Mwanaharakati wa Haki za Binadamu Nchini Saudi Afungwa Miaka Nane Jela

Makala haya ni sehemu ya Habari zetu Maalum: Wanamapinduzi washitakiwa Saudi Arabia

Abdulkareem al-Khadar, mwanafamilia ya kifalme mwanzilishi wa shirika la haki za binadamu, Chama cha ki-Saudi cha Haki za Kiraia na Kisiasa (ACPRA), alihukumiwa kifungo cha miaka nane jela kwa kosa la uchochezi na kuanzisha shirika la haki za binadamu lisilo na leseni pamoja na mashtaka mengine, katika hukumu hiyo miaka mitano itaahirishwa na kutumika tu ikiwa mwanaharakati huyo atashiriki au kuhusishwa na mkutano wowote kinyume cha sheria baada ya kuachiliwa kwake.

Shauri la leo lilifanyika katika mji wa Saudi Arabia, Buraydah na kuhudhuriwa na mamia ya wafuasi wa ACPRA, lakini hakimu hakuruhusu wanawake, akisema kuwa “wanaume wanatosha.”

Shauri la kwanza kusikilizwa katika kesi ya Dk al-Khadar lilifanyika mnamo Februari 20, alipomwomba hakimu kujitoa kwenye shauri hilo kwa sababu ya mgongano wa zamani wa kimaslahi aliwahi kuwanao, lakini hakimu aligoma. Hakimu huyo huyo, Ibrahim al-Husni, awali aliwahukumu waandamanaji wa amani kuchapwa viboko.

Dr. al-Khadar (in the middle) before the beginning of a previous session. Image uploaded by @acprahr

Dr. al-Khadar (katikati) kabla ya kuanza kwa shauri (kesi) ya awali. Picha imepakiwa mtandaoni na @acprahr

Hapo awali mwezi Machi, wanaharakati wengine wawili mashuhuri wa haki za binadamu na waanzilishi wa ACPRA walikutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo cha mpaka miaka 10 na 11 jela kwa “kuvunja kiapo cha utii kwa kiongozi na mrithi wake” na “kujaribu kuzorotesha maendeleo ya nchi”.

Baada ya shauri la leo, mwanasheria wa al-Khadar na mwanachama wa ACPRA Abdualziz al-Shubaily walishikiliwa na vikosi vya polisi baada ya wapelelezi wa polisi kumtuhumu kwa “tabia zisizofaa.” Aliachiliwa muda mfupi baadae:

خرجت قبل قليل من مركز الشرطة الجنوبي بعدما اتهمني فرد من جهاز المباحث بعمل حركات غير لائقه له

@a_abdulaziz300: Niliachiliwa kutoka Kituo cha Polisi cha Kusini baada ya mpelelezi wa polisi kunituhumu kwa kumwonyesha tabia zisizokubalika

Kufuatia shauri hilo, watumiaji wa mtandao wa Twita nchini Saudi walianzisha alama habari: (# أنا _ عضو _ حسم) (Mimi ni mwanachama wa ACPRA), ambapo waliandika majina yao kama hatua ya kutangaza kuunga mkono msimamo na madai ya ACPRA kuhusiana na mabadiliko ya kisiasa.

Makala haya ni sehemu ya Habari zetu Maalum: Wanamapinduzi washitakiwa Saudi Arabia

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.