Mtu Mmoja Afariki Kwenye Maandamano Yanayoitikisa Brazil

Kijana mdogo aliuawa kwa kugongwa na gari huko Ribeirao Preto na dazeni ya watu kujeruhiwa wakati waandamanaji walipokabiliana na polisi hukoBrasilia, Rio de Janeiro na Salvador pale zaidi ya watu milioni moja walipojitokeza katika mitaa mbalimbali ya miji mikubwa na midogo nchini kote Brazil katika maandamano makubwa ambayo hayakuwahi kushuhudiwa kwa miongo miwili.

Maafisa wa polisi walisambazwa katika miji ya Belo Horizonte na Fortaleza, miji itayokuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la shirikisho la FIFA, ambayo yalisaidia kukabiliana na maandamano ya tarehe 20, Juni 2013.

Pamoja na hali ya machafuko, maandamano mengi yalikuwa ya amani. Katika wiki hii ya pili ya maandamano ya kitaifa, ambayo yalikuja kufuatia kuongezwa kwa nauli za usafiri wa umma, maandamano yalifanyika kwenye zaidi ya maeneo 100 pamoja na kupunguzwa kwa nauli katika miji mingi ikiwa ni pamoja na miji mikuu kama vile Rio de Janeiro na Sao Paulo, kuonesha kuwa “halikuwa tu suala la senti 20”.

VemPraRua Rio de Janeiro

Maandamano huko Rio de Janeiro. Picha na Tomás Pinheiro (CC BY-SA 2.0)

Marcos Delafrate, ambaye ni kijana wa miaka 18, aliuwawa kwenye ajali ya kugongana na kisha kutokomea [pt] , kijana huyu aligongwa kwa gari na dereva aliyejaribu kuendesha gari kuelekea kwenye mkusanyiko mkubwa wa watu 25,000 waliokuwa wakiandamana kwa amani huko Ribeirao Preto, ambalo ni jimbo la Sao Paulo. Kadiri umati huo wa watu walipomzuia mtu huyo aliyekuwa akiendesha gari jeusi aina ya Land Rover, dereva huyo aliongeza mwendo wa gari hilo na kuwapitia watu zaidi ya 12. Video iliyotumwa na mtumiaji wa YouTube ViTvHd2 inaonesha (at 1'40”) tukio hilo na kutoa taarifa kuwa namba za gari hilo ilikuwa ni KVB 6963:

Nchi ipo vitani?

Ugomvi uliopo kati ya polisi na waandamanaji umepelekea mamia ya watu katika miji mbalimbali kujeruhiwa. Katika mji mkuu Brasilia, polisi walianza kufyatua moshi wa kutoa machozi na risasi za mpira kama namna ya kusitisha maandamano pale kundi la waandamanaji wasiokuwa na silaha yoyote [pt] walipotaka kuingia kwenye majengo ya serikali. Kama inavyoonekana kwenye video hii , waandamanaji wachache sana ndio waliotumia silaha kwa kuchoma moto mbele ya Kasri la Itamaraty, ambalo ni makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Nje. video hapa chini inaonesha upande mwingine wa Itamaraty:

Mpakiaji wa video hii, Ocupa Brasilia [pt] alifafanua:

Ao contrario do que a mídia anda veiculado; Uma parte dos manifestantes tentavam mobilizar outros para irem ao Congresso; Sendo que existe duas pontes/entradas e em uma delas tinha uma concentração maior de vândalos. Acabou que todos nós fomos surpreendidos com bombas de lacrimogênio e balas de borrachas; Sendo que um dos manifestantes levou um tiro bem próximo e direto em sua coxa, ficando a bala alojada até que foi levado pelo corpo de bombeiros.

Tofauti na kile kilichokwisha tangazwa na vyombo vya habari vya kawaida, baadhi ya waandamanaji walijaribu kuwashawishi waandamanaji wengine ili wakusanyike pamoja; Kuna mageti mawili, na moja ya mageti hayo kulikuwa na kiasi kikubwa cha uharibifu wa mali. Punde tulishangaa kuona mabomu ya machozi yakitupwa pamoja na risasi za mpira zikifyatuliwa; muandamanaji mmoja aliyekuwa karibu yangu alifyatuliwa kwenye paja lake kiasi cha risasi kubakia pajani hadi pale alipochukuliwa na askari wa kikosi cha zima moto.

Huko Salvador, waandamanaji walikabiliana na machafuko katika matembezi yaliyoanza kwa amani. Maandamano yalibadilika na kuwa machungu pale umati mkubwa wa watu ulipokuwa unalekea Uwanja Mkuu wa Taifa, uwanja ambao timu ya taifa ya Uruguay ilipokuwa inacheza na timu ya taifa ya Nigeria katika kombe la Shirikisho la FIFA. Gari la afisa wa polisi wa serikali ya mtaa lililokuwa na namba OKU 8877, milio ya bunduki ilirekodiwa kutoka kwenye gari hilo– kwa mujibu wa mpakiaji wa video, Felipe Amorim [pt], haikuwa risasi ya mpira. Video hii inaonesha kusambazwa zaidi ya mara elfu pamoja na maelfu ya maoni, miongoni mwa maoni hayo ni ya shuhuda Berlindo Ribeiro Reis, ambaye aliweka bayana kuwa:

eu tava la e vir tudo a Policia desceu a porrada e granada e Bala em todo mundo nao quis nem saber se tinha criança , mulher gravida

Nilikuwepo pale na nilishuhudia kila kitu. Polisi walifika na kuanza kuwapiga watu na kuwarushia watu makombora, hawakutaka kuelewa kama kulikuwa na watoto wala wanawake wajawazito

Huko Rio de Janeiro, ugomvi kati ya polisi na waandamanaji ulitolewa taarifa na wanahabari ambao ni raia. Baadhi ya watumiaji wa mtandao wa intaneti walisema kuwa, silaha halisi zilitumika dhidi ya watu katika meneo mbalimbali ya jiji. Chico Freitas [pt] kupitia mtandao wa Facebook aliripoti:

Houve guerra no Rio hoje. Um milhão de manifestantes. A polícia atacou sem pena, antes de fazermos qualquer outra coisa além de protestar, sem vandalismo. Nos cercaram em todo o centro da cidade. Usaram armas letais e não-letais, fecharam as estações de metrô e oprimiram quem tentava pegar a barca. Jogaram bombas da prefeitura até o sambódromo, nos encurralaram na Avenida Presidente Vargas, conseguimos ir até a Praça Tiradentes e vimos na TV de um bar que o Choque estava indo pra lá. Corremos em direção à Lapa e soubemos que estavam jogando bombas de gás até em crianças que brincavam por lá, então fomos pela Avenida Chile até a Cinelândia. Lá o pessoal se aglomerava de novo, em frente ao Theatro Municipal. Até que se aproximaram os carros do Choque e jogaram bombas. Me perdi do meu pessoal. Corremos todos pro aterro do Flamengo. Lá eu vi o ônibus pra Niterói e peguei. Do ônibus vi que estavam lançando bombas no aterro também. A polícia não vai deixar ninguém ir a lugar algum, aonde quer que o povo vá, eles irão atrás com opressão. Hoje a polícia foi mais violenta do que nunca. Foram truculentos, atrozes, trouxeram medo e terror. A polícia que é paga pra proteger o povo. #protestorj #ogiganteacordou #revoltadovinagre #thegiantwokeup #vemprarua #changebrazil #rio #brasil #brazil

Leo Rio ilikuwa vitani. Waandamanaji milioni moja walijitokeza mitaani. Polisi walishambulia bila ya huruma, kabla hata ya kufanya jambo jingine lolote mbali na kuandamana, hakukuwa na uharibifu wa mali. Walituzingira tukiwa katikati ya jiji. Walitumia silaha zenye uwezo wa kuua na zile mabazo si rahisi kuua, walifunga vituo vya treni za chini ya ardhi na kuwazuia kidhalilishaji wale waliokuwa wanataka kukiwahi kivuko. Waliturushia mabomu, kutoka kwenye ukumbi wa jiji hadi kwenye Sambadrome, walituzuilia kwenye Avenida Presidente Vargas, tuliweza kufika Praça Tiradentes na tukiwa pale, tuliwaona wanajeshi wa kutuliza ghasia kupitia televisheni iliyokuwepo hapo kwenye Baa wakielekea huko. Tulikimbia kuelekea Lapa na tulitambua kuwa walikuwa wakiwarushia mabomu ya machozi hata watoto wadogo waliokuwa wanacheza pale, kwa hiyo tulienda kwa kupitia Avenida Chile kwenda Cinelandia. Mahali pale, walikusanyika tena mbele ya Uwanja wa Manispaa. Magari ya polisi yalipokaria pale watu walipokusanyika, walianza kurusha mabomu, na hapo nilipotezana na marafiki zangu. Sote tulikimbilia eneo la Flamengo. Nikiwa pale, niliona gari la kuelekea Niteroi na hivyo na niliingia ndani ya gari hilo. Nikiwa ndani ya basi, niliona wakiendelea kurusha mabomu ya kutoa machozi. Polisi wasingeweza kuruhusu mtu yeyote kwenda popote. Popote watu wanapotaka kwenda, polisi wangewafuata na kuwaghasi. Leo polisi walikuwa wakatili zaidi kuliko wakati mwingine wowote. Walikuwa watu wa kutaka shari, wakatili kupita kiasi, walisababisha hali ya woga na hofu kuu. Hwa ndio polisi wanaolipwa mishahara kwa lengo la kuwalinda raia. #protestorj #ogiganteacordou #revoltadovinagre #thegiantwokeup #vemprarua #changebrazil #rio #brasil#brazil

Nchi katika hali ya amani

Picha zifuatazo zinaonesha maandamano ya amani katika sehemu mbalimbali za nchi:

Demonstration in Jaraguá do Sul, state of Santa Catarina, photo published by Chan360 (CC BY-NC-ND 2.0)

maandamano ya amani huko Jaraguá do Sul, Santa Catarina, picha ilipakiwa na Chan360 (CC BY-NC-ND 2.0)

Demonstration under rain in Cascavel, state of Parana. Photo by Alexander Hugo Tártari, published with a Creative Commons license.

maandamano yaliyoambatana na mvua huko Cascavel, katika jimbo la Parana. Picha na Alexander Hugo Tártari (CC BY-NC-SA 2.0)

VemPraRua BH

Maandamano makubwa huko Belo Horizonte, Minas Gerais. Picha na Maria Objetiva (CC BY-SA 2.0)

VemPraRua Recife

Recife, Jimbo laPernambuco . Picha na Rostand Costa (CC BY 2.0)

VemPraRua Sao Luis

São Luis, Maranhão. Picha na Kika Campos. (CC BY 2.0)

VemPraRua Natal

Natal, Rio Grande do Norte state. Photo by Isaac Ribeiro (CC BY-SA 2.0)

Maandamano mengine zaidi

Rais Dilma Roussef ameitisha mkutano wa dharura na mawaziri siku ya leo, Ijumaa Juni 21 ili kutathmini madhara ya maandamano hayo na jinsi serikali itakavyofanya majukumu yake kuanzia sasa na wakati ujao. Huku Michuano ya soka ya Kombe la Mabara ikiendelea, maandamano mengine zaidi yamesharatibiwa katika maeneo mbalimbali ya majiji kwa kufanyika siku zinazokuja.

Makala hii imeandikwa kwa ushirikiano na Paula Góes

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.