Shirika la Habari la Xinhua limeripoti kwamba raia 124 wa Kichina waliodaiwa kushiriki katika uchimbaji wa madini haramu ya dhahabu walikamatwa na kuwekwa kizuizini nchini Ghana. Serikali ya China imetakiwa kulinda na kuwatetea raia wake. Kwa upande mwingine, maoni yaliyotokana na tukio hilo yaliukosoa unyanyasaji unaofanywa dhidi ya watu wa Afrika katika biashara ya madini ya dhahabu inayosimamiwa na China nchini Ghana. Mtandao wa China offbeat unayo maelezo ya kina.