Habari Kuu kutoka Agosti 2009
Habari kutoka Agosti, 2009
Pakistani: Tatizo La Sukari Limeifanya Ramadhani Kuwa Chungu
Upungufu wa sukari pamoja na kupanda kwa bei nchini Pakistani mwaka huu kumewaathiri walaji na kumesitisha ongezeko la matumizi wakati wa mwezi wa ramadhani. Wanablogu wa kipakistani wanaichambua hali hiyo.
China: Mitizamo Potofu Pamoja na Ubaguzi wa Wa-Han Dhidi ya Wa-Uyghur
Ni mwezi mmoja na zaidi umepita tangu machafuko ya Xinjiang ya Julai 5 na wengi wa wanamtandao wa intaneti wa Kichina bado wanazilaumu nchi za Magharibi pamoja na Rebiya Kadeer kwa kuwatetea wale wanaotaka kujitenga huko Xinjiang. Hata hivyo, kuna sauti za minong’ono zinazochepuka hapa na pale katika intaneti ya...
Iangazeni Naijeria: Imetosha Sasa Basi
Pamoja na kuwa nchi yenye utajiri wa mafuta, hali ya ugavi wa umeme nchini Naijeria hairidhishi. “Katika sehemu nyingi za nchi, giza linatawala na majenereta yamechukua nafasi kama vyanzo vya nishati ya umeme” Inasema blogu ya Adebayo. Sasa Wanaijeria wameanzisha kampeni kubwa ya mtandao wa intaneti inayopinga hali hii inayogharikisha kwa kutumia tovuti za kijamii, hasa kwenye Twita kwa kutumia anwani ya #lightupnigeria (#iangazenaijeria).