Habari kutoka 9 Juni 2013
‘Sauti za Iran’ Mradi Unaowapa Sauti Raia Waishio Vijijini
Sauti za Iran ni mradi ulioundwa kwa kutumia mafanikio ya mradi wa Ushahidi. Sauti za Iran inakusudia kuripoti habari kuhusu miji midogo na vijiji vya Iran na vile vile kukusanya maombi na matatizo ya wananchi na kuyatuma kwa serikali na wabunge.
China Yadaiwa Kuchimba Dhahabu Kinyume cha Sheria Nchini Ghana
Shirika la Habari la Xinhua limeripoti kwamba raia 124 wa Kichina waliodaiwa kushiriki katika uchimbaji wa madini haramu ya dhahabu walikamatwa na kuwekwa kizuizini nchini Ghana. Serikali ya China imetakiwa kulinda na kuwatetea raia wake. Kwa upande mwingine, maoni yaliyotokana na tukio hilo yaliukosoa unyanyasaji unaofanywa dhidi ya watu wa Afrika katika biashara ya...
Je, Italia Iko Tayari kwa Waziri Aliyezaliwa Afrika?
“Je, Italia iko tayari kwa Waziri wa Serikalki aliyezaliwa Afrika?,” Donata Columbro anauliza: Miezi miwili baada ya uchaguzi wa hivi karibuni, Italia ina serikali mpya. Na Cécile Kyenge, mwenye umri wa miaka 48, daktari wa upasuaji macho na raia wa Italia aliyezaliwa Kongo, ni Waziri mpya wa Ushirikiano katika baraza la mawaziri la Waziri...