Mwaka Mmoja Baada ya Mapinduzi, Viongozi wa Madagaska Wakabiliwa na Vikwazo

Katika maadhimisho ya mapinduzi ya serikali yaliyofanyika Machi 17, 2009 nchini Madagaska, vikwazo vinavyowalenga viongozi wa sasa wa Madagaska vinaandaliwa kwa kushindwa kwao kuheshima makubaliano ya Maputo ambayo hapo awali yalifikiwa na pande zote zinazohusika. Uamuzi huu unatolewa kufuatia onyo lililotolewa na Umoja wa Afrika pamoja na Kundi la Mawasiliano la Kimataifa (International Contact Group) lililotolewa mwezi mmoja uliopita na kufuatia kufutiliwa mbali mara kadhaa kwa makubaliano ya kimataifa ya kibiashara jambo ambalo tayari limeathiri viwanda vya nchini humo. Vikwazo hivyo pia vinakuja katika kipindi ambapo Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za Binadamu na Idara ya Serikali ya Marekani ambazo kwa pamoja huweka kumbukumbu ya matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu na biashara haramu inayoendelea ya usafirishaji kuvuka mipaka ya kimataifa ya mti adimu unaojulikana kama Rosewood kutoka misitu ya nchi hiyo ya Madagaska. Kwa mujibu wa taarifa za kutoka kwa mtu aliye ndani ya serikali ya Madagaska, vikwazo hivyo vinavyowalenga watu kadhaa vitasababisha kuzuiliwa kwa mali na fedha wa watu walio sasa katika orodha na hata kukamatwa kwao endapo watasafiri nje ya Madagaska (fr).

Serikali imeendelea na jeuri yake pamoja na kuwepo kwa vitisho hivyo vya vikwazo huku ikijenga hoja kwamba ni kwa kupitia uchaguzi wa kitaifa tu kwamba mgogoro huo utamalizwa kwa ufanisi. Wakati huohuo jinsi uchaguzi huo unavyoweza kuandaliwa na kusimamiwa ni suala ambalo halijaeleweka vema na tayari tarehe ya uchaguzi wa wabunge imekwishaahirishwa.

Mkwamo huo wa kisiasa unapata ugumu zaidi kutokana na kuwepo kwa mahitaji ya misaada ya kibinadamu kutokana na Kimbunga kilichobatizwa jina la Hubert kilichoua watu 14 na kuwaacha wengine 37,891 wakiwa bila makazi baada ya kuwa kimesababisha maporomoko ya udongo mapema wiki iliyopita.

Mafuriko yaliyosababishwa na Kimbunga cha Hubert upande wa Kusini Mashariki wa Madagaska

Mafuriko yaliyosababishwa na Kimbunga cha Hubert upande wa Kusini Mashariki wa Madagaska


(Picha na: Global Green Funds).

Akitafakari kuhusu vikwazo vinavyoandaliwa dhidi ya viongozi wa kitaifa wa Madagaska, Citoyenne Malgache, ambaye ni mwanablogu aliyeko Madagaska, anapatwa na hisia mchanganyiko kuhusu madhira mbalimbali yanayoweza kuwakabili raia wa kawaida wa Madagaska. Amejawa na hisia mbili, moja ikivutiwa na wazo hilo na ya pili ikitawaliwa na hofu (fr):

Contente ? Si l’Union Africaine ne se contente pas de sortir sa liste des sanctionnées, mais présente aussi au peuple malgache (celui de 19 millions et pas celui de 912 personnes) les actions concrètes et immédiates pour la mise en œuvre des accords de Maputo [..] Worried ? En réaction à ce que l’Union Africaine dira ou fera, la troupe à Rajoelina et leurs bandes armées pourraient faire de la résistance[..] Ce 17 mars, je me demande quel monde je trouverais à mon réveil

Satisfied? Only If the African Union is not just posting the list of the penalized perpetrators but also presents concrete and immediate actions to the Malagasy people for the implementation of the Maputo agreement[..] Worried ? Depending on what the AU will decide to say or do, Rajoelina's group and their armed forces may provide resistance [..] On March 17, I wonder in what world I will wake up to

Ninaridhishwa? Hiyo itatokea endapo tu Umoja wa Afrika hauishii tu kutangaza orodha ya hao wanaohusika na mgogoro mzima bali itachukua pia hatua za haraka za kuwasaidia Wa-Madagaska katika kutekeleza makubaliano ya Maputo [..] Kuwa na hofu? Hiyo itategemea na kilie ambacho Umoa wa Afrika utasema au kufanya, inawezekana kabisa kwamba kundi la Rajoelina na vikosi vyao vyenye silaha vikapingana na hatua hizo [..] Mnamo Machi 17, sijui nitaamka na kukuta Madagascar ya namna gani.

Madagoravox anaitamani nchi yenye viwango tofauti, ambayo haitapitia katika mzunguko wa migogoro waliyokwishapitia (fr):

On pourrait aussi rêver d’une action politique qui ne serait le fruit ni de rencontres occasionnelles, ni d’un calcul personnel, ni d’une ambition partisane, mais le fruit d’une morale, d’une éthique qui engagerait pleinement chacun

Mtu anatamani aina ile ya siasa ambayo haitokani na mikutano isiyo na umiliki, tamaa binafsi, au matamanio ya kibaguzi ya vyama, bali aina ile ya siasa ambayo itakuwa ni matunda ya watu kuwa na dhamira ya kushikilia maadili na utu wa mtu.

Ndimby anafikiri kwamba njia ya kweli ya kutoka katika mgogoro huo inaweza kupatikana tu kwa kupitia mazungumzo ya kina kati ya pande mbili adui na si mikutano ya geresha kama ile ambayo imefanyika hapo kabla na iliyoishia kuleta makubaliano kwa nje tu (fr):

L’unilatéralisme ne réside pas dans l’absence ou la présence de débats mais dans le fait que le cadre du débat est déjà dès le départ tellement orienté, qu’il a empêché de parler sérieusement des choses essentielles, et de réunir les personnes qui comptent vraiment dans la résolution de crise

Ufikiwaji wa makubaliano ya pamoja sio hasa suala la kama kulikuwa na mjadala au hapana bali linakuja kutokana na ukweli kwamba misingi ya mjadala tayari ilikuwa imekwishavurugwa kiasi cha kuzuia mazungumzo kuhusu masuala muhimu na papo hapo kuwaweka sawa viongozi ambao kweli wanaweza kuleta ufumbuzi wa kumaliza mgogoro.

Vuguvugu linalojulikana kwa lugha ya KiMalagasi kama “Mitsangana” (kumaanisha Simama) lenye lengo la kuwasukuma wanasiasa kutoka katika vyama vyote kujitokeza na kujibu maswali ya raia wa Madagaska tayari imeanzishwa katika ukurasa wa Facebook.

Wakati ambapo mgogoro unaendelea kuwepo, madhara yake kwa jamii yanazidi kuongezeka. Watoa huduma za afya na madaktari walikuwa kwenye mgomo kwa miezi kadhaa, wakati huohuo wafanyakazi wa viwandani wamekuwa wakijikusanya mbele ya viwanda vinavyopanga kuwafuta kazi ifikapo mwezi Aprili.

 Wafanyakazi wakiwa kwenye mgomo nje ya kiwanda katika jiji la Antananarivo

Wafanyakazi wakiwa kwenye mgomo nje ya kiwanda katika jiji la Antananarivo

(Picha na: kundi la facebook la “Mitsangana”)

Kama ilivyo kawaida katika hali ya namna hii, jamii za vijijini ndio ambazo huathiriwa vibaya na umaskini. Louise, anayetokea Kusini mwa Madagaska, anasimulia na kueleza magumu ambayo mabadiliko mengi ya miaka kadhaa yalivyosababisha kupungua kwa rasilimali za ardhini na jamii za samaki:

Watu huko in Ilafitsignana sasa wameporwa ardhi waliyotumia kulima… Matokeo yake, watu wengi zaidi wamehamia kwenye shughuli za uvuvi, wakati huohuo rasilimali hizi nazo sasa hazitoshelezi … karibu hakuna tena Ambatsi na sâro, fiambazaha bado wapo kidogo lakini si kwa wingi kama zamani… ilikuwa rahisi sana kuwakamata angora lo na varavara zamani lakini sasa hivi karibu wanakwisha…vilevile imekuwa vigumu kupata samaki jamii ya tofoki (mwandishi anadokeza kuwa, maneno yaliyo katika hati mlazo ni majina ya samaki kwa KiMalagasi).

Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, hali ngumu ya uchumi wa Madagaska tayari umeilazimisha serikali kupunguza kiasi cha Dola za Marekani milioni 200 kutoka katika bajeti ya kitaifa ya huduma za jamii. Achille52 anaeleza kwamba mfumo wa elimu ndiyo wa kwanza kuathiriwa na punguzo hilo la bajeti na kwamba jambo hili litakuwa na madhara makubwa sana kwa taifa kwa siku za usoni (fr):

C’est le manque de financement qui est la plaie de l’enseignement publique, les enseignants ne sont pas motivés à cause de leur salaire minable, et les enfants issus de la classe défavorisé ne sont pas assez concentrés. Et si on supprime les aides qui subsistent, où va-t-on ?

Ukosekanaji wa fedha kwa ajili ya shule za serikali ni tatizo kuu. Walimu hawana hamasa ya kutosha kwa sababu ya mishahara duni na hata watoto wanaosoma katika madarasa ya shule hizi hawaweki akili zao kwenye masomo yao tena. Kama tutaondolea mbali ruzuku sasa, je, tunadhani tunaelekea wapi?

2 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.