‘Simulizi ya Kimapenzi ya Syria’ yafuatilia Safari ya Familia Ikiwa Vitani na Uhamishoni

A new film follows one Syrian family through five years of upheaval (Sean McAllister) Credit: (Sean McAllister).

Filamu mpya yaonesha mwenendo wa familia moja ya Syria kwa kipindi cha miaka mitano ya vurugu za kisiasa. Picha kwa hisani ya: Mtayarisha Filamu Sean McAllister.

Makala hii pamoja na ripoti ya rediao iliyoandaliwa na Leo Hornak wa The World, kwa mara ya kwanza iliwekwa PRI.org mnamo tarehe 24 Septemba, 2015, na inachapishwa tena hapa kwa makubaliano ya kushirikiana kwenye maudhui.

Kiwango cha janga la vita vya Syria ni vigumu kulielezea: zaidi ya watu 200,000 wamepoteza maisha, milioni 6 wakiwa wakimbizi wa ndani, na milioni 3 na zaidi wakiishi kama wakimbizi.

Kwa sasa, filamu mpya iliyojipatia tuzo inatazamia kuelezea madhara ya mtu mmoja mmoja ya raia wa kawaida yatokanayo na vita vya nchini Syria.

Tangu mwaka 2009, kabla ya kuanza kwa mgogoro wa hivi sasa, mtayarishaji wa filamu wa kiingereza, Sean McAllister alikuwa akichukua filamu ya maisha ya kila siku ya familia moja iliyo na maskani yake huko Damascus.

Amer Daoud pamoja na mke wake Raghda Hassan kwa mara ya kwanza walikutana na kuwa wapenzi wakiwa kama wafungwa wa kiasiasa kwenye seli za magereza ya Syria takribani miaka 15 iliyopita.

Kamera ya McAllister imekuwa ikiwafuatilia wao pamoja na familia yao kwa kila hatua ya mapinduzi ya Syria, vita vya wenyewe kwa wenyewe, pamoja na maisha ya uhamishoni ya familia hii huko ulaya. simulizi hii imepewa jina la “Simulizi ya Kimapenzi ya Syria.”

McAllister anasema kuwa alianza kuchukua filamu ya familia hii tangu mapinduzi yalipoanza. “Nilipigiwa simu na kuambiwa, ‘Unajua nini? Hali imechafuka tena nchini Syria!’ — na watu wakwanza kabisa kuingia mitaani walikuwa ni Amer pamoja na mtoto wake wa kiume, Kaka, na wote walikamatwa na kutiwa kizuizini.”

Hatimaye familia ipo huru, lakini Sean yeye alikamatwa na na kushikiliwa kwenye gereza moja nchini Syria kwa muda wa wiki moja. Kilichofuatia, serikali ilitambua mtu aliyekuwa akichukua filamu, na pia Amer, Raghda na walilazimika kwenda kuishi uhamishoni kwa ajili ya usalama wao.

Kadiri familia inavyozidi kuzoea nchi za kigeni pamoja na mazingira mapya, hali ya kukosa amani inajitokeza katika familia ya Amer na Raghda.

Pamoja na madhila yaonekanayo katika filamu hii, McAllister bado anaitazama filamu hii kama yenye kuleta matumainin makubwa: “Nafikiri ujumbe wa matumaini upo kwenye ujasiri usio na kificho— ujasiri ulio dhahiri wa familia moja, ambao kila mwanafamilia ameupitia.”

Anaamini kuwa filamu zinazotambua utu wa wahamiaji na wakimbizi ndizo zilizo za muhimu kabisa. “Tunaona kwenye televisheni watu wakiwa wamesombwa na maji na kuletwa pembezoni mwa ukingo wa bahari. Amer na Raghda wanawatetea watu wote hawa ambao kila siku tunawaona kwenye habari.”

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.