Habari kuhusu Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kutoka Oktoba, 2009
Misri: Watawala Wa Kiimla na Wake Zao
Baada ya kuziangalia picha za mke wa Rais wa Cameroon, Mmisri Zeinobia anasema: “Sijui ni ni kiasi gani cha pesa alichotumia kwa ajili ya nywele zake na muonekano wake lakini...
Uganda: Wanablogu wa Uganda Wajadili Muswada Unaopinga Ushoga
Muswada ambao utaufanya ushoga kuwa kingyume cha sheria nchini Uganda umewasilishwa bungeni na sasa unasubiri tu saini ya rais Yoweri Museveni. Wanablogu mashoga nchini uganda wanajadili.
Ghana: Siku ya Kublogu mwaka 2009
Kwenye siku ya Kublogu Kwa Vitendo Duniani, Waghana waliwahoji viongozi wa dunia, walichachafya karatasi za Benki ya Dunia, walitambulisha tovuti mpya na walijiuliza ni kwa nini kulikuwa na majadiliano machache sana yanayohusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa nchini – na pia walitambua kwamba kuna mambo fulani nchi kama Ghana zinayafanya vyema.
Namibia: Kampeni ya Kukomesha Chanjo za Lazima
Kampeni ya kukomesha Chanjo kwa kulazimishwa nchini Namibia imezinduliwa: “ umoja wa Asasi za kijamii umetoa wito kwa Wanamibia wote kujiunga na kampeni ya kulaani chanjo kwa wanawake waishio na...
Somalia: Je Serikali Inawaandikisha Vijana Wa Kikenya Kwa Ajili Ya Vita?
Huu ni muhtasari wa kwanza wa blogu za Kisomali mwaka 2009. Naam, ni zaidi ya mwaka mmoja tangu nilipochukua likizo ya muda mrefu kutoka kwenye shughuli za kublogu lakini sasa nimerudi, moja kwa moja. Hii ni makala ya kwanza na tarajieni makala zaidi zinazohusu ulimwengu wa blogu za Kisomali.
Big Brother Africa msimu wa IV: Mageuzi yameanza
Big Brother Africa 4: Mapinduzi ni mfululizo wa nne wa vipindi vya kituo cha televisheni vinavyoonyesha maisha halisi vya Big Brother Africa, vilivyoanza Septemba 6, 2009. Kipindi hicho kimeshaanza kuzua mijadala na maoni kwenye mtandao wa intaneti kutoka kwa wanablogu na wasomaji wao.
Gabon: Upinzani waendelea kupinga matokeo ya Uchaguzi
Wapinzani wa kisiasa wa Gabon wanaonyesha muungano wa vyama vya siasa kupinga matokeo ya uchaguzi wa mwezi Agosti, ambayo yalimkabidhi urais mwana wa mtawala wa kiimla aliyepita, Omar Bongo. Wanasiasa na raia wanaikemea Ufaransa kwa kuingilia siasa za nchi hiyo.
Australia: Wanawake wa Kenya wakataliwa haki ya ukimbizi
Wanawake wawili wanakabiliwa na uwezekano wa kutimuliwa kutoka Australia baada ya maombi yao ya kuomba hifadhi kukataliwa, pamoja na hatari wanayoweza kuipata ya kulazimishwa tohara ya kike ikiwa watarudishwa nyumbani.