Rafa Saavedra, muandishi na mtaalamu wa utamaduni wa chini chini kutoka mji wa mpakani wa Tijuana, nchini Maxico, amegeuza kila moja ya zana zake ya uanahabari wa umeme. Kwa upande upande mmoja, anachapisha hadithi fupi fupi na miradi katika blogu yake Crossfader Network [es] (pamoja na vibadiliko vyake); na kwa upande mwingine, ni mtumiaji wa twita anayeshindwa kujizuia @rafadro, ameichukulia twita kama chanzo cha ubunifu. Mradi wake wa kiuandishi, “soweird”, unachanganya utunzi mfupi-mfupi, siri na jumbe za twita.
“Mtandao wa Crossfader ndio nyumbani kwangu, sehemu ambayo ninakusanya mawazo yangu, na kufikiria dunia njema zaidi na kuyagawa yale ninayoyafanya”, anaeleza Rafa kwenye mahojiano ya barua pepe, “Twit ani nyumba yangu ya ukapera: sherehe isiyo na mwisho na marafiki pamoja na wafuasi, chanzo cha (karibu) habari zote za mwanzo, maabara ya ubunifu iliyojaa makorokoro, kejeli pamoja na dhati kwa alama 140”.
Mwezi Julai mwaka huu aliwataka wafuasi zaidi ya 200 wa twita kuchangia siri zao kubwa (au hata siri ndogo, kama alivyokiri muda mchache baadaye) ili kutengeneza utunzi unaosimuliwa na sauti mbalimbali. Baada ya kupokea siri 40 kwa kupitia Twita alikuja na kazi ya “Soweird”, ambamo utunzi na ukweli ulieleza matukio 22 ya ngono, aibu na jinai. Hadithi iliyotokana (na maradi huu) inapatikana kupitia blogu yake katika lugha za Kihispania na Kiingereza, imepangwa kuchapishwa katika jarida la kiuandishi huko Mexico El Perro [es].
Katika sehemu moja ya “Soweird” inayotilia maanani masuala ya familia, tumekutana na siri hii:
11. Mauritz alimuhujumu mpenzi wake wa kike na kutembea na mpenzi wa kike wa rafiki yake mkuu. Baada ya msichana huyo kutengana na rafiki yake mkuu, aliolewa na kaka yake Mauritz. Na hivi sasa (Mauritz) anashindwa kumfafanulia mpezni wake wa kike ni kwa nini hawawezi kuhudhuria shughuli za kifamilia bila ya kujawa na hofu ya kuzua zahama ya kiwango cha kibiblia.
Katika sehemu ya jinai, tunakutana na siri hii nyingine:
17. Elwin alianza kutumia hundi ambazo baba yake alimtumia ili kulipia gharama za masomo kwenye chuo kikuu binafsi ambacho alikuwa ahudhurii kununulia vitabu vya vikatuni. Kisha, alichukua na kutumia kiasi kikubwa cha fedha kazini kwake; na kudai kuwa aliporwa. Kuna wakati alihitaji kufanya shughuli ya haraka katika ofisi ya manispaa na aliiomba kampuni yake kiwango kikubwa zaidi ili kumuhonga afisa aliyekuwa zamu (na kutumia nusu ya kiwango kile kwenye pombe).
Mtazamo wa Saadvera kuhusu huduma hii ya kuandika blogu fupi-fupi unafika mbali zaidi ya kuandika vitu visivyo na maana: Katika twita mara nyingi watu hukiri vitu vya ajabu, visivyoaminika na vya aibu. Kuna hata anwani ya kukiri #yoconfieso (ninakiri). Kwa hivyo badala ya kunakili siri kutoka kwenye mafaili, niliamua kwamba ingekuwa ni jambo la kuvutia kufanya na siri za mtu mwingine. Nilitaka kuona ni kwa kiwango gani wanaweza kuthubutu, na ni kwa kiwango gani wanatofautiana na sura ambayo wanawaonyesha wafuasi wao kwenye twita. Kuchungulia kwa mwandishi 2.0.”
Japokuwa hawezi kufichua majina halisi ya wafuasi wake, Saadvera aliwaweka katika makundi watumiaji waliojiunga naye katika mradi: “Kuna watu wachache wan chi za nje, kundi la umri wao ni kati ya miaka 19-40. kama inavyosomeka kwenye maandishi, kuna sehemu nane ambazo zinazigawa siri (Ngono, Aibu, Wapenzi wa zamani, Familia, Jinai, starehe, vishawishi na marafiki wa zamani). Siri za watumiaji wa twita zinahusiana zaidi na familia, ngono, aibu na vishawishi. Kuna siri chache za kustusha.”
“Soweird” siyo mradi wa kwanza unaunganisha twita na fasihi ambao Saadvera ameufanya. Mwaka 2007, alikuwa kiongozi wa mradi wa ushirikiano Microtxt, ambao ulikusanya hadithi fupi-fupi 238 kwa kutumia jina la @microtxt, ambao ulichapiswa (kama fasihi teule) kwenye majarida ya Ki-Mexico Replicante [es] na Balbuceo. ”Niliwaalika marafiki ambao ni waandishi, wanahabari, wanafunzi wa mawasiliano na watu ambao nilifikiri wangevutiwa katika utengenezaji wa maandiko mafupi-mafupi na ule uandishi wa watu wanaoficha majina yao. Kanuni ya msingi katika warsha hii ilikuwa ‘uandishi ni ushirika.’ Mwanzoni hawakuelewa matumizi ya twita aidha utaratibu wa uandishi na namna ya kuandika bila kutaja jina. Baadaye tulifikia washiriki 100”, alisema katika mahojiano.
“Hivi sasa siwezi kuyaelewa maisha yangu bila intaneti, bila ya mitandao ya kijamii, bila ya kila kitu kinachotokana na hayo mawili”, alieleza, “lakini katika wakati huo huo, ninaweza kuizima tarakilishi yang una kuishi maisha yangu bila hofu yoyote. Maisha ya kwenye mtandao wa intaneti, uanahabari wa umeme na matumizi pia ni mipaka ambayo tunaweza kuivuka kukiwa au pasipokuwa na vizuizi. Kitu kama hicho hutokea katika maisha yangu hapa Tijuana”.
Saadvera alieleza ‘ukweli” anaomuhusu yeye kwa herufi 140 (au pungufu):
“Sijawahi kutaka kuwa mtu ambaye si mimi; hata hivyo, huwa ninabadilika kila wakati kiasi kwamba wakati mwingine huwa nashindwa kujitambua: naam, ninajipinga”.