Machi, 2010

Habari kutoka Machi, 2010

Serikali ya Japani: Kuhusu Kuanguka kwa Mfumo wa Ajira

  31 Machi 2010

Chombo kinachotumika kufanya tafakari nzito cha Baraza la Mawaziri la Japani, Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (内閣府 経済社会総合研究所)(ESRI) kimechapisha matokeo ya utafiti yaliyopima hadhi ya sasa ya ajira ya maisha na ulipaji ujira kwa kutumia cheo cha mtu (yaani, mfumo wa ajira wa Kijapani). Walitumia data (1989 –...

Lebanoni: Wafanyakazi wa Ndani Wanaotoroka

“Mfanyakazi wa ndani anapotoroka kutoka kwenye nyumba ya mwajiri wake, kituo cha polisi hakiwezi kufanya lolote kwa sababu hakuna sheria dhidi ya wafanyakazi wa ndani wanaotoroka. Kwa hiyo ofisa wa kituo cha polisi anamwambia mwajiri wa ki-Lebanoni aseme kuwa (mtoro huyo) aliiba pesa,” anaandika Ethiopian Suicides.

Misri: Wafanyakazi wa IslamOnline Wagoma

Mamia ya wafanyakazi, wahariri, na waandishi wa habari walianza mgomo wa kuonyesha hasira yao katika mtandao unaosomwa sana wa jiji la Cairo unaojulikana kwa jina la Islamonline baada ya kuwa wafanyakazi wapatao 250 wamefukuzwa kazi. Kwa mara ya kwanza, wagomaji wanatumia kwa ufanisi na vizuri kabisa aina mpya ya chombo cha habari ili kuvuta usikivu na uungwaji mkono katika kile wanachokipigania, kuanzia na Twita inayoendelea mpaka mmiminiko wa habari wa hapo kwa hapo.

Afrika Kusini: Ubaguzi wa Julius Malema

Wakati tabia za Rais Jacob Zuma zimekuwa zikizua mijadala mikali na yenye uhai katika ulimwengu wa blogu wa Afrika Kusini, hivi sasa ni mwanasiasa mwenye utata ambaye pia ni rais wa Umoja wa Vijana wa ANC, Julius malema ambaye anatengeneza vichwa vya habari. Hivi karibuni, aliwaongoza wanafunzi katika kuimba wimbo wa zamani wa kupinga ubaguzi wa rangi unaoitwa Ua Kaburu.