· Aprili, 2009

Habari kuhusu Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kutoka Aprili, 2009

Rwanda: Miaka kumi na tano baada ya mauaji ya Kimbari

  30 Aprili 2009

Hivi karibuni zilifanyika sherehe za kitaifa nchini Rwanda kuadhimisha kumbukumbu ya kutimiza miaka 15 tangu mauaji ya Kimbari. Mauaji hayo yaliangamiza maisha ya watu wapatao 800,000. Mnamo tarehe 7 Aprili, maadhimisho yalifanyika katika mji mkuu wa Kigali, na pia katika mji wa Nyanza, ambapo watu wapatao 5000 waliuawa kinyama. Katika Uwanja wa Mpira wa Kigali, maelfu ya mishumaa iliwashwa na kupangiliwa katika namna ambayo iliunda neno "Matumaini" katika lugha tatu.