· Februari, 2011

Habari kuhusu Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kutoka Februari, 2011

Gabon: Wanafunzi Waandamana, Wanajeshi Wasambazwa

  13 Februari 2011

Mgogoro wa kisiasa nchini Gabon ulifikia vilele vipya siku ya Alhamisi, wakati wanafunzi walipoandamana katika Chuo Kikuuu cha Omar Bongo kilichopo ndani ya mji mkuu wa nchi hiyo, Libreville. Wakati maandamano ya juma lililopita yalishirikisha zaidi wanachama wa vyama vya upinzani, mgogoro huu unaonekana kupelekea kuwa mgogoro mkubwa zaidi wa kijamii.