Bahrain: Sheria Mpya za Kudhibiti Huduma ya Skype na Viber

“Sababu za Kiusalama” zinatajwa kuwa kigezo kilichosababisha kanuni mpya zinazoweza kuhitimisha matumizi ya huduma maarufu za Skype, WhatsApp, Viber na Tango nchini Bahrain.

Magazeti yalimnukuu Waziri wa Nchi anayeshughulikia Mawasiliano Fawaz bin Mohammed Al Khalifa akisema sheria mpya zilikuwa zinaanza kutumika kudhibiti zama tumizi za sauti mtandaoni (Voice Over Internet Protocol), ambazo zimekuwa maarufu sana katika eneo la Ghuba ya Uarabuni, zikitumiwa na mamilioni ya watu wanaobadilishana habari, maoni, picha na ucheshi kila siku ikiwa ni pamoja na kupiga simu na kukutana na marafiki na familia.

Al Khalifa ananukuliwa akisema:

Hatua hizi zinakusudiwa kuhakikisha kuwa hakuna mwingiliano usiofaa wa mila na desturi ikiwa ni pamoja na tahadhari za kiusalama. Ni sehemu ya jitihada zilizochukuliwa na Baraza la Ushirikiano wa Ghuba ya Uarabuni (GCC) kuhakikisha uwepo wa sheria zinazolinda haki za watoaji huduma na kwamba hakuna matumizi mabaya ya zana hizi za mawasiliano.”

Alisema hatua hiyo inakusudiwa kulinda sekta ya mawasiliano nchini humo, akiongeza kuwa utafiti umeonyesha kuwa “watu laki moja nchini Bahrain wametumia zana hizo za mawasiliano ya sauti katika kipindi cha siku nne.”

Bahrain inaonekana kuiiga Saudi Arabia, ambayo tayari imepiga marufuku matumizi ya huduma ya Viber katika nchi hiyo ya kifalme. Saudi Arabia imezuia huduma ya kutuma ujumbe wa moja kwa moja tangu tarehe 5 Juni, 2013, baada ya kutishia kuzuia zana za kimawasiliano, ikiwa isingeruhusiwa kuwapeleleza watumiaji wa huduma hiyo. Huduma nyingine ambazo serikali ya Saudi Arabia inatishia kuzizuia ni pamoja na Skype na hduma ya kutumiana ujumbe wa simu za mkono iitwayo WhatsApp.

Kwa mujibu wa @Comms_BH, akaunti ya mtandao wa twita iliyohakikiwa, inayojieleza kuwa ni ya Wizara ya Ndani inayoshughulikia Mawasiliano:

@CommsBH: Waziri: Wizara inafanya utafiti kwa lengo la kutengeneza udhibiti wa matumizi ya teknolojia ya mawasiliano ya sauti. #Bahrain

@CommsBH: Hatua hizo zinakuja kwa ajili ya kuzuia uvunjaji wa tunu za maadili na utamaduni pamoja na sababu za usalama.

@CommsBH: Sheria na kanuni zinakusudiwa kuhakikisha usalama wa takwimu za kimtandao na kuimarisha usalama wa simu za kimataifa na mitandao ya simu.

Mtandaoni, watumiaji wa mtandao walionyesha mshangao wao kwa habari hizo.

Ahmedroid nauliza:

@albosta: Je, tujiandae kuaga huduma za mawasiliano ya sauti kama #bahrain #skype #asterisk #Twiti iliyopita #viber

Na Rasha Yousif anaongeza:

@RshRsho: Kama @Comms_BH (Wizara) inazuia huduma za viber, tango au Skype ninachoma matairi #Bahrain

Kuchoma matairi na kuweka vizuizi barabarani ni ishara maarufu za kupinga kitu nchini Bahrain, nchini ambayo imekuwa ikishuhudia maandamano karibu kila siku tangu Februari 14, 2011.

Mnamo Machi 12, Siku ya Dunia Kupinga Upelelezi wa Mtandaoni, shirika la Waandishi Wasio na Mipaka (Reporters Without Borders) liliitaja Bahrain kama moja ya nchi tano Maadui wa mtandao wa intaneti -“nchi zinazoingilia mawasiliano ya watu mtandaoni na kusababisha kuvunjwa kwa haki za binadamu.” Nchi nyingine nne ni Syria, China, Iran na Vietnam.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.