· Januari, 2009

Habari kuhusu Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kutoka Januari, 2009

Blogu za Afrika Zapendekezwa Kupokea Tuzo ya Bloggies 2009

Blogu zilizopendekezwa kwa ajili ya Tuzo ya Tisa ya Zawadi za Weblog: Mapendekezo ya blogu katika mashindano ya Bloggies ya 2009 yalifunguliwa tarehe 1 Januari na kufungwa tarehe 19 Januari. Kwa mujibu wa waandalizi, mashindano hayo ya Bloggies ni mashindano ambayo yamedumu kwa muda mrefu zaidi mtandaoni, na mapendekezo pamoja na uchaguaji wa washindani katika fainali, ni juu ya msomaji wa blogu. Mshindi hupata senti 2,009 za Marekani! Je, ni mabloga gani wa Kiafrika waliopendekezwa kwa ajili ya kinyang'anyiro cha blogu bora zaidi?

26 Januari 2009

Angola: Ebola Inapokaribia, Mipaka yafungwa

Baada ya kuzuka kwa ugonjwa wa ebola kwenye Jamburi ya Kidemokrasi ya Kongo, maambukizi ya ugonjwa huo bado hayajafika nchini Angola. Ili kuuzuia kusambaa kwa virusi hatari vya ugonjwa huo, nchi hiyo jirani imefunga mpaka wake na Jamhuri ya Kidemorasi ya Kongo, kadhalika imezuia uhamiaji wa watu kati ya nchi hizo mbili. Anaandika Clara Onofre.

18 Januari 2009

Kivu Mpaka Gaza: Namna Vyombo Vya Habari Vinavyochagua Vipaumbele

Mdahalo unaodadisi ni kwa nini vita katika Mashariki ya Kongo vinapewa kipaumbele kidogo ikilinganishwa na migogoro inayotokea Mashariki ya kati. Mwandishi wa habari wa Rue89 anauliza, "ikiwa kifo cha Muisraeli mmoja ni sawa na vifo kadhaa vya Wapalestina, ni maiti ngapi za watu wa Kongo zitakazowekwa kwenye mnara wa mazishi huko Gaza?" Wanablogu wa pande zote mbili wanalichambua swala hilo.

11 Januari 2009