Habari Kuu kutoka Juni 2013
Habari kutoka Juni, 2013
Rais Obama Kuitembelea Tanzania
Rais wa kwanza wa Marekani mwenye asili ya Afrika, Barack Obama anatarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam kesho alasiri kwa ziara ya kiserikali. Blogu ya Swahili Time imeweka ratiba ya ziara hiyo ya siku mbili. Issa Michuzi aliweka video inayomwonesha Rais Kikwete wa Tanzania akizungumzia ziara hiyo.
Kufilisika kwa Watu nchini Malaysia
iMoney.my wametengeneza mchoro unaoelezea takwimu za kufilisika nchini Malaysia. Wastani wa matukio 20,000 ya kufilisika yamerekodiwa mwaka 2012 hiyo na maana kwamba wa-Malaysia 53 wanafilisika kila siku.
Bahrain: Sheria Mpya za Kudhibiti Huduma ya Skype na Viber
"Tahadhari za Kiusalama" zinatajwa kuwa sababu zilizolazimisha kutungwa kwa sheria mpya zinazoweza kuhitimisha matumizi ya huduma maarufu za Skype, WhatsApp, Viber na Tango nchini Bahrain. Afisa wa serikali alisema utafiti unafanywa kuweza kudhibiti zana tumizi za mawasiliano ya sauti mtandaoni - huduma zinazotumika sana, na zinazosababisha hasara kubwa kwa makampuni ya simu.
Wanaharakati 36 wa Azeri Wakamatwa nchini Iran
Wanaharakati thelathini na sita wa Azeri akiwamo mwanablogu mmoja, Kiaksar, walikamatwa siku ya Alhamisi, 27 Juni katika eneo la Urmia. Vikosi vya usalama viliwaachilia huru wanaharakati hao 300 baada ya kuwahoji kwa masaa kadhaa.
Mwanaharakati wa Haki za Binadamu Nchini Saudi Afungwa Miaka Nane Jela
Abdulkareem al-Khadar, mwanafamilia ya kifalme mwanzilishi wa shirika la haki za binadamu, Chama cha ki-Saudi cha Haki za Kiraia na Kisiasa (ACPRA), alihukumiwa kifungo cha miaka nane jela kwa kosa la uchochezi na kuanzisha shirika la haki za binadamu lisilo na leseni pamoja na mashtaka mengine
Uzuri wa Mlima Everesti Nyakati za Usiku
Sinema fupi za Elia Saikaly zimenasa uzuri mkuu wa Mlima Everesti nyakati za usiku kwa kila sekunde. Anasimulia kwenye blogu yake uzoefu wake wa kupanda hadi kilele cha Mlima Everest kwa mara ya pili.
Raia wa Myanmar Wachukizwa na Mashambulizi Dhidi ya Wahamiaji Wenzao Nchini Malasia.
Vurugu za kikabila nchini Mynmar inaonekana kusambaa hata katika nchi za jirani.. Baadhi ya wahamiaji wa Mynmar wa jamii ya budha wanaoishi nchini Malasia wiki chache zilizopita ambapo watu wengi wanaamini kuwa mashambulia hayo yanahusiana mvutano wa kimakabila na kidini unaoendelea nchini Myanmar. Mwitikio wa awali wa serikali ya Myanmar wa kukanusha matukio haya uliwakasirisha watumiaji wengi wa mtandao.
Athari za Mazingira kwa Uchimbaji Madini Nchini Indonesia
Makala iliyochapishwa katika mtandao wa mongabay.com imefichua athari za uharibifu wa kimazingira ziazotokana na shughuli za uchimbaji madini katika maeneo ya vijiji nchini Indonesia. Baadhi ya wanazuoni wanahofia kwamba maeneo mengi nchini Indonesia yana kiwango cha juu kabisa cha zebaki duniani.
Simu za Bure Kwa Wakulima wa Nigeria?
Wizara ya KIlimo nchini Naijeria imetangaza mpango wake wa kugawa simu za bure za kiganjani kwa wakulima wa vijijini. Mpango huu umezua mjadala mzito kwenye ulimwengu wa blogu nchini Naijeria.
Israeli: Waandamanaji Wakumbana na Ukatili wa Polisi Jijini Yerusalemu
Maandamano yaliyoandaliwa na vikundi vitatu vinavyohusiana na Vuguvugu la Israel la haki ya kijamii (#j14) yalifanyika jijini Yerusalemu mnamo Jumamosi usiku (Juni 8). Waandamanaji walidai kubatilishwa kwa uamuzi wa kuuza zaidi kiasi kikubwa cha hifadhi ya gesi wakati ni asilimia 12.5 tu ya mapato hayo yatakwenda serikalini kama kodi.