Habari Kuu kutoka Juni 2015
Habari kutoka Juni, 2015
Abel Wabela: “Kupambana na Hali ya Kutokuchukua Hatua na Kutojali…Hii Ndio Nia Yangu Kama Mwanadamu”
"Maangalizo, vitisho, kukamatwa na mateso hakujanifanya kuacha kutumia haki zangu za msingi za kujieleza," anasema Abel Wabela, mmoja wa wanablogu wa Zone9 wa nchini Ethiopia ambao walifungwa gerezani tangu Aprili 2014.
“Hatuwezi Kukandamiza Utu wa Wengine bila Kuukana utu Wetu Kwanza
Kosa la wanablogu wa Zone9' ati lilikuwa ni kuthubutu kuonesha dhamira yao ya kuupigania "Ubuntu". Waliihamasisha jamii yao kuachana na dhana ya ubinafsi
Mradi wa Picha Waelezea Maisha Nchini Nepali Baada ya Kutokea kwa Tetemeko la Ardhi
Mradi wa pamoja wa Picha unaoendeshwa kuptia Instagram na Facebook unakusanya maisha mbalimbali ya kila siku Nchini nepali kufuatia matetemeko mabaya ya ardhi ya hivi karibuni.
Wanawake Wanaovaa Nusu Uchi Wataiokoa Sekta ya Utalii Kenya?
Je, kutembea uchi yanaweza kuwa mbinu bora ya kufufua sekta ya utalii nchini Kenya kufuatia mashambulizi ya wanamgambo wa Al Shabaab?: Seneta mteule, Mbura anasemekana kuwaomba wanawake katika mkoa wa pwani kutembea nusu uchi ili kuwavutia watalii zaidi kuzuru eneo hilo. Wito huo umeibua maswali kuhusiana na thamani ya mwanamke...
Afrika Kusini Yakumbuka Mashindano ya Kombe la Dunia 2010 Yalivyokuwa
Mnamo Juni 11, 2010, Afrika Kusini ilikuwa mwenyeji wa mashindano makubwa ya michezo duniani. Ni mara ya kwanza kwa mashindano hayo kufanyika barani Afrika.
Shughuli Husimama kwa Muda Waziri Mkuu wa Pakistan Anapotembelea Jiji la Quetta
Kwa mujibu wa makadirio, mamia ya maelefu ya raia wanaathirika moja kwa moja au kwa namna moja au nyingine kila barabara zinapofungwa kwa sababu za usalama wa watu maarufu wanapokuwa Quetta
Raia wa Uganda Wanataniana kwa Mgogoro ‘wa Kawaida’ wa Awamu ya Tatu Burundi
Maandamano makubwa na mapinduzi yaliyoshindwa vyote vlitokea kwa sababu ya Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza kutaka kugombea kwa awamu ya tatu. Rais wa Uganda anaangalia uwezekano wa kugombea muhula wa tano.
Baada ya Maandamano Burkina Faso na Burundi, Naija na Togo Zinafuata?
Wanaija 20,000 wameingia mitaani mjini Niamey, Naija mnamo Juni, 6. Kuna ababu nyingi za maandamano hayo: umaskini uliokithiri, utawala mbovu na kubanwa kwa uhuru wa kujieleza yakiwa ni moja wapo ya malalamiko ya asasi za kiraia nchini humo. Maandamano kama haya yalitokea katika nchi za Burkina Faso, Burundi na Togo....
Kwa nini Tarakimu 64, 89 na 535 Hazipatikani Kwenye Mtandao wa Intaneti China?
Leo ni Juni 4, maadhimisho ya 26 ya maandamano ya kudai demokrasia ya Tiananmen mwaka 1989. Katika miaka ya hivi karibuni, baadhi ya tarakimu zimepotea kwenye mtandao wa Intaneti nchini China kwa sababu ya udhibiti wa taarifa. Tarakimu hizi ni 64, 89 na 535 —zenye kuunganisha kupata Mei 35, namna...
Kampeni ya Kujipiga Picha Yaongeza Uvumilivu wa Kidini na Kupunguza Ukabila Nchini Myanmar
"Yeye ni Msikh na mie Mwislamu. Lakini tu marafiki. Ingawa tuna tofauti zetu, bado tunaweza kuzungumzia mitazamo na imani zetu, na kuzikubali na kuziheshimu tofauti zetu."