Habari Kuu kutoka Aprili 2011
Habari kutoka Aprili, 2011
Misri: Basboussa kwa Urais!
Mtangazaji habari wa zamani wa televisheni ya Misri na mwanaharakati Bothaina Kamel alitangaza kwenye twita kwamba ana mipango ya kugombea urais. Yafuatayo ni maoni ya kumuunga mkono na kupinga hiyo mipango yake .
Naijeria: Wafuatiliaji wa twita unaoweza kuwafuatilia wakati wa Uchaguzi wa Naijeria mwaka 2011
Ni wakati wa uchaguzi nchini Naijeria. Uchaguzi wa Wabunge umeahirishwa mpaka Jumatatu kutokana na hitilafu za kiuratibu. Uchaguzi wa Rais utafanyika tarehe 9 Aprili 2011. Hii ni orodha yetu ya kwanza ya watumiaji wa twita waliopendekezwa kama utapenda kufuatilia uchaguzi wa Naijeria 2011.
Naijeria: Wanablogu wa Ki-Naijeria wanasema nini kuhusu uchaguzi wa mwaka 2011?
Kadiri uchaguzi wa mwaka 2011 nchini Naijeria unavyozidi kukaribia, Wanablogu wa Naijeria wanatumia muda wao mwingi kuzungumza juu ya uchaguzi huo lakini je kuna mtu anayesikiliza?
Naijeria Yapiga Kura 2011: Maoni kutoka kwenye Uchaguzi
Wanaijeria walipiga kura jana katika uchaguzi wa tatu wa rais tangu taifa hilo lilipoingia kwenye utawala wa kiraia mwaka 1999. Mpaka sasa, uchaguzi huo umeelezwa na wengi kuwa ulikuwa wa mafanikio, huku kukiwa na taarifa za ghasia za hapa na pale pamoja na hitilafu za upigaji kura. Vyanzo vya habari vimeripoti kuwa watu wengi walijitokeza, foleni zenye kufuata utaratibu, na wapiga kura kusubiri hadi uchaguzi utakapomalizika ili kuhakikisha kwamba kura zao zimehesabiwa. Wanablogu wanajadili.
Côte d'Ivoire: Kuanguka kwa Laurent Gbagbo
Laurent Gbagbo alikamatwa katika makazi yake ya Cocody, pamoja na mkewe, Simone, na msafara wa watu wa karibu. Miezi mitano baada ya kukataa kukabidhi madaraka kwa rais anayetambuliwa kimataifa kama rais mpya wa Côte d'Ivoire, Alassane Ouattara, mgogoro nchini humo hivi sasa unaelekea kufikia hitimisho.Mtiririko wa matukio yaliyopelekea kukamatwa kwa Gbagbo yaliorodheshwa kwa kina kwa njia ya video za kwenye mtandao ambazo zilitolewa maoni kwenye mtandao.
Côte d'Ivoire: Gbagbo agoma, Waafrika waandamana
Wakati Rais wa zamani wa Côte d'Ivoire Rais Laurent Gbagbo akiwa bado amejichimbia ndani ya handaki nchini humo, akigoma kukamatwa kwa kuendelea kukataa kushindwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2010, ushiriki wa Ufaransa katika harakati za kumng’oa zinasababisha miitikio miongoni mwa wanasiasa na raia wa Ufaransa, pamoja na jamii ya Waafrika waishio Ufaransa.
Côte d'Ivoire: Abijani kwenye masaa ya kudhoofu kwa utawala wa Gbagbo
Siku mbili zilizopita zimekuwa na utajiri katika misuguano na mivutano nchini Côte d'Ivoire. Vikosi vinavyomtii Ouattara, vilianza mashambulizi kuelekea Kusini na Magharibi mwa nchi hiyo. Katika siku zisizozidi tatu, walifanikiwa kuikamata miji ya Douékoué na kufika Yamoussoukro tarehe 30 Machi. Wa-Ivory wanatoa maoni yao kuhusu wafungwa kutoroka, kufungwa kwa televisheni ya taifa na sehemu aliyo Gbagbo:
Naijeria: Je, Teknolojia itaathiri uchaguzi wa mwaka 2011?
Wanaijeria wanaingia kwenye uchaguzi tarehe 16 Aprili 2011 kumchagua rais wao mpya. Uchaguzi uliahirishwa kutoka siku iliyokuwa imepangwa awali ya Aprili 9 kwa sababu ya kasoro za kimuundo. Katika makala hii tunatazama namna Wanaijeria wanavyotumia teknolojia kuwezesha uwazi katika uchaguzi, ushirikishwaji wa kisiasa na utawala bora.
Ivory Coast: Je, nani anadhibiti televisheni ya taifa ya RTI?
Bado kuna mkanganyiko kuhusu swali la nani hivi sasa ndiye mwenye udhibiti wa Radio Télévision Ivoirienne (RTI) , ambacho ni kituo cha televisheni ya taifa.
Naijeria: Maonesho ya Picha za Kampeni ya Urais
George Esiri alifuatilia kampeni za kugombea urais za chama cha PDP huko Naijeria. Maonesho ya picha alizopiga yalizinduliwa jana katika Kituo cha Yar'Adua.