Haiti: Ramani za Kwenye Mtandao Zaonyesha Uharibifu Pamoja na Jitihada za Kusambaza Misaada

Hizi hapa ni baadhi ya ramani ambazo wapokeaji misaada ya kibanadamu wanazitumia kuwasilisha hali inayobadilika kila wakati katika maeneo ya tetemeko la ardhi nchini Haiti. Karibu ya juma moja baada ya janga kutokea – na matetemeko yaliyofuatia ambayo yalifanana na matetemeko mengine makuu – ramani na taswira za setilaiti zinajidhihirisha kuwa ni taarifa pekee ambazo zinaweza kutegemewa.

Mtandao wa Ushahidi umetengeneza ramani shirikishi inayotanda juu ya taarifa za vitisho, watu wanaohitaji misaada, huduma za matibabu, chakula pamoja na misaada mingine. Ramani hiyo inaendelea kuwekwa habari mpya kadri habari zinavyopokewa kwa kupitia mtandao wa ushahidi, Twita na fomu zilizo kwenye wavuti. Erk Hersman wa Ushahidi, alisema katika barua pepe kuwa mfumo wa usghahidi ulikuwa unashughulikia zaidi mawasiliano ya Twita na ya kwenye wavuti katika siku za kwanza za tetemeko, kwani mitandao ya simu za mkononi ilikuwa haipatikani katika sehemu kubwa ya kusini mwa Haiti. Hali hiyo inabadilika na huduma ya simu za viganjani, ambayo imeenea katika sehemu nyingi zaidi, “inaleta taarifa nyingi zaidi.”

Crisis Commons, mtandao wa wataalamu wa teknolojia ambo hutengeneza zana kwa ajili ya misaada ya dharura, imetangaza kuwa inaendesha mradi unaofanana ambao unaweka kwenye ramani jitihada zote za usambazaji misaada na kutengeneza ramani maalum ya janga inayoonyesha mahitaji ya mji mkuu wa Haiti, Port au Prince, ili kuyawezesha mashirika ya misaada kuitumia ramani hiyo kama nyenzo ya kufanyia mipango. Mradi huo ndio kwanza umeanza.

Mjini New York, Maktaba ya Mji wa New York una mfululizo wa ramani kwenye wavuti unaoonyesha kambi ambazo walionusurika wanahamia. Jozi ya pili inatambulisha maeneo na majengo yaliyoharibika. Ramani hizo zinahaririwa na kuwekewa habari mpya.

Taswira nyingine nyingi siyo shirikishi, lakini pengine zinatoa mtazamo mpana kuhusu hali ilivyo. Taswira hii kutoka katika Kituo cha Setilaiti cha Habari Zinazohusu Majanga inapima umbali kutoka kwenye kitovu cha tetemeko hadi kwenye maeneo waliyokuwa wakii shi watu kablka ya tetemeko huko kusini mwa Haiti. Ramani hiyo inatofautishwa kwa rangi ili kuonyesha uwingi was watu katika maeneo hayo.

Kwa mujibu wa ramani, na japokuwa halijatambulishwa rasmi kwa jina kwenye taarifa nyingi za habari , Jimbo la Leogane huko Haiti ndilo lilikuwa kitovu cha tetemeko, na lina sehemu kadhaa zinazokaliwa na watu wengi. Carrefour, kitongoji kikubwa cha jiji la port au Prince, kipo kwenye mpaka na jimbo la Leogane. Mji wa Jacmel, kwenye mwambao, pia umo ndani ya jimbo la Leogane na umeharibiwa vibaya. Mpaka kufikia jana, barabara na madaraja yaliyobomoka viliendelea kulitenga eneo hilo na shughuli za kupokea misaada, jiji ambalo lipo karibu zaidi na kitovu cha tetemeko kuliko lilipo jiji la Port au Prince.

Utafiti wa miamba wa Marekani umeweka taarifa za miji kulingana na uwingi wa watu katika jedwali linalosomeka kirahisi kwa kutumia rangi zinazoonyesha ukubwa wa tetemeko. Matokeo yake ni urahisi wa kuelewa ni idadi gani ya watu waliokuwa wakiishi katika maeneo yaliyoathiriwa zaidi na janga hili. USGS (Utafiti wa miamba wa Marekani) pia umeweka ramani ya taarifa za tetemeko ambazo imezipokea kwa njia ya simu. Inaonyesha mitazamo ya watu waliopiga simu kwenye kituo hicho cha utafiti kueleza yale waliyoyaona.

Gazeti la NYTimes limetengeneza ramani ya pande tatu yenye ufanisi mkubwa katika kuelewa ni wapi mji wa Port au Prince ulipo kiuhusiano na miamba ya Haiti. Inaonyesha mji huo katika pwani chini ya milima ambayo inakwaza usambazaji wa misaada. Ramani hiyo ya gazeti la Times pia inafafanua wazi kabisa maeneo ya vitongoji kadhaa ambapo usambazaji wa chakula na madawa umeanza, na ambapo makazi ya muda yameanza kutolewa.

Taswira za moja kwa moja za setilaiti zinapatikana hapa. Taswira za mhimili zilizochukuliwa jana zinalinganishwa na taswira za jiji la Port au Prince na mazingira yake kabla ya tetemeko, kama vile hii hapa.

Muonekano wa picha za setilaiti unaweza kuthibitisha uharibifu na mahitaji katika maeneo ambayo bado hayana mawasiliano ya uhakika. Kwa nadharia, taswira za usiku zinaweza kutuambia mambo yanayofanana kuhusiana na upatikanaji wa umeme, taa, nap engine mafuta. Hata hivyo, ikiwa taswira hizo zimeshaanza kutumika, mpka hivi sasa bado hazijawekwa hadharani.

Kwa habari za zaidi juu ya tetemeko la ardhi la Haiti, tembelea ukurasa wetu maalum kuhusu tetemeko hilo la ardhi.

Picha iliyotumika katika makala hii, Day 15 – Small World, imepigwa na kylebaker, na imetumika kwa idhini ya creative Commons. Tembelea mkondo wa picha wa kylebaker.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.