Lebanoni: Watu 90 Wanahofiwa Kufariki Baada ya Ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia Kuanguka Baharini

Rambirambi zilimiminika kwenye Twita baada ya ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia kuanguka kwenye (bahari ya) Mediterani dakika chache baaday ya kupaa ikitokea Beirut, Lebanoni. Watu wote 90 waliokuwemo wanahofiwa kuwa wamekufa baada ya ndege hiyo kushika moto katika kimbunga cha radi na kuangukia baharini.

@tsepeaces anatuma tena ujumbe wa twita wa mtu aliyeshuhudia tukio na kusema:

RT @patrickgaley: Shahidi Naame “Tuliona mlipuko kama jua angani, ulikuwa pale kwa sekunde chache halafu ukatokomea kwenye giza” #ET409

Pia anaandika ujumbe huu wa twita:

Ndege ile ilikuwa kama mpira wa moto kwa sekunde chache – hayo ni maneno yanayojirudia :-/ #ET409 Na Wapumzike Kwa Amani!

Mwanahabari wa gazeti la Daily Star na mwanablogu wa Huffington Post Patrick Galey anamnukuu mwanaume mmoja wa Lebanoni ambaye amepoteza marafiki 10 waliokuwemo kwenye ndege hiyo:

Fouad Shihab, marafiki 10 kwenye ndege: Nilitakiwa niwepo kwenye ndege ile na angalia kilichotokea. Marafiki zangu wote wamekufa.”

Katika ujumbe wa awali wa twita, anaandika:

Ndiyo kwanza nimerudi kutoka uwanja wa ndege wa Rafiq Hariri, yanayoonekana huko yanatisha. Hakuna taarifa, nimeongea na watu waliopoteza familia nzima

Hichame Assi (@hiconomics) anaandika:

Ni masikitiko makubwa kusikia kuhusu #ET409… Natumaini (msiba) utakuwa bila ya uchungu kwa kadri inavyowezekana kwa ndugu na marafiki wote. Allah Yer7am (Mungu uwahurumie)

Georges Azzi, ambaye amekuwa akifuatilia habari hii kwenye televisheni, hakuvutiwa na akaandika:

Lebanoni: idhaa nyingi za televisheni = muda mrefu hewani #habari za #et409 zinaelekea kwenye udaku na hadithi za kubuni #fail

Samer, anayetwiti kama @meetsameer, pia alieleza kuchukizwa kwake na vyombo vya habari na kusema:

Vyombo vya habari vya Lebanoni havina ustaarabu au aina yoyote ya maadili, tayari vinawaita watu ambao hawajapatikana kama “waliokufa” #ET409 #Lebanon

Amer Tabsh (@arzleb) anaelezea hisia kama hizo na anaandika:

Uchambuzi wa LBC (Shirika la Habari la Lebanoni) wa #ET409 ni wa kipumbavu na potofu #fail

Pia anatoa namba ya simu ya maelezo na maswali juu ya ajali:

Namba ya dharura 71207326 kwa ajili ya taarifa & maswali kwa familia za waliodhurika/namba ya dharura 1701 ili kutoa habari za mabaki na miili inayoonekana #ET409 #Lebanon

Wakati huo huo, Tala amestushwa na habari hii na kutwiti:

Miili 25 imechukuliwa kutoka majini, 2 kati yake ilikuwa ni ya watoto. Na bado hawajaweza kuitambua. Pumzikeni kwa Amani #ET409


Cal Perry
wa CNN pia alikuwa anandika jumbe za twita na katika ujumbe mmoja anasema:

Siku ya masikitiko #et409 – kesho tutajaribu kwenda pwani. Hii ndio habari ya usiku wa leo kutokea uwanja wa ndege. Waziri Mkuu Hariri anajaribu kwa nguvu zote kufariji

Nathan Redd yumo katika uchungu na anaandika:

Siwezi kabisa kuwa makini katika kitu chochote leo. #ET409 ndio jambo pekee kwenye akili yangu leo. Moyo wangu umevunjika.

Na @nightS anatoa muhtasari wa siku kwa kusema:

Ni siku mbaya na ya masikitiko :( #ET409

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.