, ambaye amekuwa akifuatilia kwa karibu jinsi Senegal ilivyoitikia tetemeko la ardhi, alikuwa na haya ya kusema kuhusu mpango huo:

… Dakar, ambayo inashindwa kushika kasi na kutatua matatizo yake mengi yanayohusiana na majitaka na mipango miji, ambayo vitongoji vyake vinaelea katika maji ya mafuriko yaliyotokea miaka mingi iliyopita, kwa uwezo gani itaweza kuwachukua watu au nchi nzima kutoka ng’ambo nyingine ya dunia?… [Bila ya kusema wapi itapata fedha za kufanya jambo hilo] Abdoulaye Wade, katika kuonyesha mshikamano na Uafrika (PanAfricanism), anatoa pendekezo la kupunguza watu Haiti, na kusahau kuwa wema huanzia nyumbani…

…[ni lazima ichukuliwe kuwa] Abdoulaye Wade, mwenye kupenda sana kumbukumbu za karne ya 19, anaamini kuwa Marcus Garvey bado yu hai, na kwamba harakati za “Kurudi Afrika” bado zina maana. Siku moja hatimaye atatuambia kuwa walikuwa ni Wabaguzoi wa Ku Klux Klan ambao waliitetemesha dunia kule Haiti. .. kila nchi ina majanga yake. Haiti ina majanga yake, ambayo yanasababisha moyo wa huruma, na sisi tuna majanga yetu, ambayo hufanya uharibifu sawa tu na ule wa tetemeko, matamko kama haya ya rais ambaye anashindwa kuwa mbali na mitafaruku, na ambaye rekodi yake ni chanzo zha utata. Watu wa Haiti, kama ilivyoelezwa na rais ‘ Wana haki katika ardhi ya Afrika”. Swali linabaki, ikiwa wataitaka (ardhi hiyo).

PascaleBoulerie, msomaji katika tak2.00221.info anaandika:

C'est une idée bien stupide, parce que le Sénégal souffre aussi de manque de terres cultivables, de surpopulation * et d'émigration.

Hili ni wazo la kijinga kabisa, kwa kuwa Senegal pia ina upungufu wa ardhi ianyoweza kulimwa, wingi wa watu, na kuhamahama kwa makundi makubwa ya watu.

Phillipe Souaille, akitokea kwenye makala ya Tribune de Geneve, anaandika:

Cher Gorgui, j'ai le sentiment que ton président a perdu une occasion (de plus) de se taire. Je ne crois pas que les Haïtiens crèvent d'envie de se réfugier en Afrique. La solution est forcément de trouver le moyen et les moyens de les aider à prospérer chez eux. Au moins pour parvenir au même niveau de vie que celui des îles voisines, tout de même supérieur à ce qu'il est en moyenne en Afrique, Sénégal inclus.

Une telle réflexion est même carrément effarante en ce qu'elle révèle des capacités d'analyse, de proposition et de réalisation pour le moins émoussées du bonhomme. La sénilité n'est-elle pas en train de faire son oeuvre? Il est temps qu'il laisse place à la relève, s'il n'a plus d'autres solution à proposer à un peuple qui souffre que l'abandon et l'exil !

Mpendwa Gorgui, ninahisi kuwa rais wenu (kwa mara nyingine tena) amepoteza nafasi ya kukaa kimya. Sidhani kwamba Wahaiti wanataka sana kupata ukimbizi Afrika. Suluhisho ni kutafuta njia ya kuwafanya waneemeke nchini kwao. Ili kwamba wafikie viwango vya maisha vinavyofanana na vile vya visiwa jirani, ambavyo kwa viwango vyovyote, viko juu zaidi ya Afrika, ikijumuishwa Senegal…

…je hii si kazi ya mgonjwa wa kusahau? Muda umefika wa kumpisha mtu mwingine, kama hana suluhisho lolote la kuwapa watu wanaoteseka kutokana na kuachwa pamoja na ukimbizi!

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.