Habari kuhusu Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kutoka Juni, 2013
Rais Obama Kuitembelea Tanzania
Rais wa kwanza wa Marekani mwenye asili ya Afrika, Barack Obama anatarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam kesho alasiri kwa ziara ya kiserikali. Blogu ya Swahili Time imeweka ratiba ya...
Simu za Bure Kwa Wakulima wa Nigeria?
Wizara ya KIlimo nchini Naijeria imetangaza mpango wake wa kugawa simu za bure za kiganjani kwa wakulima wa vijijini. Mpango huu umezua mjadala mzito kwenye ulimwengu wa blogu nchini Naijeria.
China Yadaiwa Kuchimba Dhahabu Kinyume cha Sheria Nchini Ghana
Shirika la Habari la Xinhua limeripoti kwamba raia 124 wa Kichina waliodaiwa kushiriki katika uchimbaji wa madini haramu ya dhahabu walikamatwa na kuwekwa kizuizini nchini Ghana. Serikali ya China imetakiwa kulinda na kuwatetea raia...
Je, Italia Iko Tayari kwa Waziri Aliyezaliwa Afrika?
“Je, Italia iko tayari kwa Waziri wa Serikalki aliyezaliwa Afrika?,” Donata Columbro anauliza: Miezi miwili baada ya uchaguzi wa hivi karibuni, Italia ina serikali mpya. Na Cécile Kyenge, mwenye umri wa miaka...
Matatizo Makuu ya Raia wa Benin ni Yapi?
Tite Yokossi anafunua matokeo ya kura ya maoni iliyoendeshwa na Mfuko wa Zinsou ambao uliwauliza wananchi wa Benin ni yapi ndiyo matatizo yao makuu leo [fr]. Tatizo la kwanza lililoorodheshwa lilikuwa uwezo mdogo wa...
Gwaride la Kwanza la Mashoga Nchini Lesotho
Leila Hall anablogu kuhusu gwaride la kwanza la mashoga kuwahi fanyika nchini Lesotho: Tukio hilo limeandaliwa na Kikundi cha Kutoa msaada cha MATRIX- Shirika lisilo la kiserikali la Lesotho- linatetea haki za watu...
Uganda: Hatimaye Magazeti Yaliyofungiwa na Polisi Yafunguliwa
Uganda imeruhusu magazeti mawili kufunguliwa tena baada ya msuguano uliodumu kwa siku 11 kati ya serikali na vyombo vya habari juu ya barua yenye waliyoipata ambayo iliyoonyesha njama ya kumtayarisha mtoto wa kwanza wa Rais Yoweri Museveni kumrithi kiongozi huyo aliyedumu kwa miaka 27.
Wafanyakazi wa Sekta ya Afya Nchini Msumbiji Wagoma Kudai Maslahi
Wafanyakazi wa sekta ya afya nchini Msumbiji wamekuwa katika mgomo uliodumu kwa siku kumi na kusababisha kusimama kwa huduma katika vitengo vingi vya kutoa huduma za afya kote nchini humo. Mgogoro wao na serikali umetokana na madai yao ya kuboreshewa maslahi na mazingira ya kazi pamoja na kurekebishwa kwa gharama za chumba cha wagonjwa mahututi katika mahospitali yote nchini humo.