Habari Kuu kutoka Januari 2010
Habari kutoka Januari, 2010
Rais wa Malawi kutangaza rasmi penzi lake siku ya Valentine
Wamalawi wanatafakari taarifa kuwa mnamo tarehe 1 Mei, rais wa nchi Dkt. Bingu wa Mutharika anatarajiwa kumuoa waziri wa zamani wa utalii Callister Moyo. Harusi hiyo itatanguliwa na sherehe za kitamaduni za uchumba wakati wa siku ya wapendanao ya Valentino tarehe 14 Februari. Wanabloga wachache wamemtakia heri rais katika mapenzi mapya aliyoyapata baada ya kifo cha mkewe Ethel miaka mitatu iliyopita.
Naijeria: Uzoma Okere ashinda kesi dhidi ya jeshi
Nigerian curiosity anaandika kuhusu kesi ya Uzoma Okere huko Naijeria: “Uzoma Okere ni msichana wa Kinaijeria ambaye kipigo alichopata kutoka kwa maafisa wa jeshi kiliondokea kuwa video iliyosambazwa sana na kuamsha hasira za wengi.”
Eritrea: Utawala Ulio Madarakani Uondelewe Haraka
Kwa mujibu wa Mohammed Hagos, mradi wa demokrasi katika Eritrea unapaswa uanze kwa kuuondoa madarakani utawala uliopo sasa: “Kikwazo kinachowazuia watu wa Eritrea kujieleza ni utawala wa Issayas. Njia ya kuelekea demokrasia kwa hiyo inaanza na kuuondoa utawala wa Issayas haraka iwezekanavyo…”
Haiti: Kituo Cha Habari Chazinduliwa Kwa Ajili Ya Uanahabari wa Haiti
Réseau Citadelle anatangaza kuzinduliwa kwa Kituo Cha Habari, mradi unaotoka kwa Wanahabari Wasio Na Mipaka pamoja na Quebecor, wenye lengo la kuwezesha kazi za wanahabari wa ndani na wa nje ambao wako nchini Haiti, na pia kuunda ubia kati ya Asasi Zisizo za Kiserikali na Vyombo vya Habari.
Colombia: Ugumu wa Kutofautisha Wazuri na Wabaya
Kwa kupitia upigaji video wa kiraia, asasi tofauti nchini Colombia zinatoa mitazamo yao kuhusu uhalifu, unyama na migogoro inayohusisha matumizi ya silaha, ambayo ni vigumu kuwatofautisha watu wazuri kutoka kwa wabaya.
Kenya: Kiswahili Kuwa Somo La Kuchagua
Bunmi anaandika kuhusu uamuzi wa kulifanya somo la Kiswahili kuwa la kuchagua nchini Kenya: “Somo hili halitakuwa tena na mtihani wa lazima katika mtihani wa taifa wa darasa la nane…”
Marekani: Dkt. Martin Luther King, Jr. Akumbukwa
Martin Luther King Jr. alizaliwa tarehe 15 Januari, 1929 na akawa mmoja wa wasemaji na watetezi wakuu wa Harakati za Haki za Kiraia huko Marekani. Nchini Marekani, anaenziwa kwa sikukuu ya taifa, inayoadhimishwa kila mwaka siku ya Jumatatu ya tatu ya mwezi Januari. Leo, wanablogu wengi nchini Marekani wanaadhimisha kumbukumbu yake kwa kuandika makala za kumuenzi, huku wakiungalisha urithi wake wa masuala ya haki za jamii na masuala ya leo, wakionyesha wazi kuwa miaka 42 baada ya kuuwawa kwa King, maneno yake bado yana maana.
Haiti: Ramani za Kwenye Mtandao Zaonyesha Uharibifu Pamoja na Jitihada za Kusambaza Misaada
Marc Herman anaziangalia kwa karibubaadhi ya ramani ambazo watoaji misaada wanazitumia ili kuwasilisha hali inayobadilika kila wakati katika maeneo ya tetemeko la ardhi nchini Haiti. Karibu ya juma moja baada ya janga kutokea - na matetemeko yaliyofuatia ambayo yalifanana na matetemeko mengine makuu – ramani na taswira za setilaiti zinajidhihirisha kuwa ni taarifa pekee ambazo zinaweza kutegemewa.
Senegal Yatoa Ardhi ya Bure kwa Walionusurika na Tetemeko la Ardhi
Rais wa Senegal, Abdoulaye Wade, ametawala vichwa vya habari kwa kutoa ardhi ya bure kwa Mu-Haiti yeyote aliyenusurika na tetemeko na ambaye “atapenda kurejea kwenye asili yake” kwa mujibu wa msemaji wake. Kwenye wavuti, tangazo hilo limepokelewa na watu wengi kwa kejeli.
Marekani: Raia wa Haiti Wapatiwa Hadhi ya Hifadhi ya Muda
Hadhi ya Hifadhi ya Muda (inayojulikana kama TPS) ni hadhi maalumu inayotolewa na Marekani kwa raia wa kigeni wanaotoka katika nchi fulanifulani ambamo kunakuwa kumetokea aina fulani ya janga au pigo la karibuni, kama vile vita au tetemeko la ardhi. Jana, Utawala wa Rais Obama ulitoa hadhi hiyo kwa raia wa nchi ya Haiti itakayotumika kwa kipindi cha miezi kumi na nane ijayo. Jillian C. York anapitia jinsi suala hili lilivyopokelewa katika blogu mbalimbali.