Habari kutoka Oktoba, 2015
Kampeni ya ‘Alaa Aachiwe’ Yashika Kasi Mwaka Mmoja Baada ya Kufungwa Kwake
Alaa Abd El Fattah ametumikia mwaka mmoja kwa sababu ya uanaharakati wake. Amebakisha miaka minne. Watumiaji wa mitandao wanapiga kelele wanapoadhimisha mwaka mmoja wa kifungo chake wakidai aachiliwe huru.
Filamu ya Difret Inayosimulia Mila ya ‘Kumteka’ Mwanamke Kulazimisha Ndoa Nchini Ethiopia
Neno "Difret" lina maana ya "ujasiri" katika lugha ya ki-Amariki. Ni filamu mpya yenye jina hilo ikisimulia mkasa wa msichana wa ki-Ethiopia aliyetekwa na wanaume waliotaka kulazimisha ndoa ya 'kimila'.
Wa-Tanzania Wamkumbuka Baba wa Taifa Lao kwa Alama ya #DearNyerere
"#DearNyerere, enzi zako, umaarufu ulitokana na matendo mazuri kwa nchi yako, lakini siku hizi ni idadi ya wafuasi kwneye mitandao ya Instagram na Twita."
Wanaharakati Waomba Ulinzi kwa Makabila Yanayopinga Uchimbaji Madini Nchini Ufilipino
"Wao ndio waasisi wa tamaduni zetu za kipekee za sanaa. Mauji dhidi yao ni mauji ya utu wa watu wetu."
Wasiwasi wa Usalama wa Mfungwa wa Syria, Aliyehamishwa Kwenda Kusikojulikana
Wanaharakati wanaitaka serikali ya Syria kumwachia huru mara moja mwanablogu mfungwa mwenye asili ya Syria na Palestina Bassel Khartabil (Safadi) baada ya kuhamishwa mapema leo kutoka kwenye gereza alilokuwepo kwenda kusikojulikana.
Raia wa Ufaransa Wastukia Hatari ya Muswada wa Udukuzi
Watetezi wa haki za kiraia wanasema muswada unaokaribia kuwa sheria unaweza kuipa nguvu Ufaransa katika udukuzi wa kimataifa wa mawasiliano ya intaneti.
‘Simulizi ya Kimapenzi ya Syria’ yafuatilia Safari ya Familia Ikiwa Vitani na Uhamishoni
“Nafikiri ujumbe wa matumaini upo kwenye ujasiri usio na kificho— ujasiri ulio dhahiri wa familia moja, ambao kila mwanafamilia ameupitia.”